Dr. Kasheku Msukuma kushiriki kwenye Kongamano la Biashara na Uchumi

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Nilipokuwa naona watu wakiponda na kumsukasuka juu ya ile PhD yake kwamba alikabidhiwa na hakuisomea🎓.

Kwa sasa anajiandaa kwenda kama mnenaji kwenye kongamano la Biashara na Uchumi akiambatana na wasomi wenzake wengine mwishoni mwa mwaka huu kama mmoja wa watakaotoa elimu ya biashara na Uchumi.

IMG_20220618_184204.jpg

đź’ Hii ndiyo Dunia aseee, angalia unavyotembea isije kuwa haupo na wenzako!.
 
Dah! nahisi kizunguzungu,au wame edit hapo kwenye picha wakamuweka?
Musukuma yuko vizuri kivitendo kwenye suala la uchumi, fedha na uwekezaji kuliko hao maprofesa wabobevu wa nadharia. Ukitaka kujua hilo fuatilia shughuli anazofanya kwenye nyanja hizo.
Binafsi ninamkubali sana Msukuma kwenye ulingo wa uchumi kivitendo kuliko wanazuoni waliotufundisha nadharia vyuoni.
 
Sawa Aende Akafundishe Maana PhD Kama Madilu Ni Mzigo Eti Kodi Miaka 18

Heri kwake!!
Funzo: Dunia hii watu husema tu
 
Musukuma yuko vizuri kivitendo kwenye suala la uchumi, fedha na uwekezaji kuliko hao maprofesa wabobevu wa nadharia. Ukitaka kujua hilo fuatilia shughuli anazofanya kwenye nyanja hizo.
Binafsi ninamkubali sana Msukuma kwenye ulingo wa uchumi kivitendo kuliko wanazuoni waliotufundisha nadharia vyuoni.
Kweli kabisa mkuu,uko sahihi tunahitaji vitendo sio Porojo za Hekaya za Abunwasi.
 
Msukuma yuko smart sana hata jimboni kwake....anawazidi wasomi wengi tu hata maendeleo ya jimbo.
 
Musukuma yuko vizuri kivitendo kwenye suala la uchumi, fedha na uwekezaji kuliko hao maprofesa wabobevu wa nadharia. Ukitaka kujua hilo fuatilia shughuli anazofanya kwenye nyanja hizo.
Binafsi ninamkubali sana Msukuma kwenye ulingo wa uchumi kivitendo kuliko wanazuoni waliotufundisha nadharia vyuoni.
Ni kwanini vyuo vikuu wasitumie tu watu waliofanikiwa kibiashara kufundisha?
 
Wao wanaangalia makaratasi ila hao waliofanikiwa waitwa mara mojamoja kutoa mdahalo wa dakika kadhaa biashara imeishia hapo. Hakika kujifunza kwa mtu aliyefanikiwa ina nguvu sana kuliko hawa wazee wa kilimo cha pdf
 
Ile ripoti ya mto mara ni majibu tosha ya aina ya wasomi tulionao.
 
Wao wanaangalia makaratasi ila hao waliofanikiwa waitwa mara mojamoja kutoa mdahalo wa dakika kadhaa biashara imeishia hapo. Hakika kujifunza kwa mtu aliyefanikiwa ina nguvu sana kuliko hawa wazee wa kilimo cha pdf
Eheee. Ndiyo! Na nia yangu ilikuwa ni kukuonyesha kuwa kufanikiwa kibiashara siyo lazima kuwe ndiyo kujua biashara. Mtu kama huyo Musukuma anaweza kuwa amefanikiwa just kwa sababu yuko aggressive kwenye kuhonga!
 
Ila kwenye masuala ya kiboashara na uchumi unaweza kukuta msukuma anauelewa mkubwa kuliko hao maprofesa waliowekwa hapo
 
Eheee. Ndiyo! Na nia yangu ilikuwa ni kukuonyesha kuwa kufanikiwa kibiashara siyo lazima kuwe ndiyo kujua biashara. Mtu kama huyo Musukuma anaweza kuwa amefanikiwa just kwa sababu yuko aggressive kwenye kuhonga!
Yote yawezekana.
Biashara ni siri na siri ndiyo mafanikio yenyewe. Kwenye mafanikio huwa kuna rafu nyingi japo kwenye kamera wahusika hawagusii kabisa juu ya hujuma watumiazo/walizotumia kufika walipo.
 
Nakubali. Ila tuache kudhani kuwa ili mtu kuwa mwalimu mzuri wa kufundisha biashara basi ni lazima ufanye biashara kwa vitendo unafanikiwe.
 
Hana uelewa kwa sababu hajasoma.
Kuelewa = Hali ya mtu kuwa na ufahamu wa jambo.

Ukitaka kupata uhalisia wa biashara inavyokwenda Tanzania ni mara mia umsikilize Kasheku aliyefanikiwa katika biashara na anayendelea kufanya biashara kuliko hawa academicians wetu ambao wengi wao wameonekana kuwa ni "opportunists"...

Mfano tu kwenye hiyo panel ni Prof. Mgaya alituambia chanjo ya COVID haina ubora tusiikimbilie kwa sababu ya msimamo wa aliyemteua, halafu alipoondoka akasema ni salama kwa asilimia 99.9%
 
Back
Top Bottom