Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,772
- 22,598
Dr Kumbuka mwanaume anayechamba kama mwanamke, mwanaume huyu ni
Presenter wa Times Fm, anamaneno kuliko wanawake wa uswahilini, usoni kajipiga kitaulo (Mkorogo).
Michambo yake inafundisha zaidi wanawake na wanaume tabia zao na jamii kwa ujumla. Zaidi pia michambo hiyo hufurahisha sana.
Hufurahisha zaidi pale anapokuwa akiongea maana huweka kionjo cha 'mama' kwakweli ukimsikiliza lazima ufurahi.
Na hii ni baadhi ya michambo yake kwa wanawake wanaoachana na waume zao na kusema wanaume vibamia hasa baada ya kuachana.
Anasema mwanamke anapokua na mwanaume humfurahisha na kumfikisha mwanamke tena mpaka anataja vituo vyote Chalinze, Ruvu mpaka Moro mjini ila akiachwa anaanza kusema 'kibamia'.
Anasema wanaume wanavumilia mengi hawasemi, ila wanawake wa siku hizi wana historia wana hila na tabia mbovu kama 'vijoka kobra' anasema wanaume hukutana na wanawake wengine mabwawa kama Mtera.
Anasema wanawake wengi wakilala wanalala kama wanasoma gazeti, wengine kila siku vifo vya mende.