Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana jamvi,
Kumekuwa na mtazamo hasi na dhaifu wa utendaji wa Dr. Ndalichako na Baraza la Mtihani Tanzania NECTA hasa kutoka kwa watu wanaojiita WACHAMBUZI na wengine hujiita Wasomi. Wengi wao wanatoa uchambuzi wao kulaumu (NECTA) bila hata kujua nini NECTA wanashughulikia.
Gazeti la leo la MAWIO, na 0056, gazeti nisilolikosa kila wiki, gazeti linalopendwa na wazalendo na kuchukiwa na watawala limeingia katika mtego huu kwa kutoa maoni yao kuhusu Dr. Ndalichako:
1. MAWIO wanamlaumu Dr. Ndalichako na NECTA kwa ujumla wake kwa makosa ya mtihani wa MOCK kwa wilaya 40 ambapo maswali yakiluwa hayajibiki. Huu ni udhaifu wa wahariri wa MAWIO kutojua nani anahusika na mitihani wa MOCK. Kwa taarifa tu, mitihani ya utimilifu (MOCK) si mitihani ya NECTA bali huandaliwa na TAHOSSA, Tanzania Heads of Secondary Schools Association. Hawa ndo wanawajibika na MOCK si NECTA. Tusiwahukumu kwa wasilohusika nalo. TAHOSSA kila kanda hufanya mitihani hii na bajeti yao ni pesa ya wazazi.
2. MAWIO na hata baadhi ya wasomi wetu wasiojua ABCs za NECTA, wanalilaumu baraza kwa kufeli wanafunzi wengi kidato cha nne. NECTA na Ndalichako wanaingiaje hapa? NECTA ni Measurement and Evaluation organ, wanatumia sylabus iliyoandaliwa na Taasis ya ukuzaji mitaala kwa sera na miongozo ya Wizara ya Elimu. Wanatunga mitihani bila kujali mwanafunzi kasoma au hajasoma, katoka St. Kayumba au St. George, kamaliza sylabus au la, shule ina walimu au la. Wanatunga mtihani kwa kufuata sylabus na kuusahihisha then hutoa matokeo. Si kazi yao kujibu kwa nini wanafunzi wamefeli.
Kwa kilicotoke mwaka jana, serikali yetu iliamua kuwaburuza kwa kuficha aibu. Wakabadili formula, kama kuna mwanafunzi alifeli au kufaulu baada ya kurudia kumark si kazi yao maana marking quide yao ndo mwongozo wa marking.
3. MAWIO na wengi wa aina mtazamo huu wanalaumu eti elimu haitapanda kama hakuna upatikanaji wa vifaaa vya kufunzia na kujifunzia. Baraza linaingiaje hapa. Tuwe wasomi na wachambuzi wa kweli si kubeza kitu bila kukijua.
4. MAWIO wanalaumu kuwa kuna walimu wamefaulu hawana sifa. Si walimu wote wanahitimu ualimu toka mikononi mwa NECTA. Kuna wengi wamepita vizuri kwenye mitihani ya NECTA na walikuwa wazuri. Wamekuwa vilaza vyuoni maana elimu ya chuo kikuu haina uhusiano na NECTA. Mhadhiri ndo NECTA na ndio humtoa mwalimu.
5. MAWIO wanasema baraza limeshindwa kudhibiti viwango wakati nchi nzima wanalia ufaulu umeshuka, nani ameonyesha kuwa ufaulu umeshuka? NECTA ndo wametuonyesha hakuna kitu katika mashule yetu so TUWAPONGEZE.
6. Kuna dini moja wanataka Ndalichako ajiuzuru eti ANAKAMATA wanafuzi wa dini hiyo. Mawazo dhaifu. ni lini na wapi kuna majina wakati wa kusahihisha mitihani ya NECTA? Hivi hakuna wafanyakazi wa dini hiyo pale baraza? Mbona wapo wengi tu. Uwezo mdogo wa wanafunzi wetu na udhaifu wa shule zetu isibadilishwe kuwa lawama kwa Dr. Ndalichako.
Dr. Ndalichako anafanya kazi kubwa sana. Nani aseme leakage ya mitihani ya NECTA leo ikoje ukilinganisha na miaka ya nyuma? Tuseme ukweli, bila Dr. Ndalichako kusimama na kufanya kazi, kwa serikali yetu hii ya mbwembwe shule za kata zingekuwa zinatoa flying colour kuficha udhaifu. Big up Dr, usikate tamaa kwa uchambuzi dhaifu.
Kuna mwandishi mmoja wa radio moja (Soma kituo cha matangazo) anaitwa Gerald Hando, kwa ufinyu wa kufikiri na kutoelewa mambo ya elimu na mgawanyo wa kazi, alimlaumu mama Ndalichako eti kwa kuonyesha picha za Zombi. Hando anasema huyu mama hafai alitakiwa aje na mikakati ya kudhibiti hili si kuonyesha zombi. Nilijiuliza kama Hando ana uelewa wa kazi za NECTA na nani anatakiwa azuie MAZOMBI. Ndalichako was right kuumbua wale waliotakiwa kuzuia Zombi.
WANDISHI wengi wa Tanzania wameingia kwenye fani kuuza sura tu au kuganga njaa. Wengi hawana uelewa wa mambo mengi na wakitumia kalamu zao kupotosha umma. Kama hujui unachokichambua kwa kina UTAPOSHA. Kwa hili MAWIO mmechemka.
Kwa taarifa tu kuna WIZARA YA ELIMU, TAMISEMI, TIE, NECTA, EMAC, TAHOSSA, na wadau wengine kila mtu kwa nafasi yake wanatakiwa wafanye kazi. NECTA is all about Measurement and Evaluation. Mliosoma ualimu mnajua nasema nini, mtakuwa mnamkumbuka Prof. Omary.
Tumtendee haki Dr. Ndalichako na NECTA in general na tumhukumu anapoboronga kwenye sehemu yake, japo si msemaji wake nalazimika kuwaambia wasiojua wakae kimya. TOA HOJA
NECTA
(NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA)
Ndugu,
Nashawishika kusema hiyo title(NECTA) haitutendei haki Watanzania na sekta ya elimu kwa ujumla.
Kuitwa BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA ni jambo kubwa na tukufu sana.Hii imenipelekea kujiuliza maswali mengi mno;
1.Je Baraza lina udhibiti wa mitihani yote inayotungwa na kufahamika hapa nchini?
Na kama siyo tuna sababu gami ya kuliita BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA?
2.Hao TAHOSSA hawafuati criterias na miongozo ya utungaji na usahihishaji wa mitihani kutoka BARAZA au na wao wana za kwao?
Kwa vyombo vingine vinavyotunga mitihani hususani katika sekondari na vyuo/Ualimu,vinapofanya makosa NECTA haina mamlaka ya kuviwajibisha?
Mimi kwa upande wangu,sijui kwa MAWIO;
Natanabaisha kwamba;
BARAZA linahusika kwa namna moja kudumaza elimu kwasababu baada ya kufanya measurement & evaluation wanatakiwa watoe mkazo katika maoni yao ambayo yataonesha dira ni vitu gani vinahitaji kufanyiwa kazi ili kuipa uhai rlimu yetu iliyoko I.C.U
4.BARAZA linahusika kuzalisha walimu wasio na sifa.
Walimu wengi katika shule zetu Tanzania wamepita katika vyuo vya Ualimu i.e.GRADE A,STASHAHADA achilia mbali kwa hawa wachache wa zama hizi wanaoganga njaa kutoka vyuo vikuu mbalimbali.
Wengi kati ya walimu halisi i.e.(grade A's & Diploma) wamefaulu mitihani ya baraza huku wakiwa ni Vilaza wa kuogofya.Sasa sijajua NECTA inapima na kuevaluate kitu gani kutoka kwa mtahiniwa.
5.Kwa baraza kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani ni wajibu wao,
kuweka walimu wenye sifa na vigezo vinavyostahili kusahihisha mitihani ni jukumu lao.
Sote tumekuwa ni mashahidi kwa walimu wanaokwenda kusahihisha mitihani ya Taifa miaka ya hivi karibuni ya kwamba uwezo wao wa kufundisha ni mdogo kiasi cha kukatisha tamaa.
Je? atawezaje kusahihisha mtihani ambao hata yeye mwenyewe akipewa aufanye hauwezi !!!
sasa ni nani wa kulaumiwa hapa kama soyo baraza?
Dr.Ndalichako hakuwa na sababu ya kuonesha picha za Zombie!
ningefarijika kama angetoa ushauri kwamba kauna sababu ya kuingiza kwenye mitaala ya sekondari somo la sanaa ya uchoraji na taaluma yake.
Naunga mkono 100% WAANDISHI WENGI WAPO KUGANGA NJAA TU,lakini kwa hili la MAWIO, tusiwahukumu kwa dhaifu moja na kusahau mazuri lukuki.NAWAPONGEZA SANA.
Ninachoweza kusema measurement & evaluation wanayoifanya NECTA ni ya kinadharia zaidi ambayo haina ufanisi wowote,
HIVYO NDALICHAKO ANAHUSIKA KWA NAMNA ZOTE. asante
ww n gerad handoo nn? Ila co mbaya n mawazo yako, nayaheshimu
Dah!. Mkuu umenena vema sana.
chatts55Measurement & evaluation wanayoifanya NECTA ni ya kinadharia zaidi ambayo haina ufanisi wowote.
Je,unauhakika hiyo ni kazi ya NECTA?
Mimi nafikiri Meas. & Evalu. inakuwa ya nadharia kwa sababu ya Mazingira ya kazi ya kufundishia na bila kusahau mgogoro kati ya walimu na serikali kuhusu maslahi ujira wao.
Hess Hapo no. 6 nakumbuka siku moja by chance nilisikia mhe. mmoja kwenye radio Imani alikuwa anasema..wanahusika na Islamic Knowledge kule Baraza hawana weledi wa kutosha..yaani wameokotwa tuu kutoka mtaani na hawana upeo wa kutosha kwenye Dini. Aligusia pia suala la usahihishaji wa mtihani wa I/Know akasema wanafunzi wanakoseshwa kwa sababu hao wanaowawakilisha hawana upeo wa kutosha..alitoa mf. Dini ya kiislamu ina nguzo ngapi?
Watu wengi hawajumu ya MoVET na NECTA. Ni vema Wizara ya Elimu ikafanya jitihada za kueleimisha umma.
akasema wanafunzi wanakoseshwa kwa sababu hao wanaowawakilisha hawana upeo wa kutosha..alitoa mf. Dini ya kiislamu ina nguzo ngapi?
kumbe NECTA wanaokota watu wasio na ujuzi na taaluma husika! na bado mnasema dr.NDALICHAKO hawajibiki
Ukifahamu mitihani ipo kwa ajili gani,utanisoma bila ya wasiwasi
Nashukuru kwa kuweka wazi majukumu ya NECTA. Kuna watu huwa wakiitisha makongamano yao, ajenda ya kuandamana kwenda kumng'oa Ndalichako kule NECTA huwa haikosekani, ukiuliza kwa nini, eti wanafunzi 'wao' wanafeli! Sasa shule zenu zenyewe ajira ya mwalimu inategemea imani yake, unategemea nini hapo? Joseph Selasini (Mb) aliwahi kuweka sawa maelezo, lakini wabunge 'wale' wakang'ang'ania kuwa sio Kawambwa, ni Ndalichako! ... kisa, Kawambwa ni 'mwenzetu'
Hivi hata hao akina Mh Saidi Mtanda wana upeo mdogo kiasi hicho wa kufikiri. Kwani NECTA iko wapi, hivi wanaposema lengo ni kuonesha kuwa tatizo ni NECTA ba siyo Wiara kwani NECA iko wapi? Kama mambo ya NECTA hayaendi vizuri ni nani anayepaswa kuwajibika kisiasa kama siyo waziri wa elimu?