Dr. Hildebrand Shayo

Dr. Hildebrand Shayo

Nyani Ngabu,

..nilivyoona jina la Philip Emeagwali almanusra nianguke kwenye kiti. nikakumbuka jinsi alivyochambualiwa na Raj Patel.

..kama ni kusoma mbona wako madogo kibao wana PhD nzito-nzito, wengine wana ma-patent na mazagazaga kibao?

Classic stuff
 
shayo.jpg


Leo Aprili 4, 2012, si kuwa naomba kura kwa Wabunge wa CCM, kwani mchakato wa uteuzi kwa hatua tuliyofikia imekamilishwa kutokana na taratibu zinazokubalika ndani ya chama cha Mapinduzi.


Leo, badala yake, napenda kutoa kura ya shukrani. Mimi kumshukuru Mheshimiwa Pinda waziri Mkuu na Mbunge ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao, Mheshimiwa Abdulrahaman Kinana mwakilishi wa CCM, wapinzani wangu katika kuwania kuteuliwa kwenda kwa wabunge kupigiwa kura yaani:

Janeth Mmari, Janet Mbene, Fancy Nkuli, Narah Mukabi, Shally Raymond, Shyrose Bhanji, Ngollo Malenya, Godbertha Kinyondo, Hamida Kalua, Angela Kizigha, Happyness Lugiko, Ruth Msafiri, Dr. Aman Kabourou, John Ngongola, Dr. Evans Rweikiza, Siraju Kaboyonga, Bernard Murunya, Dr Edmond Mndolwa, Christopher Awinia, Charles Makongoro Nyerere, Adam Kimbisa, Elibariki Kingu, simon Berege, Mrisho Gambo, Handley Mafwega, William John Malechela, Mussa mnyeti, Godfrey Mosha, Septuu Mohamed Nassor, Safia Ali Rijaal, Rukia Seif Msellem, Sahan Saleh Ali, Maryam Ussi Yahaya, Dr. Said Gharib Bilal, Abdalla ali Mwinyi, Dr Haji Mwita haji, Dr. Ahmada Hamad katib, Zubeir Ali Maulid, Khamis Jabir Makame, Abdlul azizi salim AbdulAziz na Mbwana Yahaya Mwinyi na wafanyakazi wengine ya wafanyakazi kutoka makoa madogo ya CCM Lumbumba, na kwa marafiki zangu wote ambao kwa namna moja au nyingine wamefanya kazi katika kuniwezesha kuanza safari hii kisiasa ndani ya Chama Tawala CCM na kufikia ngazi katika mchakato huu wa Bunge la Afrika Mashariki.

Japo sikuweza kufikia kuwa kati ya wale watakaopelekwa kupigiwa kura na wanbunge nzima kule Dodoma mwaka huu, kwa hakika, ninaelewa kuwa ni kutokana na upepo wa Kisiasa ndani ya chama chetu.

Waheshimiwa wabunge [CCM], nawashukuru kwa ajili ya mawazo na kwa ajili ya kura zenu, na kukubali kwenu kunisikiliza na kunikubali mimi kama damu changa katika chama ukizingatia misukosuko ambayo chama chetu cha CCM kinapitia unaojionyesha kutokana na chaguzi mbali mbali za hivi karibuni katika ngazi mbali mbali.

Tukio la jana na nafasi niliyopata kubadilishana mawazo na wabunge wakongwe na ambao wengi wao wamewahi kushika nafasi kubwa serikalini, Mawaziri, na utaratibu mzima wa kupewa nafasi ya kuhojiwa na mazingira mazima ya ukumbi wa Karimjee, itakuwa kumbukumbu ya mara kwa mara kwangu mimi na kwamba chama changu CCM ni chama chenye wagombea wazuri na wenye uwezo mkubwa.

Dkt. Hildebrand Shayo
 
Right here Ngabu...
Jana ulinikatili nilikuwa na shauku ya kumuulizia 'mgombea wako' maana niliona Billy tu anachambuliwa ...lol

Oooh vizuri. Sasa hebu rudi nyuma hadi ukurasa namba 8 usome madudu yake
 
Huyu nae alikuwa anagombea ubunge wa Afrika Mashariki lakini amepigwa chini.
Shukran sana mkuu kwa hii taarifa maana nilikuwa na shauku
 
Hata bwa'mdogo Makamba naye keshawahi kukamatwa na article za watu....
duuuh hii kubwa kuliko...sasa nimepata picha halisi ya kwanini ulitikisa kichwa alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa EAC

Hehheee bwan'makamba naye nimeona kashfa huku...daah nyie watu mlikuwa wabaya aisee...

I am more curious now...
 
duuuh hii kubwa kuliko...sasa nimepata picha halisi ya kwanini ulitikisa kichwa alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa EAC

Hehheee bwan'makamba naye nimeona kashfa huku...daah nyie watu mlikuwa wabaya aisee...

I am more curious now...

Si umeona hiyo ya article ya Valentine's day? Hiyo aliibandikaga kwa Michuzi watu wakamkamata. Kwa jinsi alivyo serial plagiarist..mwaka jana au juzi kama sijakosea...akabandika tena makala ingine huko huko kwa Michuzi...kumbe bana hiyo makala hakuiandika yeye....aliitoa kwenye gazeti moja huko Egypt na kujifanya kama yeye ndo kaiandika.

Neno likaenea na mhariri wa hilo gazeti akamuandikia Michuzi na kumchimbia biti kuhusu kubandika makala za wizi zisizo acknowledge waandishi original. Michuzi akaja kuiondoa hiyo makala.

Sasa huyo ati naye ni "Dr.".
 
Si umeona hiyo ya article ya Valentine's day? Hiyo aliibandikaga kwa Michuzi watu wakamkamata. Kwa jinsi alivyo serial plagiarist..mwaka jana au juzi kama sijakosea...akabandika tena makala ingine huko huko kwa Michuzi...kumbe bana hiyo makala hakuiandika yeye....aliitoa kwenye gazeti moja huko Egypt na kujifanya kama yeye ndo kaiandika.

Neno likaenea na mhariri wa hilo gazeti akamuandikia Michuzi na kumchimbia biti kuhusu kubandika makala za wizi zisizo acknowledge waandishi original. Michuzi akaja kuiondoa hiyo makala.

Sasa huyo ati naye ni "Dr.".

Hivi mtu anakuwa anafikiria nini hasa ku plagirize tena si mara moja?

no wonde kila mtu 'DR'...
Tunakimbizana na wanaigeria kwenye 'elimu za kisanii'
 
Naomba irejeshwe SIASA

huyu naye inabidi akaangwe kma wenzie
 
habari za kuaminika za hivi punde zinasema kwamba, Dr. shayo (US blogger) a.k.a Kawawa ndiye yule aliyemvamia mashaka kwa michuzi. Habari hizi zimepatikana baada ya Daktari kutuma barua pepe kwa bahati mbaya au nzuri kwa mtu ambaye hakuwa mlengwa

Habari hizo zimeendelea kusema kwamba, shayo amejigamba kwamba mdahalo kati yake na mashaka lazima ufanyike kwa sababu tayari wanahabari wake wameanza kumfatili mashaka ili kumshawishi kushiriki.

Mzee mzima dakta, pia ameonyesha shauku ya kugombea ubunge katika bunge lijalo

Kama hizi habari ni za kweli, basi jamaa takuwa amejidhalilisha sana.

Duh! Nilikuwa najiuliza huyu US blogger ni wa wapi ana maringo hivyo?
 
Hivi mtu anakuwa anafikiria nini hasa ku plagirize tena si mara moja?

no wonde kila mtu 'DR'...
Tunakimbizana na wanaigeria kwenye 'elimu za kisanii'
Chuo alichopta PhD full waNaigeria labda ndio alikojifunzia
 
Siku hizi kuna nyenzo kibao ambazo ni freely available on the internet zinazoweza kugundua ishara za academic dishonesty in the form of plagiarism. With that being said, nyie doubters au pengine watetezi wa huyo "Dr." tafadhali mtuwekee Phd thesis yake tuifanyie uchunguzi wa kina kufahamu kama aliiba maandaishi na utafiti wa Wasomi wengine.
 
Back
Top Bottom