Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Amen. Sifa,heshima na shukrani anastahili MUNGU wetu.Tumkumbushe rais wetu mteule asisahau ahadi sake kwa MUNGU na watanzania wote. Amtangulize MUNGU,awatumikie watanzania,auepuke uovu na anapokosea aombe toba nchi yetu izidi kubarikiwa. Asilipize visasi,maana visasi ni vya BWANA.

Kuwa Rais wa Tanzania raha sana Yaani watu wanakuamini Ingawa wao wenyewe hawaamini hicho wanachosema
 
Mungu awabariki sana, wote mlio shiriki katika kampeni ya Dkt John Magufuli

Kwanza napenda kusema Hongera sana Mtanzania.

Kwa Niaba Ya Rais wetu Mpya Naomba kuwashukuru vijana wote waliopambana kwa niaba ya CCM na Mgombea wetu Mpaka kufikia hatua hii.

Pia naomba kutoa shukrani za dhati kwa wale wote mliokuwa mkiwaelimisha vijana juu ya kujiepusha na fujo, matusi, na kejeli mitandaoni, naamini sasa wamejifunza.
Sisi sote ni waTanzania, Rais wetu ni Mmoja, na tunakiri kuwa Upinzani umekua japo demokrasia imeamua.
#HapaKaziTu
12193336_156436654708970_6785152856121518457_n.jpg


Mungu Ibariki Tanzania
Sio demokrasia dola imeamua.
 
natangaza kuanazia leo sitapiga tena kura ndani ya hii nchi na ccm mutawale milele
 
Acha waisome namba eeeeh! CCM MBELE KWA MBELEEEEEE, Heko Mh. Rais wa JMT J.P. Magufuli, hakika kura yangu haikwenda bure, wapi ibra87 hebu kujeni tusherehekeee.
Hapa nilipo sauti imekauka harafu sitamani hata kulala Leo. Uko wapi ni mtume dereva aje akuchukue?
 
Last edited by a moderator:
Hapa nilipo sauti imekauka harafu sitamani hata kulala Leo. Uko wapi ni mtume dereva aje akuchukue?

Mie nasherehekea nikiwa kitandani naumwa, ila nimefurahi sana aisee, sasa ni kazi tu.
 
Jomo Kenyatta aliwahi kusema kuwa "Mimi ninaongoza wagonjwa mahututi ila yapo mategemeo kuwa watakuja kuzinduka siku moja, huyu Julius Nyerere anaongoza maiti! Hawa hawatokaa wazinduke kamwe"
 
Viwanda vitaanza kujengwa January hakutakuwa NA machinga tenants nchi hi
 
Amani ya Mungu iwe nawe raisi wangu mteule mpendwa,

Kwanza napenda kukupongeza kwa moyo wangu mmoja kwa sababu wewe ndo naamini ni mtu unayeifaa Tanzania. Niliwai kuandika humu kwenye thread zilizotangulia kuwa Tanzania inayosumbuliwa na kiwango kikubwa cha wananchi wasiopenda kufanya kazi, wapenda dili na wizi, wapenda maneno matupu na wasiopenda kufanya kazi kwa ufasaha inaitaji mtu mkali ambaye niliwai kusema dikteta mzalendo. Tangu uchukuaji wa fomu CCM ulipoanza mie niliwaunga mkono wewe na Prof Muhongo kwa sababu niliamini nyie ndo watu mnaokidhi hiki kigezo cha dikteta mzalendo ambaye atakuwa mkali na kuwageuza wananchi kuwa wafanya kazi na sio wapenda vya bure, ambae atasababisha utumishi wa umma kuwa utumishi kweli na si vinginevyo.

Kwa wewe kuchaguliwa na watanzania kusema kweli Nimemshukuru Mungu na nasema jina la bwana lihimidiwe.
Nikiwa nakufananisha sana na watu kama Paol Kagame, Meles Zenawi(marehemu waziri mkuu wa ethiopia ambaye hadi duia imemuheshimu kwa jinsi alivyoitransform Ethiopia kiuchumi) naamini kwa moyo mmoja kuwa sasa Tanzania ipo kwenye mikono salama na stahiki.

Raisi wangu mteule umeona mwenyewe mgsawanyiko wa kura ulizopata ulivo, umeona maeneo yaliyokupigia kura kwa wingi na kuna watu wamekuwa wanakebehi eti umepigiwa kura na masikini na watu wasio na maendeleo ivyo basi nakuomba kwa uongozi wako ufanye yafuatayo.

1. Kwanza ufanye reshuffle kubwa sana serikalini hasa kwa wale watu ambao obvious una uhakika watakuangusha. Najua washauri wako watakuelezea vizuri katika hili. Hii ni kwa sababu kuna watu waliside kabisa na upande mwingine na hawakutaka wewqe uingie sasa kwa usalama wa serikali yako naomba uanze na hii reshuffle ya hawa watu.

2. Pamoja na jitihada zako za kubana matumizi ya serikali naomba kweli uyabane muheshimiwa na uwe na target kabisa ya kusave kiasi fulani cha fedha ambacho utakielekeza sehemu fulani.

3. Kwenye kuboresha mishahara ya wafanyakazio naomba uanze na waalimu na madaktari kwa sababu haya ndo makundi yanayokutana na watu wa hali ya chini karibu siku zote za maisha ya wananchi wa nchi yako, waalimu wakiwa na maslahi mazuri obvious hawatawalisha sumu na matango wanafunzi kuichukia serikali, pia watafundisha kwa morali hadi wazazi wao watafurahi na kuipenda serikali yako. Pia madaktari nao watafanyas kazi kwa hali na watatoa huduma nzuri na wananchi watafurahia na kuisupport serikali yako.

3. Naomba uwekeze zaidi kwenye miradi ya maji na umeme kwa sababu hivi ni vilio vikubwa sana vinavochangia watu kuichukia serikali. wekeza kwenye mega projects za maji na umeme ambazo zitaelekezwa kwenye maeneo yenye watu wengi. Hili litakubeba sana.

4. Naomba kwenye ahadi zako priority hasa kwenye hospitali,madawa na mikopo uanze kwa maeneo ambayo yanasemwa kuwa watapata shida pamoja na kukupigia kura nyingi. Nasisitiza kwenye hili kwa sababu asikwambie mtu raisi wangu hawa watu walikuchagua kwa sababu waliamini katika wewe na ili wasiwe na moyo uliosinyaa naomba kwenye miradi yako utekelezaji wake uanzie kwenye mikoa hii ili wakisemwa vibaya waseme tulimchagua na hatujajuta kumchagua. Then ukitoka huko ndo uende na kwingine kule ambapo walikupa kura chache na hawakuiamini CCM.

5. Naomba uboreshe na urekebishe utendaji serikalini hasa masikini na mtu wa kawaida aone kuwa kweli utendaji,uwajibikaji na huduma za serikali zimebadirika. Usilee wazembe,walarushwa na waonevu bali wape nafasi wachapa kazi.

6. Tilia maanani sana mfumo wa ukasanyaji kodi na uhakikishe mamlaka ya kodi inakuwa na watumishi wenye weredi na maadili na ambao hawaendekezi rushwa. Hapa kuwa mkali sana ikiwezekana kuunda mfumo wa kufuatilia mali na fedha za wafanyakazi wa mamlaka ya kodi kwa sababu kusema kweli hili ni sehemu mabayo imekuwa ikiirudisha sana nchi yetu.

Raisi wangu mteule haya ni mambo 6 niliyokuandikia na naomba uyatilie maanani sana na nakuamini kwa uwezo wako huwezi kushindwa.

MUNGU AKUBARIKI RAISI WANGU NA AKUPE UJASIRI, NGUVU, HEKIMA NA UTHUBUTU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Naungana nawe kumtakia kheri na mafanikio ktk kuliongoza Taifa letu. Amen
 
Nani amchaguwe lowassa mwizi yule. Hongera john pombe magufuli.
 
Kufikiria tu eti Lowassa anaweza kuwa rais JMT ni UWENDAWAZIMU USIO NA KIFANI
 
Back
Top Bottom