Dr. John aliwahi 'kuwachana' UHAMIAJI

Dr. John aliwahi 'kuwachana' UHAMIAJI

You nailed it. Yeah ROMA alikosea kuwa 'too vocal' na mbaya zaidi akajisahau akaexpose 'political alignment' yake. Katika hizi harakati ni vyema ukawa unaikosoa serikali WITHOUT revealing your political affiliation.

,Mfano hawa Wagosi, tangu waanze sanaa wametoa pini nyingi sana za kuikosoa serikali. Lakini katika mashairi yao yote hawaoneshi 'umahaba' wa kisiasa. Yani wanaichana sana serikali lakini huwezi kujua wanasapoti chama gani cha siasa. Huwezi hata sikia wakichana kwa kutaja real names/identity za viongozi wanaowachana. Huchana na kukosoa/kuponda kwa ujumla wa sekta husika.

Roma yeye kwenye hili alipitiwa.

-Kaveli-
Heshima kwako!!

Wewe Ndio umehitimisha haswa,
Sijui hili hakuliona kupitia kwa wakongwe wengine wanaofanya harakati hizi au alikuwa anafahamu akamua kama mbwai na iwe mbwai.


Huwa si kitu kizuri sana kama msanii/mchezaji wa soka kuyaweka mahaba yako mbele ya Siasa(chama)na kuyaonyesha katika Jamii hii inakubidi uchague aidha ubaki katika kipaji chako au uingie katika siasa moja kwa moja.
 
Mpaka sasa manesi wananyodo kibao.Tehe tehe!!

Walikuwa wanapazaa sauti na kusaidiana na watu wanyonge wasio na uwezo wakuanika uozo na utendaji mbovu wa sekta hizi za bongo.
mmenikumbusha nilipokuwa na mgonjwa wangu MOI yaani wimbo wa manesi ulikuwa unaweka na wagonjwa hadi unaogopa! na manesi wanasikiliza vizuri bila wasiwasi!
 
mmenikumbusha nilipokuwa na mgonjwa wangu MOI yaani wimbo wa manesi ulikuwa unaweka na wagonjwa hadi unaogopa! na manesi wanasikiliza vizuri bila wasiwasi!
Mkuu,
Hii ndio Tanzania Taifa la bongo.
 
mmenikumbusha nilipokuwa na mgonjwa wangu MOI yaani wimbo wa manesi ulikuwa unaweka na wagonjwa hadi unaogopa! na manesi wanasikiliza vizuri bila wasiwasi!


Huo wimbo 'Wauguzi' huwa ni mwiba sana kwa manesi na madaktari, japo huwa wanajifanya makauzu wanapousikia.
Kuna kipindi back in days serikali iliufungia. Ni nadra sana kuusikia hewani.

-Kaveli-
 
Hawa jamaa wanajua, sema nyota tu imegoma!!


Nyota yao imegoma haswaaa, miaka na miaka bado media inawabania sana. Na wala hawachoki kutoa mawe... dizaini kama weshaamua to do for fun & fans, not fame!

Juzi wamepakua jiwe lingine 'UPEPO SIO'.

-Kaveli-
 
Nakubaliana nawe mkuu. Wagosi ndo wasanii pekee waliobakia kuikosoa serikali kupitia sanaa. Na ni kama wapo 'makini' fulani hivi katika uwasilishaji wao wa sanaa. Huwa wapo 'non-alignment' kwenye mambo ya kisiasa, nadhani hii pia imewasaidia sana kwenye music mileage yao. Japo waliwahi kufungiwa ule wimbo wao uitwao 'Wauguzi'.

Ukisikiliza nyimbo zao kama: Lidandasi, Tanga Kunani, Umeme & Maji, Walimu, Wauguzi, Soka la Bongo, Traffic, Nyeti, n.k zinakumbusha mbali sana.

Roma yeye amekuwa 'too vocal' ... nadhani hii imechangia sana kuonekana 'anaizingua' serekali.

-Kaveli-
Mkuu mimi pia ni mmoja ya wapenzi wa wagosi wakaya since way back,kama utaweza kuatach nyimbo nyengine za wazee wa ndima itakuwa poa zaidi
 
Na hiyo ndiyo mojawapo ya 'essence' za uwepo wa HipHop. To voice out for the people. HipHop lives coz ni utamaduni ambao unazungumzia na ku-voice out juu ya maisha ya kila siku ya mwanadamu, hasa hasa kulisemea tabaka la oppressed community. HipHop ni platform ya kusema na kufichua matatizo mbali mbali yanayowagusa watu wanyonge/masikini. HipHop ni forum inayoelimisha na kuonya juu ya matatizo mbali mbali yanayoiathiri jamii yote kwa ujumla.

Mkuu, ili uelewe vyema ninachokisema, tafuta pini moja iitwayo 'MUDA WA VITENDO' by G-Solo. Ukiucheki/Ukiusikiliza huo wimbo, ndo utapata kuelewa vizuri dhima kuu ya hip-hop (conscious one) kwenye jamii. G-Solo alinyonga sana kwenye hiyo ngoma. Alitumia (sampling) beat kutoka kwenye track ya mtoni iitwayo 'THE G CODE' by Scarface.

-Kaveli-
The G code one of the best hiphop track of all time too bad scarface couldnt have the mainstream success he deserves just like wagosi although he is in the top three list of every rapper.Wagosi nadhani bifu lao na clouds ndilo lililowakosti pamoja na kutojipromote vzr wao na kazi zao
 
Back
Top Bottom