joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Mimi huwa ninafuatilia sana mazungumzo na kusoma makala za wasomi mbalimbali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati, lakini katika eneo la uchumi sijawahi kuona mtu yeyote anayemkaribia huyu jamaa.
Haya mazungumzo kuhusu SGR, KQ, LAPSET, Lamu port, kiwango kidogo cha mafuta yaliyogunduliwa Kenya na kutokuwepo kwa umakini wa viongozi wa Kenya katika kuanzisha miradi, aliyasema na kuyapigia kelele sana miaka 4 iliyopita, Leo hii yote aliyosema yametimia.
Sehemu ambayo amenigusa sana ni pale aliposema kwamba "Uwezo wa viongozi wa Kenya katika kujadili kwa undani wanapoanzisha miradi haupo tena, badala yake wanaanzisha kwa mihemuko ya kufuata mkumbo " Flag ship projects ".
Msikilize kwa makini sana, kisha na wewe uweke maoni yako hapa JF.