Rwanda ni kanchi kadogo sawa na mkoa wa Dodoma, lakini kana watu 12m+, eastern Congo kuna banyamulenge wengi sana (watutsi waliolowea) ambao hutamani kuimega congo ili iongeze ardhi kwa Rwanda. kuna siku eastern Congo itakuja kujitenga na kuwa part of Rwanda kama ilivyo kwa majimbo yaliyo mpakani mwa urusi kujimega toka ukraine. siku zoote hata iweje, hiyo ni sera ya Rwanda hawatakuja kuiacha hadi wafanikiwe kwasababu ina maslahi mapana kwa nchi. Dawa yao ni kupeleka JWTZ, na samia aachane na kagame, tuwe karibu na burundi na wakati huohuo m7 anaendelea kumbana paka abaki peke yake.
sasaivi dr congo imejiunga na East AFrica community, hivyo DR Congo wakiwa pamoja sana na Burundi, Tanzania, Kenya na kwa mbaali Uganda, Rwanda atabaki peke yake na ataona hamna namna ila kuwa na adabu tu. Tanzania tungekuwa ni nchi kubwa kidunia kama zilivyo hizo zinazopigana huko, tulikuwa na sababu ya msingi sana kwenda kuweka base yetu Congo, na Congo wangekubali kwasababu wanatukubali sana. sema ndio hivyo, nchi yenyewe hata bajeti ya jeshi ni ya 3rd world country.