Sasa ukikutana na Mbunge wa Kahama mjini na mfanyabiashara Jummane Kishimba si utakufa kabisa. Maana yule jamaa ni zaidi ya Professor.
Kwa mfano fuatilia miradi yake tu pale Dodoma utajua huyu ana akili kubwa mno. Pia ana bustani yake pale Dodoma ya mboga, nyanya n.k alichofanya kasomba udongo unaofaa kustawisha mazao hayo kisha akalima. Maprofesa wenu wa nadharia wanaishia kupima udongo tu na kukuambia haufai kwa nyanya. Sasa kama haufai tufanyeje au nini suluhisho maana ni lazima tulime hapo. Yeye kafuata udongo unaofaa kaweka juu ya usiofaa na uzalishaji ukaendelea.
Sasa hawa watu wapo mbele ya watu wa nadharia na huenda kujifunza kwao kuthibitisha nadharia zao.