Pumzika Mzee Gama. Ulifanya kazi kubwa!
LAKINI....wakati Gama akiwa Mkuu wa JKT na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, alishindwa kudhibiti ukabila:
Ktk Jeshi la kujenga Taifa aliajiri vijana wengi kutoka Mkoa wa Ruvuma wengi waliomaliza Darasa la Nane na kuwafanya ma-Afande. Kazi yao kubwa ikawa ni "kujenga" tabia ya ngono na wasichana wadogo waliomaliza Darasa la Nane waliojiunga na na JKT.
"Gama, huko kwako Jeshini, mabinti zetu hatuwaleti kuolewa na hao Maafande wako!"
Gama alishindwa kudhibiti tabia hiyo.
"Basi tutakubadilisha kazi."
Akapewa Ukurugenzi wa Usalama wa Taifa. Na badala ya kuajiri watu wenye elimu na uzalendo wa hali ya juu, Gama kawaleta ma-Afande wake, wengii wenye elimu duni! Utendaji kazi na hadhi ya idara hiyo ikadorora!
Hii haikumpendeza Rais Nyerere...ikabidi kufanya marekebisho makubwa na kumteua Hasnu Kitine aliyeajiri wasomi wenzake wengi.
Mtandao wa Gama ulisambatatishwa; ukaondoka na magari mengi ya Volkswagen ndogo - mengi yalikuwa, pengine, hayakuandikishwa!