...labda hujijui kwamba hutaurithi ufalme huokwa kweli kwa hili la serikali kumkumbatia mganga mmoja tu (na karibu baraza zima la mawaziri lilmeishakunywa kikombe), limenisikitisha sana
si kila mtu aniitaye "Bwana", "Bwana" ataurithi ufalme wa Mungu
bali yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni
jambo hili ni gumu halihitaji hukumu ya haraka. Kwa ubinadamu wetu lazima tuweweseke, lakini hebu tuangalie mazingira yake. Dawa ya babu inafahamika kama ni tiba kwa miaka mingi lakini si kwa dose moja kama afanyavyo babu. hii ndio ajabu ambayo haina majibu ya haraka. kwa mcha Mungu yeyote atabariki chakula kabla ya kula hata kikiwa na sumu haitadhuru, biblia inatueleza hivyo. babu anagawa dawa baada ya kuchemsha na kuibariki hatangazi dini kosa ni lipi! shetani anaingiaje hapa? Mungu ni dhaifu kuliko shetani hata ashindwe kusimamisha hili? Mbona wengi wamelaani na hata kufunga ili huduma ikome mbona inazidi kushamiri!!? Waganga wengi toka karne za nyuma kwa asilimia kubwa wameoteshwa hizo tiba je waliinuliwa kama babu? Mwacheni Mungu aitwe Mungu. Kwa kifupi dawa inahitaji imani mwenye imani anywe nawe usie na imani ukae kimya usije kujikuta unagombana na bosi wako (God)
Hana hoja yoyote, soko lake tu limeyumba.
Kwani yeye anakosa nini kama si kukosa soko?
kwa kweli kwa hili la serikali kumkumbatia mganga mmoja tu (na karibu baraza zima la mawaziri lilmeishakunywa kikombe), limenisikitisha sana na sasa natambua wazi kuwa ushirikina umejikita sana mioyoni mwa viongozi wetu na wengi wetu
si kila mtu aniitaye "Bwana", "Bwana" ataurithi ufalme wa Mungu
bali yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni
Samahani jamani, ni Dr Mwandulame yupi, kwani nasikia yupo mmoja Mtwango kule Njombe, mwingine Dar na mwingine yuko Mwanza.
mi nadhani wanamaanisha wa kule mtwango-Njombe hao akina mwandulami wengine wapo kweli? mi sijawahi kuwasikia
ok, wana mtandao mkubwa lakini wameshindwa kumfunika babu
kwa kweli kwa hili la serikali kumkumbatia mganga mmoja tu (na karibu baraza zima la mawaziri lilmeishakunywa kikombe), limenisikitisha sana na sasa natambua wazi kuwa ushirikina umejikita sana mioyoni mwa viongozi wetu na wengi wetu
si kila mtu aniitaye "Bwana", "Bwana" ataurithi ufalme wa Mungu
bali yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni
Sijakuelewa vizuri Miss,kutumia mitishamba kama mugariga ni ushirikina?
Mganga maarufu wa tiba za asili maarufu kama Dr. Francis Mwandulame wa Iringa amemjia juu babu kwa kitendo chake cha kuwahadaa watanzania kwamba amepewa ufunuo toka kwa Mungu. Gwiji huyo wa mitishamba anayetisha kusini mwa Tanzania amedai kuwa huo mti wa mugariga anaotumia babu yeye mwenyewe ameanza kuutumia kutiba watu maradhi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 8 sasa. Anasema kuwa alioteshwa na marehemu mama yake, na kwamba unapatikana pia huko Iringa. Hivyo amemtaka babu kuacha kuwadanganya watu kuwa mti huo ni ufunuo wa Mungu. Anadai kwa babu wa Loliondo haoni jipya zaidi ya kutangazwa sana na vyombo vya habari.
Katika hatua nyingine Mwandulame amevishutumu vyombo vya habari na serikali kwa kushiriki kumtangaza mganga wa tiba za kienyeji. Ameyashutumu magazeti, TV na redio kwa kumtangaza babu huku waganga wengine wakitozwa pesa lukuki kwa ajili ya matangazo. Pia ameishukia serikali kwa kuruhusu babu kujitangaza kutibu magonjwa sugu na hata kushiriki kumtangaza wakati waganga wenzake wa jadi wamezuiliwa kufanya hivyo. Ameonya kuwa kama hali itaendelea hivyo itabidi na wao waanze kujitangaza bila kufuata taratibu.
Source: WAPO Radio - Kipindi cha matukio - 07:15 A.M
1 Cor 2:2 For I determined not to know any thing among you, save Jesus Christ, and him crucified.