Mzalendomorogoro
Member
- Mar 15, 2018
- 26
- 36
Tanzania imepitia katika hatua kuu tatu kwenye mikakati ya kufanikisha maendeleo. Hatua ya kwanza ilianza mara baada ya kupatikana uhuru, hadi mwaka 1967 lilipotangazwa azimio la Arusha. Katika kipindi hiki, Tanzania ililenga zaidi katika kujenga umoja, mshikamano na heshima kitaifa. Nchi ilipata mafanikio kiasi ya ki-uchumi japokuwa kilimo kilikuwa dhaifu na viwanda vilikuwa havijaimarika.
Kilifuata kipindi ambapo Tanzania ilianza kufuata itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Katika kutekeleza itikadi hii, kukafanika zoezi la kutaifisha njia kuu za uchumi. Njia hizi ni pamoja na mabenki ya biashara, mashamba ya kilimo, usafirishaji, makumpuni ya kibiashara n.k. Ilidhaniwa kwamba utaifishaji ungepelekea mgawanyo sawa wa mali na mapato ya kitaifa. Ingeliwezesha serikali kusimamia na kutumia ziada inayozalishwa kutoka katika mashirika yaliyotaifishwa, kugharamia huduma za jamii kwa umma wote, na hivyo kuboresha maisha ya wananchi.
Sekta ya umma ikaanza kuendesha uchumi wa nchi. Kwa itikadi na sera za kijamaa, Tanzania ilifanikiwa sana katika kuboresha huduma za jamii kwa raia wake pamoja na kujenga umoja wa kitaifa wakati huu Tanzania ilikuwa na chuo kimoja kikuu cha Dar es salaam ambapo wanafunzi walikuwa wachache tofauti na tegemeo la serikali ambapo hat elimu iliokuwa inatolewa kipindi cha miaka ya 1970 ilifundisha sana sera ya ujamaa na kujitegemea pia kulikuwa na uchache wa shule bora , vituo vya ufundi.
Miaka ya 1970, mapungufu ya kiuendeshaji yaliashiria uwezekano wa kuanguka kwa uchumi siku za usoni. Mapungufu hayo yalijumuisha, sera mbaya ya kupanga bei, uwekezaji katika mashirika yasiyozalisha, kubanwa kwa sekta binafsi, na kufujwa kwa pesa za umma. Mashirika na makampuni yaliyotaifishwa hayakuzalisha ziada ya kutosha kama ilivyodhaniwa mwanzo.
Mafanikio yaliyopatikana miaka ya 1960 yakaanza kutetereka kwenye miaka ya 1970. Nchi ikaanza kupata matatizo makubwa ya kiuchumi kuanzia miaka ya 1990 serikali ilamua kuanzia mipango mballimbali ili kunusuru uchumi ikiwemo kupitishwa kwa sheria mpya ya mabenki na taasisi za fedha; kuongezeka kwa uwezo wa mabenki ya umma kujiamulia yenyewe masuala muhimu (autonomy) na kuongeza ushindani katika sekta ya fedha. Mabadiliko makubwa yaliyotokea ni pamoja na kuanzishwa kwa soko la mitaji na amana.
Katika kipindi cha mwanzo cha historia ya Tanzania ambapo uchumi ulimilikiwa na dola, serikali ilimiliki na kuendesha shughuli mbali mbali za kibiashara. Kufikia katikati ya miaka ya 1980, serikali ilikuwa ikiendesha mashirika 400 ya ki-biashara. Gharama za kuyaendesha mashirika hayo zilitumia sehemu kubwa ya bajeti ya serikali. Malengo ya kubinafsisha yalikuwa Kupunguza mzigo mkubwa kwa serikali. Mwaka 1984/85, serikali ilitoa Tshs. 6.3 billioni kwa ajili ya kuendesha mashirika ya umma. Kiasi hicho kiliongezeka kufikia Tshs. 50.3 billioni mwaka 1993/94, Kuwapa fursa Watanzania kuweza kuwekeza kwenye mashirika hayo. Kuongeza ufanisi, tija, na ubora wa bidhaa na huduma zinzozalishwa kwa kuyaongezea mitaji, teknologia pamoja na menejimenti nzuri.
Viwanda, shule, benki na mashirika mengine yote yalitaifishwa na serikali ya kipindi icho kwa lengo kuwa umiliki unafanywa na serikali peke ake baadhi wageni walirudi nchini kwao mfano shule zilizo taifishwa pugu sekondari, kkiwanda cha nguo cha urafiki, mategemeo ya kutaifisha hayakufanikiwa kuleta faida ya kuongezeka kwa uchumi zaidi kuleta athari kubwa
Matatizo yaliotokea Matatizo Yaliyoambatana na Zoezi la Ubinafsishaji · Wafanyakazi wengi kupunguzwa baada ya mashirika kubinafsishwa na kwa hivyo kuwepo kundi kubwa la watu wasiokuwa na ajira. · Baadhi ya wafanyakazi waliopunguzwa hawajalipwa mafao yao kwa ukamilifu. Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikifungua mashitaka mahakamani kuhusiana na zoezi zima la ubinafsishaji na ulipaji mafao. · Baadhi ya wafanyakazi hasa wa ngazi za chini wamekuwa hawauelewi mwenendo mzima wa zoezi la ubinafsishaji na kwa hivyo wakati mwingine hudhania kwamba wajumbe wa PSRC wamekuwa wakila njama na wanunuzi wa mashirika.
Kuanguka kwa ujamaa umefanya Mageuzi ambayo yamekuwapo Tanzania yamepelekea kuwa na uchumi unaoendeshwa kwa nguvu za masoko (market forces), na sekta mbali mbali zimerekebishwa ili kuendana na hali hiyo. Pamekuwapo na mageuzi katika sekta ya umma, kukua kwa sekta binafsi pamoja na mabadiliko ya miundo.
Upimaji wa kasi na mwelekeo wa mageuzi unategemea sana sekta husika na aina ya mageuzi. Kwa ujumla, katika sekta nyingi, mageuzi yamekuwa ya haraka na ya jumla. Hata hivyo, ubinafsishaji umekuwa wa taratibu ukilinganisha na malengo ya awali. Marekebisho ya muundo wa utumishi serikalini nayo hayajakwenda kwa kasi. Tathmini ya kipindi cha mpito kuelekea kwenye mageuzi kamili hapa Tanzania inabainisha mambo kadhaa.
Kwanza, mageuzi bado yanaendelea na kwa hivyo tathmini kamili hiwezi kufanywa sasa. Pili, sababu za kisiasa na nyinginezo ambazo si za kiuchumi zinachangia kwa kiasi kikubwa kwenye mwenendo mzima wa mageuzi. Mafanikio ya mageuzi Tanzania yatahitaji serikali iimarishe zaidi nafasi yake katika majukumu yake na sio kujitoa katika kila kitu na kuiachia sekta binafsi. Kipaumbele lazima kiwekwe kwenye sera nzuri na utekelezaji unaozingatia ukweli na uwazi.
Tanzania imeendelea kukua kiuchumi mnamo mwaka 2022 Tanzania ilitangazwa kuwa imeingia katika uchumi wa kati baada ya mchango mkubwa wa serikali na mashirika binafsi mfano IPP media , METL, GSM, AZAM, AZANIA na mashirika mengine binafsi.