Huu ni ukweli. Nimetafakari sana kuhusu hili na kugundua kitu muhimu sana. Nchi zinazofuata mfumo wa "Presidential" kama Marekani, Naibu Rais/Makamu ana nguvu sana. Tatizo letu ni kuwa tumechanganya Parliamentary system na presidential. Katika mfumo huu, Rais anakuwa mtendaji na ana nguvu sana lakini Makamu wake anakuwa ni symbolic na pengine yuko kama reserve ili kusiwe na power vacuum in case akisafiri, kuugua au vinginevyo. Waziri Mkuu anabaki kuwa mtu wa jikoni zaidi maana ni msimamizi wa kazi za kila siku za serikali na ni kama kiranja wa mawaziri wote. Kwa sababu hiyo naona siyo haki kusema kuwa JK anampendelea Mizengo at the expense of Shein. Ukweli ni kuwa ukimwondoa Sumaye ambaye alikuw ayes man zaidi, mawaziri Wakuu karibu wote waliopita walikuwa powerful. Ukianza na Sokoine, Salim, Waryoba, Malecela na hata Lowassa.