Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

kwa ufupi nadhani wengi hawafahamu kuwa mtihani hautungwi NECTA. Waalimu hawa wanaofundisha mashuleni ndio wanatunga maswali halafu maswali yanapelekwa NECTA kwenye question bank.
Baada ya hapo jopo la kila somo wanachagua maswali na kutunga paper 4 kwa kila somo.
Baada ya hapo jopo lingine linakaa kuangalia hayo maswali kama yanaendana na syllabus na mengineyo.

Basi baada ya hapo linabaki jopo la siri la kuchagua paper ipi ifanywe na wanafunzi.

Sasa mkimlaumu Ndalichako mtakuwa mnakosea maana utungaji mtihani una taratibu zake.

Je kuna jopo linakokaa kuangalia Kama sylabus (inayoendana na huo mtihani) imekuwa appropriately covered kwa shule zote zinazotakiwa kufanya mtihani husika?
 
Sasa jiulize, shule yenye MoU ndio ilijibu hivyo? kama yes, ni ipi?

Mnaumiza bvichwa wakati mambo yapo wazi kabisa.

Misingi ya elimu Tanzania iliwekwa kwa tabaka mvbili, mpja la wale wengi wataofundishwa namna ya kulima na jembe la mkono, kufagia na kuosha vyoo, tabaka hili halina siri, tnawaona wanafunzi wakibebeshwa majembe ya mkono, mafagio ya kuoshea uwa na vyoo na makopo ya maji. Tabaka la pli ni lile linalotayarishwa kuwa watawala na hawa shuleni kwao huwakauti wakibebeshwa fagio wala jembe la mkono wala makopo ya maji ya kusafishia vyoo.

Sasa jiulize ni shule zipi hizo?

Kwa hesabu zangu, waliosafisha vyoo, kubeba madumu ya kumwagilia maua shule, majembe na fagio za kufagilia viwanja Tanzania hii ni wengi na imetugusa matabaka mengi tofauti na unavyoiweka hapa. Sijui kwa nini wewe unaiweka kana kwamba ni kundi fulani tu ndio lililoelemewa na mzigo huo wa majembe!

Sina uhakika na MoU unazo-refer hapa (coz sina ufahamu wa content zake) kama zinamaanisha shule ziwezeshwe kwa upande wa waalimu, maabara, maktaba etc etc...una haki kabisa ya kutaka zihamie kwenye shule za kata. Coz, what's the point ya kuwa na shule majengo tu?

Hivi zomba hizo shule zenye MoU ni zipi? Manake hainiingii akilini serikali kufanya MoU na shule mbili tatu na kuacha nyingi zikiangamia kama tulivyoona matokeo ya sasa. Kwa faida ya nani?
 
Last edited by a moderator:
kwa miezi kadhaa redio imaan wamekua wakiendesha kampeni ya kulalamikia baraza la mitihani hasa Dr ndalichako, zigo la lawama pia lilidondoshwa kwa wakristo 'eti kwamba wana mkono' katika kufeli kwa vijana wao (wa redio imaan)

matokeo ya 2012 yanaacha maswali mengi ambayo redio imaan wanatakiwa wajibu

Hebu tuzitizame shule mbili zote za kiislam

1. F
eza (shule ya kiislam) ni kati ya shule zilizofanya vizuri sana wakati

2. TEMEKE YOUTH MUSLIM SECONDARY SCHOOL imefanya vibaya kuliko kawaida, watoto wote wamepata 0.

hapa tunaona tatizo sio mfumo kristo (kama redio imaan wanavotaka kuaminisha wachache). nini kimewafanya Feza wafaulu na Temeke Youth wafeli? haiwezekani awe ndalichako na sitaki kuamini kwamba ni mfumo kristo (kama hawa wenzagu wanavyopenda kuuita)

NOTE: hii haina uhusiano na uislam wala na waislam hii inawahusu redio imaan
.

Pasco nawe usije ukaingia kwenye kundi la kufikiri kwa masaburi.Nimebahatika kuona haya matokeo tatizo ni kubwa sana na tofauti tunavyofikiri kwa juujuu tu.Critical analysis has never been done by neither of you to conclude on the stake of DR.Ndalichako. To me DR Ndalichako is very mercy.Kwa Taifa linalofikri sawasaw DR. Ndalichako ni wakupewa zawwadi ya Dhahabu maana anatuamuasha usingizini kwamba tupo dhohofu kwelikweli.Hebu Pasco fanya mapitio ya matokeo hayo performance ya masomo ya sanaa yasiyo hitaji maabara na shule nyingi zina walimu wa masomo hayo matokeo yapoje?, ni balaa tupu.Nimepitia matokeo ya sekondari ya Kanyenye japo siyo mdau wao nimeona wanafunzi wamefeli kuanzia civics hadi somo la dini wote wanafeli masomo hayo ambayo hata ufundishaji wake si tatizo.Dr. Ndalichako siyo tatizo tutafute tatizo na wala tusikimbilie dalili tutafute chanzo.ALUTA CONTINUA
 
Last edited by a moderator:
Kwa hesabu zangu, waliosafisha vyoo, kubeba madumu ya kumwagilia maua shule, majembe na fagio za kufagilia viwanja Tanzania hii ni wengi na imetugusa matabaka mengi tofauti na unavyoiweka hapa. Sijui kwa nini wewe unaiweka kana kwamba ni kundi fulani tu ndio lililoelemewa na mzigo huo wa majembe!

Sina uhakika na MoU unazo-refer hapa (coz sina ufahamu wa content zake) kama zinamaanisha shule ziwezeshwe kwa upande wa waalimu, maabara, maktaba etc etc...una haki kabisa ya kutaka zihamie kwenye shule za kata. Coz, what's the point ya kuwa na shule majengo tu?

Hivi zomba hizo shule zenye MoU ni zipi? Manake hainiingii akilini serikali kufanya MoU na shule mbili tatu na kuacha nyingi zikiangamia kama tulivyoona matokeo ya sasa. Kwa faida ya nani?

Kwanza isome MoU: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...apigania-uhuru-wa-tanganyika-na-zanzibar.html
 
Pasco mbona nafasi zaukuu wawilaya zimejaa?Vipi kunatetesi kuwa wanamtoa mtu upewe nini?
 
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

Uthibitisho ni huu

Hii nimeikuta mahali nikaona niilete na humu ili wale wote wasio niealewa angalau waanze kuelewa kuwa matokeo haya sio bure, iko namna!.

Pasco.

Tangu matokeo haya yatoke kila siku unaanzisha thread za kumlaumu Ndalichako tu, hivi unadhani yeye peke yake ndo tatizo la kufeli kwa wanafunzi nchi hii? Je unayajua vizuri majukumu yake? Una uhakika yeye ndo anayetunga mitihani?
 
Mdau hongera kwa kutoa machungu yako hapa. Laikini kama uko makini zaidi na mfumo wa elimu Dr. Ndalichako is less concerned na matokeo mabovu kwani NECTA inafanya kazi ya kutunga na kusahihisha mitihani kwa mujibu wa Muhtasari husika. Nijuacho mimi anayetakiwa kujiuzulu ni Kawambwa, Mulugo na Watendaji wake kwani hawa ndiyo wameshindwa kusimamia tendo zima la kufundisha na kujifunza.

Suala lililopo hapa ni kwamba hawa watoto wa wakulima hasa wanaosoma shule za Kayumba hawajafundishwa ipasavyo je hilo ni jukumu la Ndalichako? Ndalichako yeye kashiriki kutoonesha hali halisi ya ubovu na uozo uliopo katika elimu yetu kwa sasa.

Kawambwa, Mulugo na watendaji wao ndiyo wanatakiwa kupisha wameshindwa kazi yao ya kusimamia elimu na Ndalichako anatakiwa aendelee na kazi yake ya kutahini na kutathmini jinsi wanafunzi walivyojifunza tusimwonee bure mtu huyu. Kwani hata usahihishaji hufanyika kwa namba za mitihani na wala si majina. Huyo Mkurugenzi Green Acres ASIDHANI MATOKEO NI HISTORIA
 
Sasa jiulize, shule yenye MoU ndio ilijibu hivyo? kama yes, ni ipi?

Mnaumiza bvichwa wakati mambo yapo wazi kabisa.

Misingi ya elimu Tanzania iliwekwa kwa tabaka mbili, mpja la wale wengi wataofundishwa namna ya kulima na jembe la mkono, kufagia na kuosha vyoo, tabaka hili halina siri, tnawaona wanafunzi wakibebeshwa majembe ya mkono, mafagio ya kuoshea uwa na vyoo na makopo ya maji. Tabaka la pli ni lile linalotayarishwa kuwa watawala na hawa shuleni kwao huwakauti wakibebeshwa fagio wala jembe la mkono wala makopo ya maji ya kusafishia vyoo.

Sasa jiulize ni shule zipi hizo?
jibu la kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni zaidi ya kwenye matabaka!
 
Yaan wakulaumiwa ni Necta(msahihishaji wa mtihani)?!ikumbukwe fom4 hawa ndo waliopta bila mchujo kidato cha2,na likely baadh yao ndo wale waliofaulu bila kujua KKK!wakasoma shule ya walimu wawil tena waliopoteza morali ya kazi yao!vitabu hakuna,mazngira ya kusomea hayakidhi,pia wanafunzi walio wengi kwa ss hawaonyesh kuji2ma kutafuta maarifa.SASA NECTA INAHUSIKAJE hapo?!
 
jibu la kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni zaidi ya kwenye matabaka!

Kwanini mnatafuta majibu magumu kwenye maswali rahisi?

Nini kisichojulikana? kuwa shule za MoU ndio zenye kufanya vyema, labda iwe inafadhiliwa kutoka nje kama Feza.
 
Yaan wakulaumiwa ni Necta(msahihishaji wa mtihani)?!ikumbukwe fom4 hawa ndo waliopta bila mchujo kidato cha2,na likely baadh yao ndo wale waliofaulu bila kujua KKK!wakasoma shule ya walimu wawil tena waliopoteza morali ya kazi yao!vitabu hakuna,mazngira ya kusomea hayakidhi,pia wanafunzi walio wengi kwa ss hawaonyesh kuji2ma kutafuta maarifa.SASA NECTA INAHUSIKAJE hapo?!

Malizia:

Fedha za kusomesha ambazo zingesaidia wote zinakwenda kwenye shule za makanisa MoU.
 
Sioni hoja ya kumtaka Ndalichako kuondolewa,kwa lipi hasa,eti Necta wametunga mtihani mgumu hapo hakuna hoja mimi ni Mwalimu ni nimeona mitihani waliyofanya hawa watoto, hakuna ugumu wowote ilikuwa ya kawaida,kama kujiuzulu labda Kawambwa na katibu mkuu wizara ya elimu,ingawa nao wameukuta mfumo mbovu wa elimu uliopo Tz,kutowajibika kwa wazazi,walimu,wanafunzi na Serikali ye2.
 
Simfahamu Dk Ndalichako. Ila kwa hili anaonewa. Bw Pasco unaposema NECTA wanatunga mitihani migumu una maana gani? Mitihani inatungwa kwa kufuata syllabus. Mtihani unakuwa mgumu kama mwl hakumaliza syllabus. NECTA si jukumu lao kuangalia walimu walimaliza syllabus au la wakati wa kutunga mitihani. Usimamizi wa ufundishaji ni wa Wizara ya elimu. Jamani wengine tulisoma angalau shahada ya elimu. Kabla hujashutumu tafuta kujua kwa undani zaidi.
 
hv Ndalichako ndo aliyefuta mitihani ya fm 2 kipindi flan?kuliko wafanya hata wasiojua kusoma na kuandika wakapita free na kujikuta wanafanya pepa fm 4.ndalichako sekta yake ni ya kuandaa mitihani,kuhakikisha inafanyika na kusahishwa.ubora wa elimu unasimamiwa na wizara ya Elim kwisha.ukienda hospitali kupima afya mwisho wa cku docta akakwambia una ukimwi utamlaum dokta kwamba ndo kakupa ukimwi?THINK BIG.
 
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

Uthibitisho ni huu

Hii nimeikuta mahali nikaona niilete na humu ili wale wote wasio niealewa angalau waanze kuelewa kuwa matokeo haya sio bure, iko namna!.

Pasco.

Pasco, ni vema tukawa watafiti wa ukweli wa mambo maana watu wengine ni wazushi tu kwa ajili ya kujitafutia umaalufu. Somo ukweli huu kuhusu Green Acres (attached).
 
Simfahamu Dk Ndalichako. Ila kwa hili anaonewa. Bw Pasco unaposema NECTA wanatunga mitihani migumu una maana gani? Mitihani inatungwa kwa kufuata syllabus. Mtihani unakuwa mgumu kama mwl hakumaliza syllabus. NECTA si jukumu lao kuangalia walimu walimaliza syllabus au la wakati wa kutunga mitihani. Usimamizi wa ufundishaji ni wa Wizara ya elimu. Jamani wengine tulisoma angalau shahada ya elimu. Kabla hujashutumu tafuta kujua kwa undani zaidi.
Mkuu Abednego, nilikusoma mahali ukiwa na Shadraki na Meshaki, ninacho kilalamikia mimi sio mtihani mgumu bali mtihani ambao "sio" due to "the ill motive behind!". Kuna watu tuna macho lakini hatuoni na tuna masikio lakini hatusikii!. Ili kuona hili ninalolalamikia hapa, lazima kwanza uwe na macho ya kuliona na masikio ya kulisikia!.
Pasco.
 
mtihani hautungwi na Ndalichako. acha hizo Pasco. atawakomoaje wanafunzi kwa mtihani mgumu? mbona wengine wamefaulu tena watoto wa maskini wasiokuwa hata na umeme kwao?
 
Mkuu,
Kwa hoja hii bado unadhani anayetakiwa kuondoka ni Dr Ndalichako ama Waziri Kawambwa? Stop barking up the wrong tree, the real culprit is known.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Ndalichako...ndo wa kuondoka.kwani NECTA wamechakachua matokeo....hili ni zimwi.....baada ya kuleta mambo ya namba wameshindwa kupendela ..kisawa sawa hatima yake...kila mtu kafeli
kama suala la kuwapa ufaulu waliokua hawakufanya mitihani mama huyu ni wakati wa kuondoka....au tutakua vibondo kila siku....
 
Back
Top Bottom