Rasimu imechemka umri wa urais
na Edson Kamukara
MHADHIRI wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), Dk. Kitila Mkumbo, amesema kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imechemka kwa kutoafiki maoni ya kutaka umri wa mgombea urais kupunguzwa.
Dk. Mkumbo ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Elimu cha chuo hicho, alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akitoa mada katika kongamano la hali ya elimu na mustakabali wa taifa, lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha).
Alisema kuwa matokeo ya sensa na utafiti yameonesha kuwa asilimia 45 ya Watanzania ni watoto chini ya miaka 15 na asilimia 16 ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.
Kwa hiyo utaona kuwa asilimia 61 ya Watanzania ni watoto wa umri chini ya miaka 25. Hii ni nchi ya watoto. Kwa kweli kama kuna kitu rasimu hii ya katiba imechemka ni kutokubali wazo la kupunguza umri wa mgombea urais.
Hakuna sababu ya msingi kwa nchi kutotawaliwa na mtu wa miaka 30. Huyu kama amepata elimu bora yenye kumwezesha kuchanganua mambo anafaa kabisa kuwa rais, alisema.
Hata hivyo, wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Katiba, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alisema katika kipengele hicho waliamua kuwa umri wa mgombea urais uendelee kubakia ule ule wa kuanzia miaka 40.
Kuhusu mfumo wa elimu nchini, Dk. Mkumbo ambaye pia ni mshauri wa masuala ya kiufundi wa CHADEMA, alisema kuwa nchi zote zinazopanga mipango mizuri, fedha zake nyingi huelekezwa kwenye elimu ili kuwekeza kwa vijana.
Leo nchi haina wataalam, ina vijana wenye elimu isiyowawezesha hata kuajiriwa au kujiajiri, lakini watawala wanazungumza kuchimba gesi. Hiyo gesi bila elimu itawalipukia. Tatizo letu tumechagua wenye akili ndogo kuwatawala wenye akili kubwa, alisema.
Mkumbo alifafanua kuwa jamii iliyoelimika vizuri inapenda na kuheshimu kazi na haiamini kwenye ujanja ujanja, inapenda maadili na kuchukia rushwa, inapenda demokrasia.
Elimu yetu imekaa kimitihani, wanafunzi wanasomea kufaulu mitihani wala si kuelewa. CHADEMA tunataka kutengeneza mfumo wa watu kujifunza, ambao utaunganisha elimu ya msingi na ufundi ili kuzalisha watu wanaofikiri na kujiajiri badala ya kuangalia vyeti na vyeo, alisema.
Msomi huyo alifafanua kuwa taifa hili limekaa zaidi kwenye kuombaomba badala ya kujitegemea kama muasisi wake Mwalimu Nyerere alivyoweka misingi hiyo.
CHADEMA inataka kutengeneza taifa la kujitegemea ndiyo maana tumeweka nguvu zote kwenye elimu. Tunapaswa kusema hapana kuwa ombaomba. Kulijenga taifa si kuimba tu Peoples Power, hiyo ni hamasa, lazima tufikirie mbali na kufanya kazi kwa bidii, alisema.
Alisema ili kuitathimini elimu yetu tunapaswa kupima ni watu wangapi wanapata elimu, ni elimu ya namna gani inatolewa kama wanaweza kufikiri, kuajirika na kuajiri wengine na anayehitimu anaaminika kwa kiwango gani katika jamii.
Katika kupata suluhu ya hili, CHADEMA tunaona cha kufanya ni kuandaa sera mpya ya mfumo wa elimu yetu ambayo tutaitoa kwa wananchi kabla ya uchaguzi ili waisome na kutafakari nini tunataka kufanya, alisema.
Mkumbo aliongeza kuwa kumekuwa na mfumo mbovu wa kubadilisha hovyo mitaala na kuwepo kwa mifumo mingi ya elimu ndani ya nchi moja ambayo imeharibu mfumo wa shule za umma na kukumbatia za binafsi.
Alisema CHADEMA haitafuta mfumo wa shule binafsi bali itaugawa katika makundi mawili ambapo moja litakuwa la huduma ambalo litasimamiwa na serikali ili kudhibiti kupandisha ada kiholela.
Kundi la pili utakuwa mfumo wa biashara ambao utawaacha wapandishe ada watakavyo, lakini tutawatoza kodi kubwa, alisema.
Aliongeza kuwa CHADEMA itatengeneza mfumo utakaowavutia watu wenye vipaji kujiunga na ualimu tofauti na sasa katika utawala wa CCM ambapo sifa moja ya kujiunga na ualimu ni lazima uwe umefeli.
Alisema kuwa hao wenye vipaji na wito watakapojiunga na ualimu watalipwa mishahara na maslahi yanayolingana na taaluma nyingine, kwamba CHADEMA inataka mishahara ya watumishi wa umma ifanane.
Posho ya kufundishia lazima irudishwe kama ilivyokuwa zamani ili kumfanya mwalimu atulie aache kuhangaika kutafuta njia zingine za kuuza maandazi kujikimu kipato, alisema.
Mwisho