Tukubali ama tusikubali Material matters. Kwa wale ambao kipindi cha kama miaka 4 iliyopita ambao walikuwa kwenye sekta ya utalii watakuwa mashahidi. English amabayo hawa tuwaitao tour guides waliyokuwa wanaongea, ni balaa tupu. Kwa mwelewa wa lugha hii na bahati mbaya ukawa ni mtanzania basi utavunjika mbavu! mfano unaweza msikia mtu akijitambulisha kwa mgeni (naomba maguides mnisamehe) "Your may name is Juma and you?" ama anamwambia mgeni " this is elephant toilet" unashangaa ana maana gani huyu! lakini kwa wenzetu wazungu hawako kwenye grammer tunazosema sisi bali wamelenga zaidi kuwa unataka kusema nini hapa. Then wanapata wakitakacho wanaendela mbele. Hata wao wageni huwa wanakosea tu kiswahili chetu. Wakati fulani niliwahi kuwaambia watu fulani kuwa wanajua kiingereza sana ila wana uoga wa kukiongea ndio maana wanakuwa bubu. Walipoanza kuvunjavunja hiyo lugha sasa wanaongea as if wako kwa malkia. Pia kuna tofauti ya kiinglishi cha kuandika na kuongea. Hata kiswahili, tulipokuwa huko kijijini tulikuwa tunawahara sana waliotoka mjini kuwa wanajua kiswahili, lakini njoo kwenye kuandika hicho kiswahili! Hawakuwa wanaona ndani, tuliwaacha mbali sana. Final MATERIAL MATTER THAN ALL THAT BOMBASTIC AND GRAMMER THAT WE ARE TALKING ABOUT.
Nionavyo mimi.