Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Yote hayo ni kutaka katiba penekezwa ipite kiulaini.lakini yaguju! Mamlaka kamili ,zanxibar kwanza muungano baadae
 
Magufuli ni Team Mkapa, Naona Jk anaenda ku-suffer kama alivyomuhenyesha Mkapa mpaka "akamsimamisha" kortini kutoa Utetezi kwenye kesi ya Mahalu.

Kamuhangisha Mkapa wa watu kwenye kamradi kake ka Kiwira mpaka akarejesha Serikalini. Tujiandae kwa Vatalu vya Gesi kadhaa kurudishwa Serikalini, ninaimani mkulu kajimilikisha angalau kisima kimoja pale Mtwara. Ngoja tumsikilizie Magu..!!!

BACK TANGANYIKA
 
Inaelekea Lizaboni ni mtu wa system maana siku nyingi alikuwa akisema rais atakuwa Magufuli. Sijui alijuaje?
 
HV alama hii % unaelewa maana yake au umekurupuka? Asha angepata 59% sio ndo angekuwa mshindi? jf great thinkers,probably

Hivi shule ulimaliza lini wewe? Au ndio wale wa kizazi cha mlugo? Wewe ndio unajiita JF Great Thinker? Unakurupa kuuliza ujinga. Wewe ndio hujui maana ya %.

Ngoja nikufundishe unayejifanya unajua wakati kichwani uko empty. Mtoa mada ameandika Asha Rose Migiro kapata 59%(59/100) ya kura zote. Hii inatoa picha kwamba Asha Rose ndiye mshindi kwa sababu ukipiga hesabu alivuka zaidi ya nusu ya kura.

Cha ajabu zaidi ni pale ilipooneka Magufuli kapata 87%(87/100) na ndio mshindi. Hii tayari inatoa picha nyingine tata kimahesabu. Ukijumlisha percentage za Asha na Magufuli kwa pamoja unapata 146%(146/100). Sijui kwa upande wako wewe mwenye akili unaelewaje.

Lengo ilikuwa ni kuwekana sawa tu ili mada ieleweke na si ilivyoandikwa kwa haraka. Na nafikiri akili yako ndio ilikurupuka kukosoa bila kuelewa.
 
Mimi kwa mawazo yangu nafikiria rais atatoka CCM, basi tuweke nguvu kubwa tupate wabunge wengi wa UKAWA ili serikali isilale.Ni maoni yangu

Unakosea, ukianza na kutanguliza kushindwa hautashinda hata siku moja, japo nakubaliana na wewe kuwa ushindi unaanza na maandalizi. Kama unatamani kushinda wabunge wengi basi tukubaliane kuwa wale wanaotegemea wawapingie wabunge wampigie na rais. Najua wingi wa kura za rais ndio unaoangaliwa wakati wa kujua chama kipi kipate ruzuku kiasi gani. CCM wameweza kupata fedha nyingi na kuwawezesha kuboresha mazingira ya kazi. Angalia ukumbi wao, magari katika ngazi za mikoa na wilaya hivyo kuboresha utendaji kazi wao. UKAWA tunahitaji mazingira kama hayo.
 
Wale missiontown anzeni kutafuta fursa mpya maana 'kupiga deal' kumefikia tamati. Watumishi wa umma badilikeni 'business as usual' ndio bye bye. Wafanyabiashara jiandaeni kulipakodi kwa mujibu wa sheria 'mambo ya hongo' kwishney. Na kwa wachapazi hii ni fursa ya kula 'matunda mema' ya jasho lao. Ahsante na j'pili njema!
 
Wale missiontown anzeni kutafuta fursa mpya maana 'kupiga deal' kumefikia tamati. Watumishi wa umma badilikeni 'business as usual' ndio bye bye. Wafanyabiashara jiandaeni kulipakodi kwa mujibu wa sheria 'mambo ya hongo' kwishney. Na kwa wachapazi hii ni fursa ya kula 'matunda mema' ya jasho lao. Ahsante na j'pili njema!

Huu hakika ni ujumbe mzuri
 
Back
Top Bottom