Haki na uongozi bora vinakuwepo pale tu ambapo utekelezaji wa sheria hauangalii cheo au sura ya mkosaji.
Kwa Tanzania tumefika mahali ambapo kosa linategemea cheo cha mtu na hilo ni hatari kweli kweli.
Wengine tumeshuhudia hapa UK, jinsi posho ndogo tu zilivyowayumbisha wabunge na mpaka karibu wabunge 200 kati ya 650 kulazimika kuachia ngazi hapo mwakani.
Maneno ya Spika ndiyo yamenitisha zaidi, kwamba mbunge ni mtu mkubwa na hata kuhojiwa kwake lazima kufanywe na watu wakubwa. Nijuavyo mimi sheria haina mkubwa wala mdogo na lazima watu wote wawe sawa mbele ya sheria.
Kutokana na kukiukwa kwa misingi hii ya haki sawa kwa wote, leo hii bunge letu lina criminals ambao walitakiwa kuwa jela, lakini wanapeta bungeni. Leo hii serikalini kuna watu ambao wanaona hawana sababu za kufuata sheria walizotunga wenyewe. Akina Chenge na kashfa zote hizo bado wako bungeni. Akina Zombe wanatoka huru mahakamani pamoja na ushahidi wote, akina Ditopile wanabadilishiwa mashitaka kwasbabu tu ni watu wakubwa, huku maskini kibao waliosingiziwa kesi za kuua wanasota mahabusu miaka na miaka.
Spika anataka kabla ya wabunge kuhojiwa mpaka yeye apewe taarifa kwanza, mbona hakusema hivyo walipohojiwa akina Mramba? Anatakiwa apewe taarifa ili awatonye wahusika?
Lazima kuwe na sheria moja kuanzia sisi maskini mpaka kule juu kwa rais. Tupige kelele hizo sheria zisipotekelezwa kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa mafisadi lakini jitihada ya kuhalalisha wizi wowote inaonyesha hatuko serious na hivyo vita tunavyojidai tunapigana navyo.