Dr. Kitila na Mwanakijiji wawavaa wapinzani na wahafidhina...

Dr. Kitila na Mwanakijiji wawavaa wapinzani na wahafidhina...

jobe ayoub

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
203
Reaction score
100
[h=5]Kitila Mkumbo
[/h]Bado tuna safari ndefu sana ya kuwaelewa CCM. Yaani kuna mtu alitarajia kwamba Sitta angetenda tofauti na wanavyotenda CCM? Yaani kuna watu walijifanya kusahau kwamba Sitta ni member wa cabinet au ndio kusema hawajui jinsi cabinet inavyofanya kazi? Yaani Waziri mwandamizi katika serikali ya CCM ambao imeshaweka msimamo wazi kuhusu katiba hii mlitegemea atende haki? Yaani hamkujui kwamba Sitta angelitumia bunge hili kujisimika na kujijengea uhalali ndani ya CCM? Hamkujua kabisa hili?
Tulipowaambia ni makosa wapinzani kumpa imani kubwa kiasi hicho Sitta mkasema wewe sio mzalendao. Sasa habari ya kutaka kususia bunge inatoka wapi? Kaeni humo humo 'mpaka kieleweke' pengine mkitoka mtakuwa mmeshawajua CCM!


[h=5]Mimi Mwanakijiji
[/h]Ninachowaza: Sijui nimefyatuka tu au nini; nimeamka na kutaka kuona kuwa CCM kwenye Bunge lao la Katiba wanasimamia kanuni zao na maslahi yao... nataka nione wakitumia wingi wao kupitisha Katiba wanayoitaka kwanza kwa sababu wao ni wengi zaidi kwenye Bunge hilo na vile vile wao ndio watawala wa nchi hii wakiwa na wingi mkubwa tu. Wapitishe kanuni na hatimaye rasimu waitakayo wao ili iwe Katiba itakayopendekezwa; watumie wingi wao kuzima hoja za wapinzani.

Ninachotaka kuona ni wapinzani watafanya nini... maana kama walikubali mchakato huku wakijua kabisa kuwa ni mchakato uliotengenezwa na CCM ili kuinufaisha CCM iweje sasa waanze kung'aka; iweje waitake CCM isitumie nafasi hii ya pekee ya kujikita zaidi madarakani? Hivi kweli kuna mtu anafikiria kuna mpinzani atasusa na kujitoa kwenye bunge la Katiba? labda dakika za mwisho.. lakini siyo SASA...
 
Nimeshtuka kuona mwanakijiji anayeishi mjini kuendelea kuitwa mwana kijiji umenikumbusha alivyompokea slaa pale u.s leo anaponda utumishi wake
 
Huwa wanasubiri wale weeee ndo wasusie wakati wameshiba...... GARI YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI........ POSHO LUKUKI ZA KIBUNGE..... e.t.c.
 
Yuda ananyosha kidole anasema hawajui cicm Je yeye anajua u Yuda wake
 
Nyie hadi sasa hamumjui Mwanakijiji? hamkumbuki 2010 kuhusu CCJ aliyokuwa akiipigia debe na kuiponda Chadema?

Mara hii mmeshasahau kweli? Kwamba lengo ni kuvunja nguvu ya CDM? Huyu bado ni shushushu tu wa TISS. Ingawa mara nyingine hujifanya ni mtetezi wa upinzani na hoja zao, lakini wapinzani wakionekana tu kutaka kufunga goli, basi Mwanakijiji bila aibu huwa tayari kuhamisha nguzo ya goli!

Hii ndiyo kazi ya Mwanakijiji siku zote! Ni mnafiki wa kutupa! Pu!
 
ni kweli kuwa kitila amaijua ccm vizuri kwani ndio mabwana zake waliomfanya asaliti mabadiliko! ni ajabu sana mtumwa kutomjua bwana wake vizuri!
 
ccm kweli kiboko,kama walimwingiza mkenge yeye na msaliti mwenzie zzk na sasa wamebakiza makelele tu mitandaoni wakidhani siasa za TZ zinaendeshewa mitandaoni na kwenye magazeti uchwara!!!!! watz wenye uwezo wa kuingia mitandaoni wote wanajielewa na kujitambua hivyo hawawezi kuyumbishwa na kelele zao za kinafiki!
 
Nyie hadi sasa hamumjui Mwanakijiji? hamkumbuki 2010 kuhusu CCJ aliyokuwa akiipigia debe na kuiponda Chadema?

Mara hii mmeshasahau kweli? Kwamba lengo ni kuvunja nguvu ya CDM? Huyu bado ni shushushu tu wa TISS. Ingawa mara nyingine hujifanya ni mtetezi wa upinzani na hoja zao, lakini wapinzani wakionekana tu kutaka kufunga goli, basi Mwanakijiji bila aibu huwa tayari kuhamisha nguzo ya goli!

Hii ndiyo kazi ya Mwanakijiji siku zote! Ni mnafiki wa kutupa! Pu!

Duh! Umenikumbusha ule mjadala humu JF kuhusu CCJ. Alianza kuishabikia CCJ baada ya nyota ya Slaa kuanza kung'aa. Nakumbuka MKKJ baada ya kubanwa sana kuhusu CCJ yake alitoweka kwa siku 3.

Ni mnafiki tu -- yeye na CCM damdam. Kama usemavyo hujifanya kutetea hoja za wapinzani kiujanjaujanja tu. Hana lolote!!
 
Mwanakijiji n mtu mwenye kuangalia upepo unavuma wapi,.ila mawazo yake n mazuri mara nyngi..
 
Uungwana ni pamoja na kukubali makosa, na sasa kwa vile wameshayavulia nguo, hakuna budi kuyaoga.

Hivi kweli kwa umoja wao huo wa Ukawa, wote kabisa watakubali kuacha posho bila kufarakana? Yetu macho na masikio tumeelekeza Dodoma.
 
naona siku hizi mkuu Mzee Mwanakijiji kaisusa jf kimtindo baada ya kupata members wengi kupitia fb account yake .ukitaka kupata nondo zake barabara muibukie fb.huwa nanaoma sana kule.
 
Last edited by a moderator:
Kama kuna mtu anawaza kuwa katiba ni ya ccm,cdm au cuf bado anafikiri kwa moyo wake na si kwa akili yake"katiba bora ni ile itakayotekelezeka kwa chama chochote kitakacho twaa dola kwa maslahi ya wtz wote,maana ndio nyenzo pekee itakayopima uzalendo wa watawala wetu"
 
Naomba mnijuze rangi ya mwanakijiji ili niwezekuchangia nami. Maana kama yule mnyama wa rangi rangi hivi
 
mwana kijiji kaanza zile makala zake za kuaminisha watu kuwa CDM inakosea kwa kiasi ambacho wananchi hawaonai ila mwanakijiji,zitto, kitila na wengine....wanaofanya kazi ya CCM ku impose fikra za kubuni kwa wananchi ili situmike kuihukumu CDM. Hivi mwana KJJ hakuona chama kingine ch aku invest?Au kukilaumu? Au anataka sema mawazo yake ndio yameifiksiha CDM hapo?
 
Nimeshtuka kuona mwanakijiji anayeishi mjini kuendelea kuitwa mwana kijiji umenikumbusha alivyompokea slaa pale u.s leo anaponda utumishi wake

To be honest, sijaona wapi MMM amemponda dr. Usually anachokisema ni facts ambazo zilihitaji umakini wa hali ya juu for great thinkers. Unadhani ni reflection gani itatoka kwenye jamii pale CCM ikifanikisha mipango yake kwenye huu mchakato wa Katiba?
 
I for one sijawashambulia wahafidhina kwani mimi najitambua kama mhafidhina...

Mzee Mwanajiji hata mimi nimeona hivyo kwamba haujamshambulia mtu! Hata humu If iliposikika kwamba Sitta anagombea wengi tulipiga vigelegele kama kwamba huyo mburura ni malaika!
 
Back
Top Bottom