Dr. Kimei awania tena tuzo ya African Banker of the Year Award

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
4,315
Reaction score
309
Mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dr. Charles Kimei , ameorodheshwa tena kwenye tuzo ya African Banker of the year award kwa mwaka 2014.

Tuzo hii hutolewa na Benki ya Africa (ADB) kwa viongozi wa mabenki Afrika ambao wameonyesha weledi wa uongozi na utendaji mzuri wa taasisi zao na sekta nzima ya fedha.

Dr. Kimei anakuwa Mtanzania wa kwanza kuwania tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo (2013 & 2014). Mshindi wa tuzo hii atatangazwa mjini kingali -Rwanda mnamo tarehe 21 Mei 2014.

My take : Tunakutakia mafanikio mema Dr. Kimei kwenye tuzo hizo, na hii yaonyesha watanzania tuna viongozi ambao wanaweza na uwezo mkubwa wa kuongoza.

Source
: The Guradian news paper 29.04.2014 (Business and Foreign).
 
Mkuu alipowania 2013 alishika namba ngapi?

Anyway hongera zake ingawa walalahoi tuna uchungu sehemu kubwa ya fedha za EPA ziliibiwa kupitia hii benki chini ya uongozi wake. Pia maafisa mikopo wake wana njaa Sana, bila rushwa hawakupi mkopo, na wale ma bank teller wake wanapiga Sana multitasking, yaani uko counter anashugulika na cheki na slip za waliotoa cha juu wasikae kwenye foleni huku wewe unaangalia live. Dr Kimei akirekebisha haya anaweza kushinda hiyo tuzo.
 
Acha upumbavu wa kuulizia kabila la mtu! Ufanisi wa mtu na kabila lake vinahusianaje? Au wadhani aliyepost ni mchaga na kama ndiyo shida ipo wapi? Mmekaririshwa kusema uchaga itafika mahali maumbile yako utasema yamekaa kichaga! ----- ww!
 
Mkuu nashkuru wa kunisaidia kujibu. Kwa kweli JF ya sasa tuna aibisha sana, badala ya kujadili hoja tunajadili kabila la mtu. Hivi kweli ndio Great Thinkers tunatakiwa kuwa ? nadhani yabidi JF tujirekebishe.
 
Mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dr. Charles Kimei , ameorodheshwa tena kwenye tuzo ya African Banker of the year award kwa mwaka 2014.

Tuzo hii hutolewa na Benki ya Africa (ADB) kwa viongozi wa mabenki Afrika ambao wameonyesha weledi wa uongozi na utendaji mzuri wa taasisi zao na sekta nzima ya fedha.

Dr. Kimei anakuwa Mtanzania wa kwanza kuwania tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo (2013 & 2014). Mshindi wa tuzo hii atatangazwa mjini kingali -Rwanda mnamo tarehe 21 Mei 2014.

My take : Tunakutakia mafanikio mema Dr. Kimei kwenye tuzo hizo, na hii yaonyesha watanzania tuna viongozi ambao wanaweza na uwezo mkubwa wa kuongoza.

Source
: The Guradian news paper 29.04.2014 (Business and Foreign).

Asante kwa Taarifa Mkuu, Binafsi mie nakubaliana na utendaji wake..
Tuzo hizo zinapigiwa kura au?
Naomba utusaidie tujue ni jinsi gani tunaweza kuchangia hiyo tuzo kuja nyumbani.
Watanzania kwanza.
 
Nashukuru sana mkuu kwa kutaka ufafanuzi zaidi. Hizi tuzo hutolewa na Benki ya Afrika, ambapo huundwa jopo la wataalamu na kupitia utendaji wa viongozi wa mabenki mbali mbali barani Afrika. Jopo hili hufanya uchambuzi na kuchuja na kisha kuchagua wanao stahiki. Katika kinyang'anyiro hiki Dr. Kimei anashindana na wengine wapatao takriban 9, amabo hupigiwa na kura na CEOs wa mabenki ya Africa.
 
CRDB inabidi isome alama za nyakati, benki inaanza kuelemewa na wateja, mwisho wa siku itakuwa yale ya NMB.

Angalia branches nyingi zinakuwa na foleni kubwa zisizo na msingi.

Tawi lina madirisha 5 lakin yanayofanya kazi ni 2

Wasipoangalia itakula kwao.
 
mimi sitaki kuwasikia hao crdb ukitaka kudeposite pesa utawekwa kwa foleni mpaka ukome.
 
CRDB kutwa inaibia wateja. Hakuna faida yeyote mtu anapata kwa kuweka fedha humo. ATM zake full majanga. Wafanyakazi jeuri halafu what.... Banker of the year? My foot
 
Kimei ilikua zamani,si sikuhizi.tuzo ataisikilizia kwenye majira.
 
Nashukuru sana mkuu kwa kutaka ufafanuzi zaidi. Hizi tuzo hutolewa na Benki ya Afrika, ambapo huundwa jopo la wataalamu na kupitia utendaji wa viongozi wa mabenki mbali mbali barani Afrika. Jopo hili hufanya uchambuzi na kuchuja na kisha kuchagua wanao stahiki. Katika kinyang'anyiro hiki Dr. Kimei anashindana na wengine wapatao takriban 9, amabo hupigiwa na kura na CEOs wa mabenki ya Africa.
Poa Mkuu, asante kwa taarifa..
Natumaini atashinda maana anastahili.
 
Huyu si Nchagga huyu?

Ukweli inakera sana ndugu yangu, cjui ni akili za namna gani!? Mtu anaacha issue iliopo mezani anajadili kisicho kabisa!! Watu wanaiga wanasiasa kila wimbo wanaouimba kwa maslahi yao nao wanaiga ama kutumiwa bila kutafakari athari zake!

Mkuu nashkuru wa kunisaidia kujibu. Kwa kweli JF ya sasa tuna aibisha sana, badala ya kujadili hoja tunajadili kabila la mtu. Hivi kweli ndio Great Thinkers tunatakiwa kuwa ? nadhani yabidi JF tujirekebishe.
 
unajua dunia hii kuna watu wapumbavu sana. ukiwatukana watadhani umewaonea. huyo anaeuliza eti Dr. kimei ni mchaga , mwambie amuulize mama yake!.
yule mzee anastahil tuzo. changamoto zingine sio za kwake ni za bank in general
 
Back
Top Bottom