DR Congo yaivuruta Rwanda Mahakama ya Kimataifa ICJ ikiituhumu kufadhili Waasi wa M23

DR Congo yaivuruta Rwanda Mahakama ya Kimataifa ICJ ikiituhumu kufadhili Waasi wa M23

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa imefungua kesi dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ikilalamikia mchango wa nchi hiyo katika mgogoro wa muda mrefu mashariki mwa Kongo.

DRC inaishutumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi wa kikundi cha M23, ambao kwa sasa wanadhibiti maeneo makubwa upande wa mashariki.

Kwa upande mwingine, Rwanda nayo inadai kuwa DRC inapigana bega kwa bega na kundi la FDLR—kikundi chenye makazi yake nchini Kongo kinachoundwa na baadhi ya watu walioshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Mgogoro huu wa miongo kadhaa una mizizi yake kwenye mauaji hayo ya kimbari, baada ya makundi yaliyohusika kukimbilia ng’ambo ya mpaka na kuingia Congo.

Ingawa viongozi wa nchi zote mbili walitia saini makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani huko Washington mwaka 2025 ili kupunguza mapigano kwenye mikoa hiyo ya mashariki mwa DRC mambo yamebadilika. Katika

Soma pia Marekani yaituhumu Rwanda kukiuka makubaliano ya Amani ya DRC yaliyosainiwa Washington

Taarifa iliyotolewa na DRC imeishutumu Rwanda kwa kukiuka mikataba ya kimataifa, ikiwemo ile inayohusu mauaji ya kimbari, ubaguzi wa rangi, na utesaji.

DRC inasisitiza kuwa makosa hayo yaliyofanywa dhidi ya raia kwa muda wa miongo mitatu sasa, yanajumuisha mauaji ya halaiki, mauaji ya kiholela, utesaji, ukatili wa kijinsia, na kuwalazimisha watu kuyahama makazi yao. Kutokana na hayo, DRC inaiomba mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa kuiamuru Rwanda isitishe ukiukwaji huo na kutoa fidia kwa serikali pamoja na wahusika wa mapigano hayo.

Hadi sasa, serikali ya Rwanda haijatoa majibu ya haraka kuhusu hatua hiyo na imekuwa ikikanusha mara kwa mara madai ya kwamba inasajili au kusaidia makundi yoyote ya waasi yanayofanya oparesheni zao nchini DRC.


1782542877500.png

=============

The Democratic Republic of Congo said it has filed a case against Rwanda at the International Court of Justice over its role in the long-running conflict in the eastern Congo.

Kinshasa accuses Kigali of backing the M23 rebel movement, which controls large swathes of territory in the east after a ⁠lightning advance last year.

Rwanda, for its part, says the DRC is fighting alongside the FDLR, a Congo-based group that includes remnants of those responsible for Rwanda’s 1994 genocide.

The ‌decades-long ⁠conflict is rooted in the genocide, after remnants of the forces associated with the genocide fled across the border into Congo.

Leaders of the two countries signed a US-brokered deal in Washington last year to de-escalate fighting in the Congo’s restive eastern provinces.

But in ‌a statement on Friday, Kinshasa accused Kigali of breaching international conventions, including those on genocide, racial discrimination, and torture.

It said the alleged crimes, committed against civilians over three decades, included massacres, extrajudicial killings, torture, sexual violence, and forced displacement.

The DRC is calling on the United Nations court to order Rwanda to cease the alleged violations and award reparations to the state and victims.

There was no immediate response from the Rwandan government.

Kigali has consistently denied allegations that it backs any rebel groups operating in Congo.

But UN experts and Western governments have sided with the DRC in finding Rwanda responsible for providing support to M23 militants.

Relations between the two countries is severely strained over the conflict and the filing opens a new legal front in one of Africa’s longest-running disputes.

Source: African news
 
Back
Top Bottom