Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.




Je kuna jopo linakokaa kuangalia Kama sylabus (inayoendana na huo mtihani) imekuwa appropriately covered kwa shule zote zinazotakiwa kufanya mtihani husika?
 

Kwa hesabu zangu, waliosafisha vyoo, kubeba madumu ya kumwagilia maua shule, majembe na fagio za kufagilia viwanja Tanzania hii ni wengi na imetugusa matabaka mengi tofauti na unavyoiweka hapa. Sijui kwa nini wewe unaiweka kana kwamba ni kundi fulani tu ndio lililoelemewa na mzigo huo wa majembe!

Sina uhakika na MoU unazo-refer hapa (coz sina ufahamu wa content zake) kama zinamaanisha shule ziwezeshwe kwa upande wa waalimu, maabara, maktaba etc etc...una haki kabisa ya kutaka zihamie kwenye shule za kata. Coz, what's the point ya kuwa na shule majengo tu?

Hivi zomba hizo shule zenye MoU ni zipi? Manake hainiingii akilini serikali kufanya MoU na shule mbili tatu na kuacha nyingi zikiangamia kama tulivyoona matokeo ya sasa. Kwa faida ya nani?
 
Last edited by a moderator:

Pasco nawe usije ukaingia kwenye kundi la kufikiri kwa masaburi.Nimebahatika kuona haya matokeo tatizo ni kubwa sana na tofauti tunavyofikiri kwa juujuu tu.Critical analysis has never been done by neither of you to conclude on the stake of DR.Ndalichako. To me DR Ndalichako is very mercy.Kwa Taifa linalofikri sawasaw DR. Ndalichako ni wakupewa zawwadi ya Dhahabu maana anatuamuasha usingizini kwamba tupo dhohofu kwelikweli.Hebu Pasco fanya mapitio ya matokeo hayo performance ya masomo ya sanaa yasiyo hitaji maabara na shule nyingi zina walimu wa masomo hayo matokeo yapoje?, ni balaa tupu.Nimepitia matokeo ya sekondari ya Kanyenye japo siyo mdau wao nimeona wanafunzi wamefeli kuanzia civics hadi somo la dini wote wanafeli masomo hayo ambayo hata ufundishaji wake si tatizo.Dr. Ndalichako siyo tatizo tutafute tatizo na wala tusikimbilie dalili tutafute chanzo.ALUTA CONTINUA
 
Last edited by a moderator:

Kwanza isome MoU: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...apigania-uhuru-wa-tanganyika-na-zanzibar.html
 
Pasco mbona nafasi zaukuu wawilaya zimejaa?Vipi kunatetesi kuwa wanamtoa mtu upewe nini?
 

Tangu matokeo haya yatoke kila siku unaanzisha thread za kumlaumu Ndalichako tu, hivi unadhani yeye peke yake ndo tatizo la kufeli kwa wanafunzi nchi hii? Je unayajua vizuri majukumu yake? Una uhakika yeye ndo anayetunga mitihani?
 
Mdau hongera kwa kutoa machungu yako hapa. Laikini kama uko makini zaidi na mfumo wa elimu Dr. Ndalichako is less concerned na matokeo mabovu kwani NECTA inafanya kazi ya kutunga na kusahihisha mitihani kwa mujibu wa Muhtasari husika. Nijuacho mimi anayetakiwa kujiuzulu ni Kawambwa, Mulugo na Watendaji wake kwani hawa ndiyo wameshindwa kusimamia tendo zima la kufundisha na kujifunza.

Suala lililopo hapa ni kwamba hawa watoto wa wakulima hasa wanaosoma shule za Kayumba hawajafundishwa ipasavyo je hilo ni jukumu la Ndalichako? Ndalichako yeye kashiriki kutoonesha hali halisi ya ubovu na uozo uliopo katika elimu yetu kwa sasa.

Kawambwa, Mulugo na watendaji wao ndiyo wanatakiwa kupisha wameshindwa kazi yao ya kusimamia elimu na Ndalichako anatakiwa aendelee na kazi yake ya kutahini na kutathmini jinsi wanafunzi walivyojifunza tusimwonee bure mtu huyu. Kwani hata usahihishaji hufanyika kwa namba za mitihani na wala si majina. Huyo Mkurugenzi Green Acres ASIDHANI MATOKEO NI HISTORIA
 
jibu la kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni zaidi ya kwenye matabaka!
 
Yaan wakulaumiwa ni Necta(msahihishaji wa mtihani)?!ikumbukwe fom4 hawa ndo waliopta bila mchujo kidato cha2,na likely baadh yao ndo wale waliofaulu bila kujua KKK!wakasoma shule ya walimu wawil tena waliopoteza morali ya kazi yao!vitabu hakuna,mazngira ya kusomea hayakidhi,pia wanafunzi walio wengi kwa ss hawaonyesh kuji2ma kutafuta maarifa.SASA NECTA INAHUSIKAJE hapo?!
 
jibu la kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni zaidi ya kwenye matabaka!

Kwanini mnatafuta majibu magumu kwenye maswali rahisi?

Nini kisichojulikana? kuwa shule za MoU ndio zenye kufanya vyema, labda iwe inafadhiliwa kutoka nje kama Feza.
 

Malizia:

Fedha za kusomesha ambazo zingesaidia wote zinakwenda kwenye shule za makanisa MoU.
 
Sioni hoja ya kumtaka Ndalichako kuondolewa,kwa lipi hasa,eti Necta wametunga mtihani mgumu hapo hakuna hoja mimi ni Mwalimu ni nimeona mitihani waliyofanya hawa watoto, hakuna ugumu wowote ilikuwa ya kawaida,kama kujiuzulu labda Kawambwa na katibu mkuu wizara ya elimu,ingawa nao wameukuta mfumo mbovu wa elimu uliopo Tz,kutowajibika kwa wazazi,walimu,wanafunzi na Serikali ye2.
 
Simfahamu Dk Ndalichako. Ila kwa hili anaonewa. Bw Pasco unaposema NECTA wanatunga mitihani migumu una maana gani? Mitihani inatungwa kwa kufuata syllabus. Mtihani unakuwa mgumu kama mwl hakumaliza syllabus. NECTA si jukumu lao kuangalia walimu walimaliza syllabus au la wakati wa kutunga mitihani. Usimamizi wa ufundishaji ni wa Wizara ya elimu. Jamani wengine tulisoma angalau shahada ya elimu. Kabla hujashutumu tafuta kujua kwa undani zaidi.
 
hv Ndalichako ndo aliyefuta mitihani ya fm 2 kipindi flan?kuliko wafanya hata wasiojua kusoma na kuandika wakapita free na kujikuta wanafanya pepa fm 4.ndalichako sekta yake ni ya kuandaa mitihani,kuhakikisha inafanyika na kusahishwa.ubora wa elimu unasimamiwa na wizara ya Elim kwisha.ukienda hospitali kupima afya mwisho wa cku docta akakwambia una ukimwi utamlaum dokta kwamba ndo kakupa ukimwi?THINK BIG.
 



Pasco, ni vema tukawa watafiti wa ukweli wa mambo maana watu wengine ni wazushi tu kwa ajili ya kujitafutia umaalufu. Somo ukweli huu kuhusu Green Acres (attached).
 
Mkuu Abednego, nilikusoma mahali ukiwa na Shadraki na Meshaki, ninacho kilalamikia mimi sio mtihani mgumu bali mtihani ambao "sio" due to "the ill motive behind!". Kuna watu tuna macho lakini hatuoni na tuna masikio lakini hatusikii!. Ili kuona hili ninalolalamikia hapa, lazima kwanza uwe na macho ya kuliona na masikio ya kulisikia!.
Pasco.
 
mtihani hautungwi na Ndalichako. acha hizo Pasco. atawakomoaje wanafunzi kwa mtihani mgumu? mbona wengine wamefaulu tena watoto wa maskini wasiokuwa hata na umeme kwao?
 
Mkuu,
Kwa hoja hii bado unadhani anayetakiwa kuondoka ni Dr Ndalichako ama Waziri Kawambwa? Stop barking up the wrong tree, the real culprit is known.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Ndalichako...ndo wa kuondoka.kwani NECTA wamechakachua matokeo....hili ni zimwi.....baada ya kuleta mambo ya namba wameshindwa kupendela ..kisawa sawa hatima yake...kila mtu kafeli
kama suala la kuwapa ufaulu waliokua hawakufanya mitihani mama huyu ni wakati wa kuondoka....au tutakua vibondo kila siku....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…