Pre GE2025 Dr. Nchimbi: Rais Samia kwa mapenzi yake kwa watu wa Ruvuma alikataa kubadili ratiba ili aende Marekani ambapo jana angehutubia UNGA!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi amemshukuru Rais Samia Kwa kukataa ushauri wa kubadili ratiba Ili aende Marekani ambapo jana angehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Kwa niaba yake hii hotuba imesomwa huko Umoja wa Mataifa :

Ujumbe wa 4R, Uchaguzi 2024 pia 2025, Matumaini, Utu kwa Wote na Amani kwa Dunia Yote Uliotolewa na Tanzania UNGA79

Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akihutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa la 79 jijini New York nchini Tanzania :


View: https://m.youtube.com/watch?v=tGE2Y4GwALY
Kassim Majaliwa Majaliwa,Prime Minister Of The United Republic Of Tanzania, Addresses The General Debate Of The 79th Session Of The General Assembly Of The United Nations (New York 24-30 September 2024)
Malengo endelevu na ushirikishwaji wa wote, utu wa mtu na watu wote, utatuzi wa migogoro, amani, ukosefu wa chakula .... haki kwa wote, uwajibikaji, Haki ya Kuishi ili Kufikia Matarajio yao yote msishani ni tamko Tanzania inasisitiza asema waziri mkuu wa Tanzania akihutubia Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa akimuwakilisha rais Samia Hassan katika kutano hilo muhimu la kila mwaka ....

Kuhusu uchaguzi wa November 2024 wa serikali za mitaa na ule uchaguzi mkuu wa 2025, waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ameihakikishia Dunia na Jumuiya ya kimataifa kupitia mkutano wa UNGA 79 kuwa chaguzi zitakuwa wazi, huru na wa haki kwa vyama vyote vitavyoshiriki ...
 
Hapa tunaongopewa mchana kweupe. Samia kamuogopa mange Kimambi na kundi lake la maandamano kupinga mauaji na utekaji.
 
Hii inaonyesha wapangaji Ratiba za Taasisi ni "wahuni" na wateteaji WA hili nao ni "wahuni" ndio maana Haraka Haraka alizungumzia uwepo wa "wahuni" katika Sirikali ya awamu hii, akaishia kukimbizwa nje ya nchi awape nafasi " wahuni" wafanye KAZI zao za kihuni bila kusongwa songwa
 
UWT wajitokeze wajibu hili
 
Anataka kutwambia UNGA iliitishwa ghafla Bila taarifa...hiyo ni sawa na kumsifia Mbunge aliyeamua kutoshiriki Bunge la Bajeti na kuamua kufanya ziara katika kata fulani kwa kisingizio cha upendo kwa wapiga kura wake...Na Bila shaka watu walishangilia sana
 
Kumbe na nchimbi nalo takataka! Ameacha kwenda UNGA sababu ya mapenzi, bladifaken kumbe naye!
 
Samia aanza kukwepa safari za nje kama alivyokuwa Magufuli.
 
Ukiwa ccm kidogo lazima dish liyumbe sijui kwanini
 
Hilo ni dongo katupiwa Kizimkazi kiaina! Siasa ziko hivyo ukipata nafasi unakusumiza jab ionekane unasifia kumbe...walaaah!

Uliona wapi Rais wa nchi anaacha kwenda kwenye hafla muhimu kisiasa tena kwa ndege ughaibuni kuhutubia mkutano mkuu wa mwaka wa UNGA, podium moja na mwamba Benjamin Netanyahu ukimbilie mikutano ya Peramiho, Mpitimbi na Magagula? ๐Ÿ˜ฒ๐Ÿ˜ฎ๐Ÿคฏ
 
Kwa mapenzi ya madaraka. Hakuwa na hakika juu ya matokeo ya maandamano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ