TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Donyongijape

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2010
Posts
1,497
Reaction score
814
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.

"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.

"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza.

Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.

CHADEMA WATOA RAMBIRAMBI
 
Hii ni habari ya huzuni kwelikweli. Nimepata mshtuko mkubwa na dimbwi la huzuni kupata taarifa ya kufariki leo hii kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwanasheria Mahiri na Kiongozi wa NCCR-MAGEUZI Dr. Sengondo Mvungi. Nilipata nafasi na heshima ya pekee kushirikiana naye wakati wa sakata la Wanafunzi 29 wa Kitanzania waliotelekezwa na serikali ya Tanzania huko Ukraine. Dr. Mvungi alikuwa mstari wa mbele kujitokeza wazi pasi ya kujali jina lake na nafasi yake kuwasemea vijana wale na kutoa mchango wake kwa hali na mali katika kuwasaidia vijana wale. NI wakati huo ndipo nilipotambua kujitoa kwake katika kupigania mabadiliko ya kweli ya kisiasa nchini.

Familia yake imepata pigo kubwa leo na taifa vile vile. Natumia nafasi hii kutoa pole za dhati kwa familia yake, ndugu na jamaa pamoja na chama chake ambacho kimempoteza mmoja wa viongozi wake mahiri. Nawaombe wote faraja wakati huu wa majonzi makubwa na Mwenyezi Mungu amhurumie ndugu yetu na kumpa pumziko la milele. Amina.
 
RIP Dr. Mvungi. Mungu akulaze mahala pema peponi. Japo umeondoka kivuli chako kitaishi. Aliyekuondoa atakufuata soon japokuwa hatakuona. Naipa pole familia yako. Maisha yetu kwa sasa nchini ni kudra za Mwenyezi Mungu. Ni kwamba tupigwe, wengine wamepona lakini wewe umeondoka. Hao wezi watapotea kama wapigaji wa wengine walivyo potea. Pole sana.
 
Kama hii ni fact. RIP mtu mzima muvungi, tutakuombea daima
 
Too sad.. RIP Dr. Mvungi. Tutakukumbuka kwa harakati za kuwataka watanzania kuwa huru zaidi katika nchi yao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…