Dr. Mpango hapa umetupanga 100%, huwezi kuacha umakamu wa Rais ili uende kulima. Vipi umefukuzwa?

Kuna vitu ukivisikia tu, hapo hapo akili inakataa. Dr. Philip Mpango, makamu wa Rais wa Tanzania ameamua kufunguka sasa kwa kueleza wazi yeye mwenyewe (sio kusemewa tena) kuwa, kwa sasa anakwenda kustaafu nafasi ya makamu wa Rais, hivyo kuanzia November baada ya uchaguzi mkuu kwisha hatarejea tena kwenye hiyo nafasi na atakwenda kujikita na kilimo cha uzeeni.

Kwanza tuweke sawa, kwa mazingira ya kisiasa yanayozunguka nafasi yake, hakupaswa kusema anastaafu. Alipaswa kusema hana mpango wa kutaka kuomba ili kupewa tena hiyo nafasi baada ya kipindi cha muda wake kwisha.

Hoja kuu hapa ni kutaka kujua, nini msukumo uliopelekea Dr. Mpango kusalimu amri mapema sana wakati muda na sababu za kuendelea kuishikiria hiyo nafasi upo?

Dr. Mpango anasema, anajipanga kwenda kufanya kilimo mara baada ya muda wa kipindi cha makamu wa rais kwisha. Hoja hizo ni dhaifu sana kwa sababu;
1. Umri wa kufanya kilimo Dr.Mpango hana. Mstaafu wa serikalini na kilimo cha kitanzania (jembe na samadi) wapi na wapi?

2. Afya ya kufanya kilimo hana.
Sote tunajua kilichomkuta na kumuachia athari mbaya kiafya. Kwa afya ile akaingie shambani kulima atakuwa anatafuta nini?

3. Historia ya kufanya shughuli za kilimo hana. Muda mwingi ameutumia katika kusoma sana, kutumikia serikalini na kumalizia kwenye siasa.

4. Sababu za kujikita na kilimo hazipo. Kama ni kutafuta kipato cha kujikimu, sote tunajua Dr. Mpango ataendelea kulipwa mpunga mrefu na marupurupu kibao mpaka mwisho wa maisha yake.

Ukiwaza kwa kina, utagundua kuna namna Dr. Mpango ametupanga vilivyo hapa. Kwa haraka sana wengi tunahisi mwamba huenda amefukuzwa au ameshinikizwa kuachia kijiti.

Muda utakuja kutupa majibu mazuri zaidi.
Rostam anakujibu soon
 
Sababu za yeye kukimbia kiti alizitoa bibi chau mwenyewe alisema jamaa anapenda kuendelea kuishi maisha marefu, bahati mbaya amekosea hesabu maana utabiri umeshatoka tayali pengine na yeye angepanda pale
 
Kuhusu kulima , kwa yeye haitaji nguvu za mwili bali kutoa maelekezo tu.

Na kuhusu ujuzi , anaweza kutumia wataalamu wapo vijana wengi wamesomea kilimo na mifugo anaweza kuwatumia ili atimize maono yake.

Kuhusu kufukuzwa au kuachishwa kwa nguvu .

Jibu linaweza kuwa ndiyo au hapana Ila kwa nature ya Kazi ya umakamu inamuhitaji MTU strong hasa kiafya hivyo Dr Mpango pamoja na kuwa na busara kubwa Ila Afya yake ya mwili inahitaji utulivu.

Kuacha kwa matakwa yake
Kuachishwa
Kushinikizwa na familia

Yote haya yanaweza kuwa majibu.
Jambo moja nauhakika kuhusu wewe ni mtu makini
 
Ataongea kama Ex CAG Assad muda ukifika,naye alisema anaenda kulima bamia.

NB:Kilimo cha viongozi wakuu wastaafu siyo hicho cha yeye kushinda shamba,JK alipo analima na kufuga tena Dom na Pwani.
 
Kuna vitu ukivisikia tu, hapo hapo akili inakataa. Dr. Philip Mpango, makamu wa Rais wa Tanzania ameamua kufunguka sasa kwa kueleza wazi yeye mwenyewe (sio kusemewa tena) kuwa, kwa sasa anakwenda kustaafu nafasi ya makamu wa Rais, hivyo kuanzia November baada ya uchaguzi mkuu kwisha hatarejea tena kwenye hiyo nafasi na atakwenda kujikita na kilimo cha uzeeni.

Kwanza tuweke sawa, kwa mazingira ya kisiasa yanayozunguka nafasi yake, hakupaswa kusema anastaafu. Alipaswa kusema hana mpango wa kutaka kuomba ili kupewa tena hiyo nafasi baada ya kipindi cha muda wake kwisha.

Hoja kuu hapa ni kutaka kujua, nini msukumo uliopelekea Dr. Mpango kusalimu amri mapema sana wakati muda na sababu za kuendelea kuishikiria hiyo nafasi upo?

Dr. Mpango anasema, anajipanga kwenda kufanya kilimo mara baada ya muda wa kipindi cha makamu wa rais kwisha. Hoja hizo ni dhaifu sana kwa sababu;
1. Umri wa kufanya kilimo Dr.Mpango hana. Mstaafu wa serikalini na kilimo cha kitanzania (jembe na samadi) wapi na wapi?

2. Afya ya kufanya kilimo hana.
Sote tunajua kilichomkuta na kumuachia athari mbaya kiafya. Kwa afya ile akaingie shambani kulima atakuwa anatafuta nini?

3. Historia ya kufanya shughuli za kilimo hana. Muda mwingi ameutumia katika kusoma sana, kutumikia serikalini na kumalizia kwenye siasa.

4. Sababu za kujikita na kilimo hazipo. Kama ni kutafuta kipato cha kujikimu, sote tunajua Dr. Mpango ataendelea kulipwa mpunga mrefu na marupurupu kibao mpaka mwisho wa maisha yake.

Ukiwaza kwa kina, utagundua kuna namna Dr. Mpango ametupanga vilivyo hapa. Kwa haraka sana wengi tunahisi mwamba huenda amefukuzwa au ameshinikizwa kuachia kijiti.

Muda utakuja kutupa majibu mazuri zaidi.
Naamini hajafukuzwa.Na kama angelifukuzwa asingendelea na kazi.Huenda dhamira ya mh.Makamu imesema naye na wamekubaliana Siku ikifika tutamtakia heri kwa utumishi mwema
 
Back
Top Bottom