Dr.Ndugulile angelitakiwa kuanza kazi leo

Dr.Ndugulile angelitakiwa kuanza kazi leo

Quimica

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2018
Posts
1,036
Reaction score
1,286
Moment of Silence katika Mkutano wa 156 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kumkumbuka Mkurugenzi Mkuu Mteule wa WHO AFRICA, Marehemu Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile.

Leo ni siku ya kihistoria, ambapo kama Dkt. Faustine angekuwa hai, angelipitishwa rasmi na kuanza majukumu yake kama Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kwa Ukanda wa Afrika (@WHOAFRO), jukumu ambalo lingemuweka kama kiongozi wa maendeleo ya afya kwa mamilioni ya watu barani Afrika.

Lakini kutokana na msiba huu mkubwa, Kamati ya WHO ilifanya Mkutano wa Dharura uliohusisha wawakilishi wa nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Mawaziri wa Afya kutoka mataifa yote ya Afrika. Katika mkutano huo, ilikubalika kuwa Mataifa ya Afrika yatapendekeza tena wagombea kwa nafasi hii muhimu. Siku ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 28 Februari, 2025.

Soma:
Kamati hiyo itapitia na kutoa nafasi kwa wagombea watakaopitishwa kujinadi mbele ya jopo la majaji tarehe 2 Aprili, 2025 (Political Forum), ambapo watapata fursa ya kuonyesha uwezo wao katika uongozi wa afya duniani.

Dkt. Tedros @DrTedros, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, ataitisha Mkutano wa Pili (Second Special Session) tarehe 8 Mei, 2025, ili kuongoza mchakato wa kura kwa ajili ya kuteua Mkurugenzi mpya wa Ukanda wa Afrika.

Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Afya wa Dunia (World Health Assembly), utakaofanyika tarehe 15-27 Mei, 2025 huko Geneva, Uswisi, ambapo masuala ya afya duniani yatajadiliwa na kutolewa maamuzi muhimu.

Hatimaye, katika mkutano wa 157 wa WHO, utakaofanyika Agosti 2025, jina la Mkurugenzi Mkuu mpya wa Ukanda wa Afrika litatangazwa na kupitishwa rasmi!

Tunaendelea kumuenzi Dkt. Faustine kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya Afrika na duniani kwa ujumla.

Kila la kheri kwa Tanzania !
 

Attachments

  • Screen_Recording_20250204_190744_X.mp4
    10.8 MB
  • images-68.jpeg
    images-68.jpeg
    29.9 KB · Views: 2
Jamani maisha ni fumbo familia yake ilikuwa imefurahi nasi pia kwa kuwa angeenda kutuwakilisha ila muda haukuwa mikononi mwake.Alale mahala pema peponi Amen
 
Back
Top Bottom