Mganga maarufu wa tiba za asili maarufu kama Dr. Francis Mwandulame wa Iringa amemjia juu babu kwa kitendo chake cha kuwahadaa watanzania kwamba amepewa ufunuo toka kwa Mungu. Gwiji huyo wa mitishamba anayetisha kusini mwa Tanzania amedai kuwa huo mti wa mugariga anaotumia babu yeye mwenyewe ameanza kuutumia kutiba watu maradhi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 8 sasa. Anasema kuwa alioteshwa na marehemu mama yake, na kwamba unapatikana pia huko Iringa. Hivyo amemtaka babu kuacha kuwadanganya watu kuwa mti huo ni ufunuo wa Mungu. Anadai kwa babu wa Loliondo haoni jipya zaidi ya kutangazwa sana na vyombo vya habari.
Katika hatua nyingine Mwandulame amevishutumu vyombo vya habari na serikali kwa kushiriki kumtangaza mganga wa tiba za kienyeji. Ameyashutumu magazeti, TV na redio kwa kumtangaza babu huku waganga wengine wakitozwa pesa lukuki kwa ajili ya matangazo. Pia ameishukia serikali kwa kuruhusu babu kujitangaza kutibu magonjwa sugu na hata kushiriki kumtangaza wakati waganga wenzake wa jadi wamezuiliwa kufanya hivyo. Ameonya kuwa kama hali itaendelea hivyo itabidi na wao waanze kujitangaza bila kufuata taratibu.
Source: WAPO Radio - Kipindi cha matukio - 07:15 A.M
1 Cor 2:2 For I determined not to know any thing among you, save Jesus Christ, and him crucified.