Matokeo ya Urais: DK. Magufuli atangazwa mshindi
kwa asilimia 58.46
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
( NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, leo jioni
amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa
Tanzania wa mwaka 2015 kuwa ni Ndugu John
Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yametangazwa leo
ambapo mwenyekiti huyo amemtangaza Dk.
Magufuli kama rais wa Serikali ya awamu ya tano
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Dar es
Salaam.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji
Mstaafu, Lubuva alisema kwa mujibu wa Ibara ya
41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais
atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo
tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine
yeyote.
Aidha Lubuva, amesema kwa mujibu wa ibara ya
47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais
akichaguliwa basi na mgombea mwenza wake
atakuwa Makamu wa Rais.
?Kwa kuwa Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli
wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea
yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na
kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B
vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343,
ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais
wa 2015.
?Mheshimiwa Mheshimiwa John Pombe
amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu
amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,? alikaririwa na
FikraPevu mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura
waliojiandikisha ni 23, 161, 440, waliopiga kura ni
15, 589, 639 sawa na asilimia 67.31 ya wapiga
kura wote waliojiandikisha.
Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni kura halali 15,
193, 862 sawa 97.46% kura zilizokataliwa 402, 248
sawa 2.58% hivyo Magufuli amepata kura ambazo
ni 8, 882, 935 sawa na 58.46% ya kura zote halali.
Matokeo ya wagombea wengine akiwemo, Anna
Mghwira wa (ACT-Wazalendo) 98,763 sawa 0.65%,
Chifu Lutalosa Yemba (ADC), 66, 049 sawa na
0.435 huku Edward Lowassa (Chadema) akimfuatia
kwa kura Dk. Magufuli kwa kupata kura 6, 772,
848, sawa 39.97% na Hashim Rungwe wa
(CHAUMMA) aliyepata kura 49, 256, sawa na
0.32%.
Wagombea akiwemo Janken Kasambala (NRA) 8,
028 sawa 0.03% na Maximilian Lyimo (TLP) 8, 198
sawa na 0.05% Fahmy Dovutwa (UPDP), 7, 785
sawa 0.05%.
Hata hivyo, Vyama 6 vimesaini matokeo ya urais
ambapo wagombea wawili wa vyama vya CHADEMA
na CHAUMMA, hawajasini karatasi ya matokeo ya
nafasi hiyo ya urais.
Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani
amesema majimbo 6 hayajafanya uchaguzi na
sababu mbalimbali ikiwemo vifo, wakati majimbo 5
hayajafanya uchaguzi kutokana na mapungufu
mbalimbali.