Dr. Mbando (Ag. CMO) katika hili ulikosea kujibu; Tuokoe kwani ni wajibu wako

Dr. Mbando (Ag. CMO) katika hili ulikosea kujibu; Tuokoe kwani ni wajibu wako

Whisper

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2009
Posts
502
Reaction score
207
Gazeti la Raia Mwema ktk toleo lililopita liliripoti kuwepo kwa dakarai mmoja anayejiita Bingwa wa magonjwa ya moyo (Consultant Cardiologist), ambaye weledi wake una utata. Kijana huyu baada ya kutapeli wanachi wengi wa Mbeya na kuivuruga Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kiasi cha wafanyakazi kutishia kufanya mgomo, alihamishiwa Hospitali ya mkoa wa Morogoro. Ameanzisha dispensari bubu na anachaji gharama za juu sana. Gazeti la Raia Mwema limeripoti kijana huyu akiendeleza utapeli wa kuweka rehani afya za watanzania kwa gharama kubwa sana ya fedha.

Kaimu Mganga Mkuu wa wizara dr. Mbando alipoulizwa na mwandishi alijibu hivi; nanukuu kwa ufupi
“Kushughulikia suala la serikali lazima tupate complain (malalamiko),“Sisi tukishughulikia tunaanzia wapi, wenye malalamiko watuandikie, kama ni mtu au mkoa.”

Sasa Dr. Mbando, unataka malalamiko gani? ni wanachi wangapi wanaweza kufahamu huyu ni daktari na huyu ni tabibu. Mbona kijijini kwetu hata nesi wa kiume tunamwita daktari?, Sasa magazeti tunayokununulia kwa pesa ya watanzania yanakusaidia nini wewe kama kiongozi?
Nilitegemea kuwa taarifa hii itakuwa ni mwanzo mnzuri kwako kuanzisha uchunguzi juu ya watu hawa wanaoweka rehani afya za watanzania.

Kitu anachofanya kijana huyu tapeli ni uuaji, na tunakuomba uingilie kati mara moja.

 
Kaimu Mganga Mkuu wa wizara dr. Mbando alipoulizwa na mwandishi alijibu hivi; nanukuu kwa ufupi
"Kushughulikia suala la serikali lazima tupate complain (malalamiko),"Sisi tukishughulikia tunaanzia wapi, wenye malalamiko watuandikie, kama ni mtu au mkoa."


Dr Mbando vipi unatuangusha, tunakutegemea sana, tunataka tukupe unaibu waziri wa afya baadae kidogo, chapa kazi uonyeshe makeke.
 
Back
Top Bottom