Wakuu wote hapa heshima mbele,
- Tafadhalini sana tunahitaji kuwa wastaarabu na waangalifu kwa sababu kwa mwendo ninauona hapa, kuna hatari ya kuwaharibu viongozi imara sana hapa yaani DK na George, ninasema wote ni watu makini sasa tuache tabia zilizokataliwa na Obama juzi kule Accra, za ku-invest kwenye majina badala ya institutions na sound policies, Obama amesema wazi kwamba Africa hatuhitaji majina makubwa au dictators na that is exactly kuna mnaokifanya na hizi kampeni chafu.
- Hakuna mahali popote ambapo George ametangaza kwamba anagombea ubunge wowote ule, sasa hata wale mnaomuongelea hamumsaidii hata kidogo, na wale mnaomuongelea DK ndio kabisa mnanishangaza sana, shujaa wa taifa kama yeye kweli anahitaji hizi cheap kampeni namna hii? Ukweli ni kwamba mnamshusha hadhi na hizi nyepesi nyepesi.
- Tufike mahali tuwajali wananchi wa Kyela kwanza, badala ya ubinafsi wetu wao ndio waamuzi kwamba nani anawafaa, na besides hivi sio vita wala ugomvi kwa sababu DK alimngóa Mwakipesile na hakukuwa na tatizo, kwamba amemuonea jimbo lake sasa kwa nini mnataka kuligeuza hili jimbo kuwa ni la DK badala ya wananchi wa Kyela? Ninamheshimu sana DK na kazi yake kwa taifa, lakini sijui sana huko jimboni, na pia ninamheshimu sana George na idea zake iwapo ataamua kugombea kama inavyotabiriwa hakuna ubaya wowote, na yes niko in contact naye kila siku ya Mungu,
- Anaendelea na likizo yake, najua leo yuko Arusha sasa tuache majungu na wewe unayechochea sana kwamba ametumwa ni vyema ukaacha hayo majungu mkuu, kwa sababu huna ushahidi wala dataz ya hizo sumu unazozitema sana, Rostam aliamua kuacha ubunge lakini mafisadi wenziwe wamemwambia kwenye kikao cha siri kuwa akiacha tu ajue anatinga Segerea kwa hiyo anagombea na ameshaanza kampeni za chini chini, Lowassa anajua sana kwamba akitoka tu jimboni mwake anaondoka na maji, Nchimbi naye anajua maji ni ya shingo kwa hiyo hakuna wa kuacha jimbo lake kwenda la mwingine au kumsaidia mwingine,
- George akiamua kugombea ni sawa kabisa kwa sababu itakuwa vichwa viwili vinapiganishwa na matokeo tutapata ukweli mtupu na itakuwa kampeni of the Century, watakaofaidika ni wananchi wa Kyela na vita hivyo kama vitatokea, na Mungu awajalie wote yaani DK na George, ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi Kyela, maana hata bila ubunge George atawasaidia sana wananchi wa huko Kyela pamoja na umasikini wake kwa sababu ni mkweli na ni committed kwa maendeleo ya Kyela.
Otherwise, ninamtakia heri DK kwa kupona na arudi haraka bungeni na kuendeleza libeneke, na pia ninamtakia George likizo njema na hasa safari nyingi alizonazo, sijui hata kama atapumzika kabla ya kurudi nyumbani.
Respect na Likizoni, tuache uzushi tuwajali wananchi wa Kyela.
FMES! Ni Wazee wa sauti ya umeme!