Dr. David Bell: Magufuli kukataa lock down nchini Tanzania kuliokoa maisha ya maelfu ya watu

Sweden hawakuweka lockdown na zipo nchi nyingine pia.
Sweden waliweka lockdown kwa wazee hasa kuanzia miaka 70 kuendelea, walitengwa katika makazi maalum. Pia kulikuwa na social distance na uvaaji wa barakoa. Ibada zilizuiwa. Nyingi waliendesha kwa online na watu kusalia majumbani kwao. Shughuli nyingi zilifungwa ikiwepo na migahawa.
Kuna nchi ambazo hawakuwa na full lockdown lakini shughuli nyingi zilifungwa. Mfano Ethiopia walifunga shughuli zote za serikali. Maofisi yalifungwa. Makanisa na misikiti ilifungwa. Pia ilikuwa ni sheria kuvaa barakoa, usipovaa unakula bakora, na hata unaweza fungwa.
Tanzania ilikuwa tofauti, zilizofungwa ni shule pekee, ila huduma nyingine ikiwepo kuabudu iliendelea. Na haikuwa lazima kuvaa barakoa.
 
Kuna dada mmoja mlokole yupo Tegeta. Alikuwa anamsifia Magufuli kuwa kamaliza Corona Tanzania. Mwaka jana mwezi June/Julay mama yake na bibi yake walikufa kwa Corona. Walipishana siku mbili.

Hadi leo hataki kumsikia Magufuli.
Vitu vyengine vinafurahisha kweli sasa Magufuli ana kosa gani hapo? huyo dada kweli chenga.
 
Mimi naongelea total lockdown.
 
Wamepata wapi twakwimu za wagonjwa na vifo wakati ilikua ni siri ya kinjekitile?

Huu ni ugoro full stop.
Takwimu zinakufanya ujue idadi katika wingi wa wagonjwa wenye kuhitaji mashine za kusaidia kupumua, takwimu zinakufanya ujue idadi ya maiti katika wingi misiba iliyopo.
 
Naomba mnisaidie hivi ni dunia nzima ilikua katika lockdown isipokua Tanzania tu?
Nope sweden hakukua na lock down. Nadhani mie nakubaliana na wazo kuwa lockdown kwa TZ pengine haikuwa na umuhimu. Lakini nabakia na msimamo wangu wa kisayansi kupiga chanjo, kuvaa barakoa hususan kwenye maeneo yaliojifunga, msikitini kwenda na mkeka wangu n.k.

Siamini kama kufusha na nyungu au vituguu saumu vitaweza kutuvusha kwenye janga la covid.
 
Magu aliiunganisha nchi ktk vita ya covid 19... Alimuheshimisha MUNGU ktk nchi - kila anaemwabudu Mungu hatutamsahau JPM ! ... Hakika nchi ilhamasika ikaitikia ..ktk dunia iliyochoka kama hii kumtaja Mungu siyo jambo jepesi ( hasa kwa wanasiasa )
 
Jumaapili Kareem!

Huu ukweli hata chadema na Mwenyekiti wa kudumu Mh. Mbowe anajua na alishakiri, kwamba Hayati Magufuli ametufunza ujasiri na udhubutu wa kufanya tofauti.

Najaribu kutazama swala la kukabiliana na Corona naona kabisa bado kuna kivuli cha Hayati kipo nyuma ya maamuzi ya Marais wetu waliobaki.

Si kwania mbaya bali walijifunza kwake na wakaona inalipa ila wao wameboresha kwa aina yao.

Hebu fikiria angekua ni Mh. Mama Corona ilivoingia 2020 nadhani tungepitia njia waliopitia wakenya kwakua mama ni "professionalism " anaye amini katika mlengo wa kimataifa zaidi.

Swala la kukubali chanjo iwe kwa hiari na kuweka masharti/mkazo nafuu kwenye kupambana na maambukizi ya corona ni dhahiri shairi bado wanaenzi ujasiri wa Haiti katika pambano hili.

Hivyo mnyonge tu mnyonge ila haki yake tumpeni.

Note: Mimi sio mataga,sukuma gang Wala team Veronica na Musiba....
#kaziiendeleeeeee
 
Ngoma hiyo, JPM aliicheza kijanja Sana, ki ukweli TZ tunaishi habari ya korona hatuna, ikitajwa kama hivi, ndio tunashituka kuona, aahaaa..! Kumbe tupo Kwenye janga la kidunia la ugonjwa wa korona
 
Hata mimi najuai ni kwa watu ''maalum'' kama wewe. Mimi niko hapa kukuondoa kutoka kwenye hilo kundi la ''umaalum''. Na ndiyo lengo hasa la JF.
Umekosea kidogo. Siko huko.
Sina hakika kama una habari kuwa kuna watu waliaojiriwa kwa kazi maalum ya “kuthibisha kuwa Magufuli alikuwa sawa (right) katika kila alichosema na kuagiza”? Kuwa alikuwa “infallible”? - kama Mungu.
Nina ndugu yangu mmoja siku ya taarifa ya kifo alilia sana kiasi cha kuniduwaza kabisa. Nilipomuuliza kulikoni akanijibu “yaani sasa wale maadui watajisifu kuwa corona imemshinda!” kilio kikaendelea na kuugulia siku nzima!
Hao watu na mada zao hapa JF zinatambulika kwa mtindo wa maandishi, nukuu fake, upenzi wa conspiracies na wanavyopokezana majibu (replies). Hawana haja ya ukweli wala mantiki.
Ukiweza kuwashawishi waachane na ujinga huo litakuwa jambo la heri sana.
 
Asante. Nilikuwa sijakuelewa na samahani.
 
Akina Kigwa wako wengi . Mwandishi nae kafuata hisia Zake badala ya fact.
POSHO ZA WIZARA YA FEDHA MWEZI MARCH,APRIL NA MEI.

Tarehe 31/03/2021 Shilingi 251,000,000/= (kazi maalum)

Siku hiyo hiyo tena tarehe 31/03/2021 Shilingi 198,000,000/=

-Mwezi April ilikuwa balaa.

Tarehe 08/04/2021 Shilingi 44,500,000/=

Tarehe 13/04/2021 Shilingi 155,295,000/=

-Tarehe 30 April nayo ilikuwa balaa

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,900,000/= (kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 14,400,000/=
(siku ya wanawake)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,000,000/=

Mei mosi siku ambayo sio ya kazi.

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi asubuhi Shilingi 184,100,000/=

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi Mchana Shilingi 264,000,000/=

Tarehe 03/05/2021 Shilingi 146,500,000/=
(Kuandika mpango Kazi wa manunuzi watu 125 [emoji3])

Siku hiyo hiyo tena Shilingi 171,200,000/=(kuandaa nyaraka za bunge)

#WeMissYouJPM.
#Tunakukumbuka JPM.
 
Appropriate use of face masks is important. The face mask should completely cover the face from the bridge of the nose down to the chin. Clean hands with soap and water or alcohol-based hand sanitiser before putting on and taking off the face mask. When taking off the face mask, remove it from behind, avoiding to touch the front side. Dispose the face mask safely if it is disposable. Wash your hands or apply alcohol-based hand sanitiser immediately after removing the face mask. Washable, reusable face should be washed as soon as possible after each use, using common detergent at 60 °C. Campaigns for the appropriate use of face masks may improve the effectiveness of the measure.
 
Walimu 90,000 wa wapi hao!!?
Kwa nini mnakuwa waongo kama baba yenu baba wa uongo!?
 
Hajasema vifo vya uviko-19, bali ukosefu wa chakula na lishe, hususan ni kwa watoto. Muwage mnasoma kabla ya kutoa maoni.
CC: Daudi Mchambuzi

Issue hapa ni tradeoff, kwamba umepoteza wangapi na umeokoa wangapi.

Sasa kama takwimu za waliopotea hazipo, huwezi jua labda corona ilitambaa na wengi zaidi ya walio okolewa.
 
Watakubishia na hili pia😡!
 
Naomba mnisaidie hivi ni dunia nzima ilikua katika lockdown isipokua Tanzania tu?
Hapana, zipo nchi nyingi tuu ambazo hazikuwa katika lockdown duniani, pamoja na nchi zilizoendelea sana kama Sweden na kadhalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…