Je, DRC imeona ni bora kuwa na marafiki wachache wenye tija kuliko kuwa na marafiki wengi wasio na tija, au ipoje?
Habari kamili.
==========
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imetishia kujiondoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iwapo jumuiya hiyo itashindwa kuiwajibisha Rwanda kwa madai ya unyanyasaji katika eneo la Mashariki lililokumbwa na ghasia.
Tishio hilo lilitolewa baada ya Mahakama ya Haki ya EAC kuripotiwa kukubali kuanza kesi dhidi ya Rwanda kuhusu kuhusika kwake na ghasia mashariki mwa DR Congo.
Naibu Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Samuel Mbemba aliutaja kuwa "ushindi wa mahakama kwa nchi yetu".
Mbemba pia aliitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ukatili wa Rwanda mashariki mwa DR Congo.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa likipambana na kundi la waasi la M23 - linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.
Taifa la Rwanda limekuwa likipinga madai hayo ya DRC.
Chanzo: BBC Swahili