MAPUMA MIYOGA
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,792
- 2,365
wewe utakuwa unaugua ule ugonjwa wetu wa siku zote wa kulinganisha visivyolingana, hata ktk hizo nchi ulizozitaja kila Nchi imeweka Umri ambao inafikiri unafaa kutokana na utamaduni wake, sasa kwa nini sisi iwe tofauti?
Mila na desturi zetu hazikubaliani na hilo swala, kwetuu sisi mtu wa miaka 30 bado sana kwanza hata hajakomaa, wengi wetu bado tunakimbizana na videmu, ktk jamii nyingine kijana wa miaka 25 tayari anajua majukumu yake ktk jamii inayomzunguka kwa sababu jamii yake imeshamuandaa, wenzetu Ulaya, kijana wa miaka 18 anahama nyumbani anajitegemea analipa bili zake mwenyewe n.k na anajua nafasi yake, sisi kwetu miaka 25 bado ni mtoto tu na sia ajabu ktk maisha yake hajawahi hata kujilipia kitu chochote, hivyo hajakomaa!
Hata hizo ulizozitja usikute hizo sheria ni mpya, baada ya kuona labda sasa wameshafikia mahali ambapo vijana wao wameshakomaa kuweza kuwa viongozi, sisi kwetu bado, hivyo usilinganishe visivyolingana, kijana wa Miaka 30 Tz sio kijana wa miaka 30 Ulaya!
Na ushahidi upo, nenda Dodoma ukaone Wabunge wamjaa Disko wanacheza mduara na kushika shika malaya Disko, Wabunge wa Ulaya hawafanyi hivyo!
Jamani katika mjadala huu wa umri, Tusisahau kuwa hadi huyu kijana achaguliwe katika umri wa say miaka 30, ina maana amepita katika mikono salama na jopo la watu wamemkubali ndio maana anapitishwa kugombea. Tusichukulie kama vile miaka 30 basi ni given kuwa rais. Kuna sifa zingine za kumwezesha kuwania urais hata kabla ya hio ya umri.
Kwangu mimi miaka 30 ni sawa tu. huyu mtu atafikaje hadi kufikia kuwania urais bila kuwa amepata exposure na kukomaa kiumri na kisiasa bila ya kuonekana na watu. Watu watamuona na kuridhika KUWA katika umri wake huo, tayari anafaa. Mbona DHAIFU aliambiwa na mding kuwa bado hajakuwa, na miaka kumi baadae si mmeona mambo yake au mtasema alikuwa bado tena.
Miaka 30 ni sawa.
