Dr. Ndalichako na waandishi wetu wa habari

Hess

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
593
Reaction score
675
Wana jamvi,

Kumekuwa na mtazamo hasi na dhaifu wa utendaji wa Dr. Ndalichako na Baraza la Mtihani Tanzania NECTA hasa kutoka kwa watu wanaojiita WACHAMBUZI na wengine hujiita Wasomi. Wengi wao wanatoa uchambuzi wao kulaumu (NECTA) bila hata kujua nini NECTA wanashughulikia.

Gazeti la leo la MAWIO, na 0056, gazeti nisilolikosa kila wiki, gazeti linalopendwa na wazalendo na kuchukiwa na watawala limeingia katika mtego huu kwa kutoa maoni yao kuhusu Dr. Ndalichako:

1. MAWIO wanamlaumu Dr. Ndalichako na NECTA kwa ujumla wake kwa makosa ya mtihani wa MOCK kwa wilaya 40 ambapo maswali yakiluwa hayajibiki. Huu ni udhaifu wa wahariri wa MAWIO kutojua nani anahusika na mitihani wa MOCK. Kwa taarifa tu, mitihani ya utimilifu (MOCK) si mitihani ya NECTA bali huandaliwa na TAHOSSA, Tanzania Heads of Secondary Schools Association. Hawa ndo wanawajibika na MOCK si NECTA. Tusiwahukumu kwa wasilohusika nalo. TAHOSSA kila kanda hufanya mitihani hii na bajeti yao ni pesa ya wazazi.

2. MAWIO na hata baadhi ya wasomi wetu wasiojua ABCs za NECTA, wanalilaumu baraza kwa kufeli wanafunzi wengi kidato cha nne. NECTA na Ndalichako wanaingiaje hapa? NECTA ni Measurement and Evaluation organ, wanatumia sylabus iliyoandaliwa na Taasis ya ukuzaji mitaala kwa sera na miongozo ya Wizara ya Elimu. Wanatunga mitihani bila kujali mwanafunzi kasoma au hajasoma, katoka St. Kayumba au St. George, kamaliza sylabus au la, shule ina walimu au la. Wanatunga mtihani kwa kufuata sylabus na kuusahihisha then hutoa matokeo. Si kazi yao kujibu kwa nini wanafunzi wamefeli.

Kwa kilicotoke mwaka jana, serikali yetu iliamua kuwaburuza kwa kuficha aibu. Wakabadili formula, kama kuna mwanafunzi alifeli au kufaulu baada ya kurudia kumark si kazi yao maana marking quide yao ndo mwongozo wa marking.

3. MAWIO na wengi wa aina mtazamo huu wanalaumu eti elimu haitapanda kama hakuna upatikanaji wa vifaaa vya kufunzia na kujifunzia. Baraza linaingiaje hapa. Tuwe wasomi na wachambuzi wa kweli si kubeza kitu bila kukijua.

4. MAWIO wanalaumu kuwa kuna walimu wamefaulu hawana sifa. Si walimu wote wanahitimu ualimu toka mikononi mwa NECTA. Kuna wengi wamepita vizuri kwenye mitihani ya NECTA na walikuwa wazuri. Wamekuwa vilaza vyuoni maana elimu ya chuo kikuu haina uhusiano na NECTA. Mhadhiri ndo NECTA na ndio humtoa mwalimu.

5. MAWIO wanasema baraza limeshindwa kudhibiti viwango wakati nchi nzima wanalia ufaulu umeshuka, nani ameonyesha kuwa ufaulu umeshuka? NECTA ndo wametuonyesha hakuna kitu katika mashule yetu so TUWAPONGEZE.

6. Kuna dini moja wanataka Ndalichako ajiuzuru eti ANAKAMATA wanafuzi wa dini hiyo. Mawazo dhaifu. ni lini na wapi kuna majina wakati wa kusahihisha mitihani ya NECTA? Hivi hakuna wafanyakazi wa dini hiyo pale baraza? Mbona wapo wengi tu. Uwezo mdogo wa wanafunzi wetu na udhaifu wa shule zetu isibadilishwe kuwa lawama kwa Dr. Ndalichako.

Dr. Ndalichako anafanya kazi kubwa sana. Nani aseme leakage ya mitihani ya NECTA leo ikoje ukilinganisha na miaka ya nyuma? Tuseme ukweli, bila Dr. Ndalichako kusimama na kufanya kazi, kwa serikali yetu hii ya mbwembwe shule za kata zingekuwa zinatoa flying colour kuficha udhaifu. Big up Dr, usikate tamaa kwa uchambuzi dhaifu.

Kuna mwandishi mmoja wa radio moja (Soma kituo cha matangazo) anaitwa Gerald Hando, kwa ufinyu wa kufikiri na kutoelewa mambo ya elimu na mgawanyo wa kazi, alimlaumu mama Ndalichako eti kwa kuonyesha picha za Zombi. Hando anasema huyu mama hafai alitakiwa aje na mikakati ya kudhibiti hili si kuonyesha zombi. Nilijiuliza kama Hando ana uelewa wa kazi za NECTA na nani anatakiwa azuie MAZOMBI. Ndalichako was right kuumbua wale waliotakiwa kuzuia Zombi.

WANDISHI wengi wa Tanzania wameingia kwenye fani kuuza sura tu au kuganga njaa. Wengi hawana uelewa wa mambo mengi na wakitumia kalamu zao kupotosha umma. Kama hujui unachokichambua kwa kina UTAPOSHA. Kwa hili MAWIO mmechemka.

Kwa taarifa tu kuna WIZARA YA ELIMU, TAMISEMI, TIE, NECTA, EMAC, TAHOSSA, na wadau wengine kila mtu kwa nafasi yake wanatakiwa wafanye kazi. NECTA is all about Measurement and Evaluation. Mliosoma ualimu mnajua nasema nini, mtakuwa mnamkumbuka Prof. Omary.

Tumtendee haki Dr. Ndalichako na NECTA in general na tumhukumu anapoboronga kwenye sehemu yake, japo si msemaji wake nalazimika kuwaambia wasiojua wakae kimya. TOA HOJA
 
Nashukuru kwa kuweka wazi majukumu ya NECTA. Kuna watu huwa wakiitisha makongamano yao, ajenda ya kuandamana kwenda kumng'oa Ndalichako kule NECTA huwa haikosekani, ukiuliza kwa nini, eti wanafunzi 'wao' wanafeli! Sasa shule zenu zenyewe ajira ya mwalimu inategemea imani yake, unategemea nini hapo? Joseph Selasini (Mb) aliwahi kuweka sawa maelezo, lakini wabunge 'wale' wakang'ang'ania kuwa sio Kawambwa, ni Ndalichako! ... kisa, Kawambwa ni 'mwenzetu'
 
Makala au hoja kama hizi ndiyo ninapenda kusoma. Hakuna cha kupingwa hata kimoja hapo.

1. Hivi ni nani aliyewaroga waandishi wetu kuandika utumbo kama huo eti MOCK huandaliwa na NECTA.
2. Toka lini mtu anayekuonesha kasoro iko wapi akawa adui.
3. Vitabu shuleni hakuna, walimu hakuna analaumiwa Ndalichako. Basi mpeni Uwaziri wa Elimu tujue moja kama mnaona anafiti mambo yote hayo. Maana hapa Tanzania kuna idara na Taasisi chini ya MOEVT wakuu wake wanakula raha kweli. Hwana hata ulinzi kutwa wapo viwanja hawana maadui wakati tuhuma nyingine kama mitaala zinawahusu wao lakini Mama wa watu anabebeshwa mzigo. Mnataka afanye nini kw anchi hii ili mjue anafanyakazi.

Mama wa watu nilisikia kwenye warsha moja wakiongea wakati mwingi halali anakesha ofisini akitumikia Taifa ili tu mitihani iende kama ilivyopangwa, wakati huo watoto wao wachora mazombie wamakoroma wakiota kuchora badala ya kujisomea, halafu eti mtangazaji mmoja na elimu yake ya kuunga unga anahoji kwanini alimuumbua mdogo wake kwenye media.

Utafika wakati kwa uandishi huu tutakuwa tunasikiliza na kuangalia BBC pekee, tukimaliza hapo mpira EPL.

Kwa kweli mkuu Hess ningeomba kuku-add kwenye kolamu yangu ya Friends kama hutajali.
 
Na vipi kuhusu uozo wa Islamic knowledge 2012?
Katika mambo ambayo Dk. Ndalichako alikiri kinyume na wengi wa viongozi wetu ni hilo na hatua zikachukuliwa marekebisho yalifanyika na tukayaona. Muhusika wa mifumo akawajibishwa au ulitaka kilakosa likitendeka hata na mtumishi wa chini basi kiongozi ajiuzulu? Nchi hii mwisho tutawaita wazungu waje kuwekeza hata na kwenye uongozi.
 
UCHAMBUZI ULIOFANYA INGEKUWA AMRI YANGU, ningekupa hadhi aliyonayo Shaban Robert, kwani kuandika sio maandishi mengi bali uhai wa hoja iliyoko kwenye maandishi hayo.

Ulionena hapa yataishi siku nyingi kwani ni WACHACHE sana wanaoweza kuchallenge MAWIO na kuungwa mkono.
Hongera, Usiwe kama Mwanakijiji hata kwenye YES lazima atasema NO.
 
Aise ninyi ndo mnahitajika mkuu.ni zaidi ya uchambuzi,hi makala iongezee manjonjo iweke kama barua kwa muhariri ibandikwe gazetini watu wapate elimu.big up
 

wamechoka kuongozwa na wakristo, wanataka sasa iwe zamu ya sheikh ponda !
 
Kuna wengine mpaka post za kwenda f5 zlvyochelewa walikuwa wanailaunu NECTA wakat hawajui kuwa NECTA kazi yao n kutunga na kusahihisha mitihani waliotunga tu
 
Mimi naomba kutoa hoja:

Kwa kuwa imekuwa ni kawaida sasa kila tatizo la kielimu kutupiwa Dr. Ndalichako hata kama linahusu idara na taasisi nyingine zilizopo chini ya Wizara ya Elimu. Je mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haoni kwamba ni wakati muafaka sasa kumteua Dk. Ndalichako kuwa Mbunge wa viti maalumu kama alivyofanya kwa Dk. Mgimwa na Prof. Muhongo na kumteua moja kwa moja kuwa WAZIRI WA ELIMU?

Maana wananchi wengi wamekuwa na imani naye kwamba yeye ndiye suluhisho kwa kila tatizo la Elimu lakini tofauti na matarajio yao hana rungu hilo, ni wakati mwafaka sasa apewe rungu hilo.

Naomba kutoa hoja.

CC: Waheshimiwa wote humu wakiongozwa na Hess.
 
Umenena vyema mkuu ni kweli tasnia ya elimu tanzania hasa suala la utahini lisingekuwa na ubora iliyonayo sasa bila msaada wa Dr Ndalichako..................Hail Dr Ndalichako!!!!!!
 
tatizo la nchi hii ukiwa mtendaji mzuri maadui wanakua wengi kila kukicha. binafsi namkubali sana yule mama ni muwazi na ni mchapa kazi pia ni mzalendo mwenye lengo la kuleta mabadiliko kwnye elimu nadhan muda umefka wa kumpa wizara
 
Ni wakati sasa wa jk kumpa hii wizara Dr Ndalichako coz katika wizara nzima kwenye kila idara yeye ndo anatupiwa lawama zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…