Dr Levy: Ali Kiba ni dozi ya kutwa mara tatu

Ningekuona genius kama ungemuelezea Ali Kiba bila kumtaja Diamond
itu vingine vinakuja automatically.

Huwezi kumkwepa Diamond halipo Ali.
Huwezi kumkwepa Ronaldo alipo Messi.
Huwezi kuikwepa Yanga ilipo Simba.

hii ni kwa mashabiki wa Ali wanaotaka awe kama Diamond.

We ni muelewa...naamini umenielewa.
 
Yale yale ya Ray na Kanumba, yule kajiita "the great" huyu akaja na "the greatest" , yule alivyoanza kutoboa kimataifa huyu nae akaamka usingizini nae akaanza mbio za kimataifa, yule amefariki huyu nae akakosa motivation sasa hivi yupo yupo hana cha kimataifa wala kitaifa. Halafu mkumbuke huyu alianza game kabla ya marehemu what a coincidence[emoji23]
[emoji134] [emoji125] [emoji23] [emoji23]
 
Ali alikuwepo miaka 6 kabla ya ujio wa Diamond....sasa sijui nani anaetumia boost ya mwenzie
Iyo miaka 6 kabla ya diamond aliufikisha wapi mziki wetu,?
Wakati hata kutoa video kulikuwa kunamshinda
 
Ali hashindani na mtu.

Mashabiki wake ndio wanamshindanisha na Diamond.
Kitu ambacho kipo ni ushindani kati ya Diamond na timu yake wakishindana na Mashabiki wa Ali.

Yeye Ali hana hata habari...anafanya muziki wake kama burudani na sio kama biashara.
na sijasema anashindana na mtu ebu soma vzur bandiko langu au uelewa mdogo
 
Iyo miaka 6 kabla ya diamond aliufikisha wapi mziki wetu,?
Wakati hata kutoa video kulikuwa kunamshinda
Ndio hapo mnapojichanganya kutaka Ali awe kama Diamond.

Huyo Ndio Ali na muziki kwake ni burudani kama anavyoburudika kucheza soka kule Jangwani.

Angeweza kufika mpaka ligi kuu kama angetaka ila achezi football kibiashara.
 
Ukimfunika kukata mauno atakushinda kutunga. Ukimfunika umaarufu atakutesa kwa sauti. Ukimsumbua kuhonga media yeye atakuumiza kwa kutojisumbua na hizo media.
Ni kama kumpenda mwanamke ambaye hajui kama unampenda.Na mbaya zaidi hata hisia juu yako hana.
Utaumia sana.

Ndo Ali.Hata mashabiki wake wanampenda kuliko yeye anavyowapenda.Anachofanya ni kuwapa kile alichopewa na Mungu.
Sauti.
Watu wanadata naye.

Wakati watu wengi sana wakimsifia kwa sauti ambayo anayo yeye tu ktk dunia hii.
Kuna kitu wanakisahau.Ana tofauti sana katika tungo zake.

Sikiliza Mapenzi yana Run Dunia.

Anamuimbia mapenzi mwanaume mwenzake. Ngumu sana mwenye akili ya kisoda kuelewa ule wimbo.

Mchizi anamuimbia mchizi wake ngoma la mapenzi afu lina bamba mbaya.Hata R Kelly na wenzake akili hii waliikosa.

Dem kaenda kwa Ali kumshitakia ujinga wa bwanaake.Of coz watoto wa kike wanapenda faraja.
Ali akampa faraja.

Mchizi kugundua kaamua kumtosa mtoto.Mtoto kaamua kutangulia mbele ya haki.Alimpenda mchizi wake ila Ali alimpa faraja tu baada ya ushauri.Hata mimi ningemfariji kwa namna hiyo mtoto mzuri.
Kasikilize hilo ngoma ukiwa na akili timamu usichanganye na mawazo ya hali ya Wema Sepetu kwa sasa.Hutaelewa alichoandika Ali.

Kiba siyo wa nchi hii.

Kinachofanywa na computer yeye anakitoa kwenye koromeo lake.
Kuna sauti kutoka kooni kwake ni ya pekee kuliko upekee wenyewe.Hawezi kusema ila Diamond na wenzake hicho kitu kinawaumiza sana.

Ali hajui kujitangaza.Ndo maana hata gari anayotumia haijulikani.
Ali hajui kiki.Ndo maana huwezi kumsikia akiongelea issue zake na madem zake.Hajui kujiongeza ndo maana husikii ana nyumba au shilingi ngapi kwenye account zake za bank.

Na ni ngumu kumkuta news room za udaku. Vyote hivyo hana lakini bado anawaumiza kichwa kundi kubwa la watu.

Katikati ya magwiji wa hizi kazi.

Fella,Tale na wenzao.Sallam muweke kando hajui fitna za game hili.
Pamoja na lundo la hao watu Alibbado anasimama nao katika mstari mmoja.
Ogopa sana.
Heshimu.

Hana anachowaweza zaidi ya lile koo lake na akili ya kuandika kinachotakiwa kuandikwa.
Hapa siyo suala la team flan.Ukweli uko wazi kuwa kuna upinzani wa wazi na wa siri kati ya Kiba peke yake na Diamond na watu wake. Huwezi kusikia management ya Ali ikimuongelea Diamond.Ila ni rahisi zaidi kusikia management ya Diamond ikiongea jambo la Kiba.
Ndo ukweli.

Watu wanaomzunguka Diamond huwezi kushindana nao hata kwa nusu saa.Game la muziki liko vyumbani mwao.Linawatii kuliko askari wa Dar mbele ya Makonda.Lakini Ali kaendelea kuwepo kwenye kilele bila kutumia nguvu.Alichonacho Ali kwenye koo angekuwa nacho Diamond dunia ingesimama.

Ni kama Ronaldo angekuwa na kile alichonacho Messi katika miguu yake.

Mashabiki wanatumia nguvu nyingi sana kupambana na Diamond mitandaoni,wakati Kiba anawauliza wadogo zake vilipo viatu vyake vya michezo akacheze football bondeni pale Jangwani.

Diamond anajituma sana na muziki wake.Ali anatufanya tuamini kuwa muziki ni burudani na ufanywe kiburudani.
Wakati soko la muziki likilazimishwa liwe na muziki unaochezeka.Ali alikuja na ngoma kama Mac Muga ambao hauchezeki na siyo wa mapenzi na alikuja na ngoma ya Mwana ambayo sio wa mapenzi wala sio club bagger.ukakamata vibaya sana.
Kasikilize Karim.

Utagundua kuwa Kiba ni zaidi ya biti na promo.

Imeandikwa na mkongwe Dr.Levy Baba ubaya
Baba levi kitambo sana nipm ndg kuna jambo nikushirikishe
 
ALIKIBA nikama CRISTIANO RONALDO kila siku anapambanishwa na watu mbali mbali but still yuko juu
 
Kweli we ni mzaramo nilikua nasikia tu
 
itu vingine vinakuja automatically.

Huwezi kumkwepa Diamond halipo Ali.
Huwezi kumkwepa Ronaldo alipo Messi.
Huwezi kuikwepa Yanga ilipo Simba.

hii ni kwa mashabiki wa Ali wanaotaka awe kama Diamond.

We ni muelewa...naamini umenielewa.
Wazaramo siwawezi....
 
uu vitu vingine vinakuja automatically huwezi kuvipinga....

Huwezi kumzungumzia Messi bila kumtaja Ronaldo.
Huwezi kuizungumzia Simba bila kuiweka Yanga.

Kikubwa Diamond alichomzidi Ali ni kutafuta Kiki peke yake kwa sababu Ali anafanya Muziki na Diamond anafanya biashara kwenye Muziki.

Diamond alichomzidi Kiba ni ubunifu na akili ya biashara, full stop. Diamond has made himself a multi milion brand. He has worked so hard to spread his music to the rest of Africa. He has opened a record label, he has signed 4 artists. His brand has seen him become a brand ambassador for lucrative brands such as Vodacom. Automatically his woman and his children have also become brands (angalia 40 ya Tiffa na angalia makampuni yaliyo sponsor 40 ya Nillan). All this came through his hard work and creativity. He is becoming wealthier every year. His children and his family have a secured life and future.

Kaeni hapo mkimuongelea Ali Kiba na sauti yake. Yes ana sauti nzuri kushinda Diamond. Haya hiyo sauti inatamfikisha wapi kama hana ubunifu? Hana akili ya biashara...muziki ni talent na bila kufanya biashara utabaki unaimba for nothing. Kuweni na akili na mshaurini Ali vizuri. Mnafikir mki mponda Dai ndio Ali Kiba anafanikiwa? Diamond ameshapita yuko mbali mnoo.
Halafu mlivyo hamna akili mnamuita Dai mpenda kiki. Yes ana penda kiki, maana kiki zinampa fans wengi, zina fanya watu hata kama sio mashabiki wake wamuangalie wamfollow. Vodacom na makampuni makubwa wakiangalia wanamuona Dai anafuatwa na watu zaidi ya milion 2 kutoka kila pembe ya Africa. Who is a better person to carry their brand more than Dai?
Ndio maana nasemaga, Dai hajasoma mpaka chuo kikuu but ana akili sana za maisha. Na Mungu ana msimamia.
Kaeni hapo mkiandika mapost ya kumponda Dai na kumpaka Ali mafuta.... hata Dai aache mziki leo, Ali Kiba hamfikii mafanikio yake ng'oo. That's just how Ali Kiba is.
 
Back
Top Bottom