- Jasusi njakusiwa mwamba, kumbuka kuwa huwezi kuwa a good politician bila ya kuwa na kaunafiki japo kadogo, Salim alipopigwa chini na Urais aliapa kwamba hatajihusisha tena na siasa, au CCM alijifungia ndani kama siku nne akilia na kwamba hatajihusiha tena na Muungwana na Mkapa, infact alikuwa kwenye matayarisho ya kwenda kukutana na waaandishi wa habari Courtyard Hotel ili kuwachafua Mtandao na Mkapa, akawahiwa na Malecela akaacha na leo yeye na hao wote aliojiapiza nao ni damu damu! ndio politics!
- Lakini kwa maoni yangu ni kwamba wale wote walioko kwenye marathon ya Urais one thing they want ni Salim kuwemo kwenye kinyang'anyiro cha Muungano, ndio maana baadhi ya hawa vigogo wanaotayarisha huu mpango wa yeye na Visiwani ni kutoka Mtandao ingawa so far wanapata taabu sana kuiuza hii idea kwa CCM-Asilia, ambao wangependa kuona Salim anagombea kwenye Union level.
- Karume recently ameibuka na kuwa a strong player wa maamuzi muhimu ya taifa na muungano, ni kutokana na kuwa na a strong team kule Visiwani na kusikiliza sana mashauri ya Shein on how to play na sisi wabara. Kule ana kikundi kidogo lakini chenye very intelligent people ambao wameshituka sana na ule mchezo wa kwenda kichwa kichwa na wanasiasa wa bara na huu mshikamano wao ulianzia Butiama, ambapo kwa mara ya kwanza waligundua kwamba Muungwana ni weak!
- Salim has nothing to lose sasa hivi kwa kuanza na Urais wa Visiwani, infact itampa nafasi ya kujisafisha na lawama nyingi sana ambazo amekua akirushiwa kwamba hana record ya uongozi na kwamba alikuwa akibebwa na Mwalimu, akiweza kuji-establish kule na kufanya tofauti na bara, basi bara tutamlilia mara moja kwamba ana-belong kwetu sio kule atajitengenezea njia nzuri sana ya kurudi Bara na kuwa Rais wa Muungano. Salim atashinda urais kule tena kwa kishindo kikubwa sana kwa sababu yeye na CUF wanachukua hela zao kwa tajiri mmoja huko Oman, sasa CUF na Seif hawawezi kuleta kivuli kwa Salim, no way! Na hata kama asipoweza kuwa rais wa Muungano, kwa kuwa Rais wa Visiwani Salim atapata nafasi ya kuwarudi Mtandao bara kiuongozi ambao hawana sera zaidi ya wizi tu wa hela za wananchi, kwa hiyo Salim has everything to gain kwa kuwa Rais wa Visiwani now!
- Tatizo lake kule litakuwa ni Shamuhuna, Hussein na Dr. Bilali, ambao Muungwana anaweza kuwapumzisha pembeni bila ya tatizo na kumnyooshea njia ya urais!
Respect.
FMeS!