Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa habari, hii lakini ndugu KKN punguza ukali wa maneno. Hii ni tabu kidogo kuyatamka makavu makavu hivi. Ehe!
Hata katika kugombea ubunge wa Vunjo kwa tiketi ya CCM, mimi nasimama na Dr. Kimei'Myonge myongeni haki yake mpeni' pamoja na tuhuma zote hizi mimi ni mmoja ya wanaokiri, Dr. Kimei na CRDB yake, amesaidia sana watu na taasisi mbalimbali. Mema yake ni makubwa kuliko hayo maovu hata ukiyachanganya yote.
Kuhusu tuhuma za ngono, Mtoa tuhuma pamoja na yote, ana chuki binafsi. Hii haitashusha hadhi na heshima ya Dr. Kimei mbele ya jamii. Kwetu sie Wasukuma hiyo mbona sifa!.
Hili la mapenzi ofisini sio kweli ila kwa sisi ngozi nyeusi jamani hizo ndio zetu naomba tusilizungumzie sana vinginevyo kama wewe mkeo ndio wakwanza wako naye wewe ndie wakwanza wake, vinginevyo kama wewe si wakwanza basi si lazima uwe wa mwisho, kuna waliokutangulia na watakao kufuatia. Tukianza kuchambua vigogo vipanga, mbona list itakuwa ndefu mpaka jamaa wa Magogoni ataingizwa. Alishindwa Clintoni akiwa rais, tena ikulu ya Marekani, itakuwa Kimei! .
Sisi tunaoripoti Bunge Dodoma mbona tunashudia mengi, lakini hatusemi kwa sababu hayo ni utawala binafsi, hii ya ngono hapa JF. Si mahali pake tusiijadili tusijeshusha hadhi yetu.