Dr Joyce Ndalichako ateuliwa kuwa Rais wa umoja wa mabaraza ya mitihani Afrika

Dr Joyce Ndalichako ateuliwa kuwa Rais wa umoja wa mabaraza ya mitihani Afrika

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
[h=3]DR JOYCE NDALICHAKO ATEULIWA KUWA RAIS WA UMOJA WA MABARAZA YA MITIHANI AFRIKA[/h]

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania ( Necta), Dk Joyce Ndalichako, ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Serara Moahi wa Botswana.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuteuliwa kwake, Dk Ndalichako alisema atatumia fursa hiyo kuendeleza ajenda mbalimbali zitakazosaidia kuinua elimu Bara la Afrika.

“Hii ni heshima ya pekee kwa Baraza la Mitihani Tanzania, kipindi cha mwaka mmoja nikiwa Rais wa AEAA nitaendeleza yaliyoanzishwa na mtangulizi wangu, pia kutekeleza ajenda mbalimbali zitakazoleta manufaa kwa nchi yetu,” alisema Dk Ndalichako. Pia, alisema atajitahidi kuwa mbunifu na kupanua ushirikiano na nchi nyingine.

, kuhakikisha anawajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa mabaraza ya mitihani kwa nchi wanachama.

“Kwa mfano kwetu naona changamoto kubwa ni suala la standardisation (kusanifisha alama za mitihani), nitajitahidi kuhakikisha watu wetu wanajengewa uwezo kwenye nyanja hii,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kushauri nchi za Afrika kuhakikisha zinatilia mkazo zaidi kuongeza walimu wa kutosha, walio bora na vifaa vya kujifunzia. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba, alisema kupata cheo hicho ni heshima kwa nchi.

MY TAKE:
WATAKAOKASIRIKA WATAFUTE NCHI YAO WAKAJIFICHE HUKO
 
DR JOYCE NDALICHAKO ATEULIWA KUWA RAIS WA UMOJA WA MABARAZA YA MITIHANI AFRIKA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania ( Necta), Dk Joyce Ndalichako, ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Serara Moahi wa Botswana.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuteuliwa kwake, Dk Ndalichako alisema atatumia fursa hiyo kuendeleza ajenda mbalimbali zitakazosaidia kuinua elimu Bara la Afrika.

"Hii ni heshima ya pekee kwa Baraza la Mitihani Tanzania, kipindi cha mwaka mmoja nikiwa Rais wa AEAA nitaendeleza yaliyoanzishwa na mtangulizi wangu, pia kutekeleza ajenda mbalimbali zitakazoleta manufaa kwa nchi yetu," alisema Dk Ndalichako. Pia, alisema atajitahidi kuwa mbunifu na kupanua ushirikiano na nchi nyingine.

, kuhakikisha anawajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa mabaraza ya mitihani kwa nchi wanachama.

"Kwa mfano kwetu naona changamoto kubwa ni suala la standardisation (kusanifisha alama za mitihani), nitajitahidi kuhakikisha watu wetu wanajengewa uwezo kwenye nyanja hii," alisema.

Alitumia fursa hiyo kushauri nchi za Afrika kuhakikisha zinatilia mkazo zaidi kuongeza walimu wa kutosha, walio bora na vifaa vya kujifunzia. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba, alisema kupata cheo hicho ni heshima kwa nchi.

MY TAKE:
WATAKAOKASIRIKA WATAFUTE NCHI YAO WAKAJIFICHE HUKO

huyu mama ni jembe!
 
Ha! ha! ha! Cheo cha kuteuliwa?! halafu ni cha kuzunguka kila baada ya mwaka?!
...acha wafu wazike wafu wenzao!.
 
Is it a big deal? Hongera zake.
Hatuhitaji sifa kubwa wakati watoto wetu wanaumia (si kosa lake BTW)
 
Si wao walitaka atoke pale baraza la mitihani Tz? Sasa wamepata sababu nzuri za kumwondoa kimya kimya. Nadhani nikwa mtindo huo huo Bw. Masilingi alipata nafasi ya ubarozi na kuondoka jimboni na kumwacha Prof. Anna Tiba akivinjari na kupunguza adui mkubwa kwenye kura za maoni.
 
Ha! ha! ha! Cheo cha kuteuliwa?! halafu ni cha kuzunguka kila baada ya mwaka?!
...acha wafu wazike wafu wenzao!.

pole sana najua hii si habari njema kwa kundi "maalumu" ila ndo hivyo tena Dr JOYCE NDALICHAKO anapaa!
 
Waliberali mtakalia sana lakin habari ndo hiyo!! Polen mnaomchukia Mwanamke kiongozi Jembe kuliko wote Tz.
 
Ni mafanikio gani aliyoyapata nchini katika kazi yake?
 
Hatujui tunakotoka.... hatuwezi hata kutambua tulipo............ sio rahisi kujua tunakoelekea

"Have a nice journey to middle of nowhere....TANZANIA."
 
Katibu wa baraza la mitihani Tanzania Joyce Ndalichako, amechaguliwa kuwa Rais wa Mabaraza ya Mitihani barani Afrika katika mkutano uliofanyika jana jijini Arusha ambapo wadhifa huo hapo awali ulikuwa ukishikiliwa na raia wa Kenya.
 
Safiiiiiii sanaa sis tunamlaumu wakati wenzetu wanatambua kuwa ni jembe
 
.............n rais wa balaza la mitian kwa nchi zinazoendelea afrika hukitoa s.afrika.......🙂
 
Back
Top Bottom