Rafiki yangu Kanda2 unanifurahisha, nakuja June kama upo TZ natamani nikuone MAANA wewe unasifa zote za kuwa mpiganaji wa kweli.
Ila sikuweka undergraduate kwa sababu za msingi maana ulizungumzia MBA. Lakini pitia vizuri website utaona.
Pia nadhani hauifahamu vizuri system ya higher learning ya UK, kwa hiyo hata nikieleza hutanielewa KIMSINGI iko tofauti na TZ. Kuna level zipo (Ukiwaona NACTE watakufafanulia) Kimsingi pale first year wanakuwa awarded Diploma na Advanced Diploma ambayo ni level 3, then mwaka wa pili ni wanatop up digrii, ila nilazima uwe na UK Qualifications.
Miaka miwili digrii ni normal sana, ILA LAZIMA UWE NA UK Qualifications. Kawaone NACTE watakufafanulia vema hizo level maana wao wanazo.
Halafu vyeti vyao vinatoka University of Wales, Institute Cardif na University of East London as awarding Board.
Pale ni kweli panawanafunzi wengi mpaka huwa wanakataa kurecruit, ila wana Compus tatu kwa hapo London.
Ni miongoni mwa vyuo vinavyokubalika hata home office (Walishapongezwa kwa umakini)
Wahadhiri wanao ambao ni very respected kama umesoma Marketing nadhani umekutana na Profesa Geoff Lancaster huyo ni baadhi tu ya walimu.
Pia fahamu waingereza ni wavivu na hawapendi kusoma hilo hata Brown aliwaeleza walipokuwa wanaandamana wakipinga nafasi nyingi kushikwa na wageni.
Kama hauko UK, ni vema ukafanya utafiti kwa kuwasiliana na BAC (British Accreditation Council for Independent Further and Higher Education).
Hatushindani tunaelimishana.hakuna traditional university yeyote kati ya zile nilizotaja including Oxford na Cambridge zinazotoa kozi au zenye intake kwa undergraduate zaidi ya moja kwa mwaka ukinithibitishia hilo nitakubali kuwa DR.Shayo ni bingwa wa uchumi na si mazingira.
unasema system ya Tanzania na UK ni tofauti sio kweli.elimu yetu ni ya UK,bunge letu,sheria zetu wao ni jumuiya ya madola na sisi ni wanachama wao.labda uwambie watu wanaotoka china,japan au Iran kwao ndio system tofauti.
mimi napenda kuwaambia watanzania tuwe wadadisi na wenye kutafiti kwenye kwenda kwenye vyuo hasa kama hiki.
Mzovya mimi najitahidi kufuatilia mambo haya ya elimu ingawa elimu yangu ni darasa la saba lakini duniani ya sasa ni kijiji mitandao inatupa uhalisia hata kama hatuko ulaya.
ukisoma gazeti la The Guardian la UK la tarehe 11,may 2009 wameorodhesha vyuo vikuu vya UK na chuo cha DR.Shayo kimeshika nafasi ya pili kwa umwisho.
wakati Times walikiweka cha mwisho kuonesha kuwa magazeti haya hayajiandikii tu ila yana wataalaam wanaofanya tafiti hizi.
Watanzania jaribuni kupitia website ya chuo cha LONDON SCHOOL OF COMMERCE www,lsclondon.co.uk kwenye website tu utajua kuwa chuo hiki kina mushkeli.wana kozi tatu za masters MCS TOURISM AND MANAGEMENT,MSC MANAGEMENT AND HOSPITALITY NA MBA GENERAL.na tunaambiwa kuna wanafunzi elfu nne.kozi hizo zinamfaa mtanzania gani? labda watu wa Tanapa na bodi ya utalii Tanzania,
rafiki yangu kasema chuo hiki kina wanafunzi hadi kinawakataa, kama ndivyo kwanini wamepunguza Ada? kwani price strategy ya marketing unapunguza ada ili upate wanafunzi wengi au mauzo makubwa au wateja wengi,hawa wamepunguza kutoka elfu sita na mia tisa hadi £3950. watu hawa wanaokataa wanafunzi wameweka Tangazo lao michuzi blog na wanalipia, wakisisitiza kuwahi kujisali kabla ya mwisho wa offer-(sale).hili linathibitisha kuwa chuo hiki hakina soko na watanzania ndio eneo lao pekee la kuwachukulia pesa zao kwani tumekuwa wazito kwenye kufanya utafiti au tunaingia mambo kichwa kichwa.
tujihadhari inawezekana kabisa hii ni sampuli nyingine ya DECI unajua unapata kumbe unapatikana.
kama Ada pounds elfu tatu bora mtu uende India au Malaysia au Uganda ukasome kwenye chuo chenye hadhi ya chuo sio usome NEW DELHI lakini cheti na chuo chenyewe kiko Bombay.
kwanini umefunga safari hadi huko na usifike kwenye chuo chenyewe? kwani ukienda London school of commerce hutakutana na wenye nchi au walimu bora na facility hakuna, kama ni cheti cha bei ndogo soma DISTANCE LEARNING ukijua mateals na cheti kinatoka kwenyewe kuliko kwa third party.
hivi umesoma London school of Commerce umeenda kuomba kazi na anatakiwa referee ambaye ni mwalimu wako utatoa reffence Cardiff au hapo London school of commerce?
kwani lecturer wa Cardiff hafundishi LSC huko yuko Mhindi Mr.Patel.mfano timu yangu ya Yanga imekusajili lakini hujacheza mazoezi na Yanga hapa kaunda hata siku moja na wala kocha KOndic hajawahi kukuona jee wewe unafaidika na unatumia facility za Yanga?
Umesema niwaone NACTE unakusudia NECTA ambao wanahusika na elimu ya O level na A level sio elimu ya juu kama hizo Diploma unazosema. au unakusudia Acrrediation council ya Tanzania? nayo sio kazi yake kuhakiki vyeti kazi zao kutizama ubora wa vyuo na elimu wanayotoa kwa vyuo vya ndani ya nchi na usajili wa vyuo.
umesema niwasiliane na British ACCREDIATION COUNCIL hawa si goverment body ni charity organisation na vyuo vikuu kama Leeds university huwezi kuona BAC wanajihususha nao. hawa wana deal na vi college vya mtaaani.
Umesema kuna professor wa Marketing hapo chuoni kwako lakini website ya chuo haisemi kuwa kuna huyo professor hivyo ni ngumu kwangu kuamini maneno hayo ni sawa na Yebo yebo aliyeandika kuwa dr.shayo ni associate professor bila ushahidi na nimembana hajarudi tena hadi leo kabaki kutoa Thanks tu alifikiri ataniburuza ameshindwa TA itaweza JF?
umesema kuwa Waingereza wavivu TUNAKUPA MFANO mikoa ambayo imeshikiliwa na wageni mfano wahindi kama BRADFORD,Birmingham,Leicester ambako umesema kuna rafiki yako aliomba ukitizama website za vyuo vyao wanaoshika na kufundisha ni wazungu www,bradford,ac.uk,
University of Leicester au
www.barmingham.ac.uk anachokisema Gordown Brown hata Majjid Mjengwa aliwahi kuandika hapa kwenye Rai ni kuwa namba ya waingereza ni ndogo wanaohitimu kuliko wachina na wahindi wanaomaliza kwa mwaka milioni 4 na 2 respectively.
kuna jamaa yangu alikuja huko huko kusoma chuo cha mtaani kozi ya Acca chuo cha London school of Accounting and Management-LONDONSAM ukitizama website ya chuo hiki hata kama cha mtaani lakini kina watalaam kwa kiasi fulani ingawa naamini watakuwa on part time basis cheki website yao..
wengine ni London school of Accountancy,Kaplan zamani Emil wolf au BPP ni vyuo vyenye hadhi kuliko LSC kwani college hizi kama tuition providers kwa professional courses kama ACCA,CIMA,CFA n.k lakini school of commerce hata professional courses hawana kama hizo.
umegusia sana AWARDING BODIES najua wazi kozi kama ya diploma na Advance diploma ya business inatoka IAM au institute of Administrative management halafu ndio mnampeleka mtu Cardiff au kwa kugha yako Top up.
Rafiki umesema kuwa kuna mtanzania ndio alileta hiyo discount sawa ni jambo zuri lakini ujuwe kuwa hapa tunazungumzia maisha ya watu.wazungu walipokuwa wanatawala makoloni au kutafuta watumwa walikuwa na watu wanawatumia kutoka same backgruond. tusipumbazwe na vidiscount vya wahindi na tukawaingiza mkenge ndugu zetu kwa kuwapeleka LSC KWENYE BURE GHALI AU DECI.
lengo la mjadala huu kuwafungua watanzania tuwe tunaumiza kidogo vichwa haswa kwenye maamuzi yanayogusa future zetu.
ndugu yangu amekuwa akikazia kila dakika na kukoza maneno KUWA HOME OFFICE wanakitambua chuo. HOME OFFICE hao hao mara ngapi wanatoa visa kwa wana bongo fleva jee wao ni watalaam wa bongo fleva?au wanawapa visa watu wakiamini ni genuine kumbe ni wauza madawa ya kulevya.HOME OFFICe hao hao wanadanganywa na wapemba ambao ni watanzania wanawambia ni wasomali hatimaye wana wapa pasipoti za Uingereza,nilisoma gazeti moja kuwa kuna wahamiaji haramu laki tano kama ni taasisi makini yasingekuwa hayo.
hujawahi kusikia wakuu wa Home office wamejiuzulu kwa maskendo? taasisi inayodanganywa na wapemba iko makini na kuipa mfano?wahindi waliotufundisha EPA watashindwa kuwazuga HOME OFFICE na college kama LSC?
The bottom line home office sio academicians wala hawajui taaluma ni nini?hivi mtu akisema Mzumbe kuna walimu feki jibu kuwa nenda mambo ya ndani kwani kuna wazungu walipewa visa kuja kutembelea chuo kikuu cha Mzumbe,Mambo ya ndani inahusika nini na taaluma?
NIMELAZIKA KUANDIKA sana ili watu wapate ujumbe naamini kuna ya msingi out of my pumba.niliowaboa mtanisamehe natanguliza uzalendo itakuwa aibu na ajabu mtu afunge safari kwenye kusoma kwa mzungu anakutana na MR.PATEL darasani.