Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Mheshimiwa Dr. Kikwete,
Mheshimiwa rais, Katiba ni maridhiano- tumefundishwa mashuleni theories za social contract- Social Contract Theories as expounded by Hobbes, Locke and Rousseau and many others. Rejea maandiko hayo!
Naomba niseme tu kuwa katiba hii itaacha mpasuko mkubwa katika jamii ya watanzania. Umoja , ushirikiano vimetikiswa-mpasuko kama alivyotuasa baba wa taifa. Historia itakuwa juu yako. Litafakari upya. Hatuna haja ya haraka kiasi hicho!
Kuna mtu alisema kuwa labda hajasoma social contract niliyoisema kwenye post yangu
kwann unasema hivo? Kwani hakuna watanzania tunao ihitaji katiba pendekezwa?
nyie inawauma sana kuona katiba hii inayopendekezwa kwamba inaelekea kushinda, jamani tanzania ni yetu sote kuweni wazalendo acheni maneno maneno tena kumtajataja rais kikwete. Kuweni wazelndo kwa nchi yenu.
suala hapa siyo katiba kupita, ni zaidi ya hapo. Ni suala la kuimarisha umoja na mshikamano wa taifa. Utapata faida gani katiba ikipita huku ikiacha mgawanyiko katika taifa??? Grow up kid! Uzalendo siyo kulazimisha katiba inayowagawa watanzania bali ni kuchukuwa hatua zozote zinazofaa ili kulinda umoja wa taifa.
Rais ni wetu sote hivyo kumtaja sio kosa wala dhambi, muhimu ni kutokumvunjia heshima. Kwenye mambo muhimu usiendekeze ushabiki.
nyie inawauma sana kuona katiba hii inayopendekezwa kwamba inaelekea kushinda, jamani tanzania ni yetu sote kuweni wazalendo acheni maneno maneno tena kumtajataja rais kikwete. Kuweni wazelndo kwa nchi yenu.