Dr Shein: Anabaguliwa?

Dr Shein: Anabaguliwa?

I think his talents are wasted on the political arena with a CV like that.
 
Inategemea Makamu wa Rais anakuwa na shughuli gani pindi zinapotokea events kama hizo. Kuna mambo muhimu ambayo Mh. Shein anatakiwa kufanya kuliko kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa baraza la mawaziri nchi jirani. Ni mikutano mingapi ya Kimataifa ambayo Shein ameudhuria ambayo inaendana na ngazi yake!! Acheni mambo ya udaku. Si kila habari inayoandikwa kwenye gazeti Bongo JF inatakiwa kuisadiki. Kama itakuwa hivyo basi hata habari za magazeti ya mafisadi Rai, Tazama, Mtanzania na mengineyo kila leo yangekuwa yanajadiliwa hapa. Mie nafikiri hilo gazeti lililoandika hiyo habari linaweza likawa na MOJA YAKE KICHWANI.

Dr Shein kama Dr Shein hana tatizo lolote. Tatizo lipo kwenye nafasi yenyewe ya Umakamu wa Rais. Kama mnakumbuka CCM wenyewe walichukua muda mrefu kuweka sawa namna Makamu wa Rais atakavyopatikana. Alikuwa ni Mwalimu ndiye aliwachimba 'mkwara' mzito ndipo wakaamua haraka haraka namna ya kumpata Makamu wa Rais. Mpaka leo Wazanzibari wengi hawaridhiki na namna Makamu wa Rais anavyopatikana. Wao walitaka Makamu wa Rais awe ni Rais wa Zanzibar.

CCM waliogopa hilo la Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais ukichukulia na upinzani mkali iliouonyesha CAF kabla ya uchaguzi wa 95. Kama Seif angeshinda Urais wa Zanzibar na kuwa Rais ni wazi angekuwa Makamu wa Rais (kama wazanzibari watakavyo) hivyo basi angekuwa ni Makamu wa Rais (kutoka upinzani) akiongozwa na Rais kutoka CCM. Hilo liliwaogopesha sana CCM na mwalimu alipokuja juu ndipo 'wakarukia' kuweka Makamu wa Rais kama mgombea mwenza bila kuainisha vizuri kazi zake! Anachokifanya Shein ni kile kile alichokuwa akikifanya Marehemu Omar Juma!

Shein kama Shein ni mchapa kazi. Kwenye serikali kama hii JK inayoongiozwa na 'mazomozi' unategemea Shein afanye nini zaidi ya kukaa kimya na kusubiri mshahara wake! Hata mimi ningekuwa yeye ningefanya hivyo hivyo. Huyu Shein ndiye Waziri pekee aliyeingia kwenye serikali ya Karume kutoka serikali ya Salmini mwanzoni ukiachilia akina Shamhuna waliokuja juzi juzi. Inasemekana Shein alikuwa ndiye (Naibu) Waziri pekee alioyeonyesha msimamo wa kumuunga mkono Amani tangu wakiwa katika Serikali ya Salmini.

Shein huyu huyu aliongoza Nchi vizuri tu wakati Mkapa akipata matibabu huko Uswisi ikiwa ni pamoja na kutengua maamuzi ya Prof Mwandosya ya kumuachisha kazi Kanali Nalingigwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume ya Mawasiliano.

MWACHENI SHEIN WA WATU!
 
aw,aachwe aendelee kula mshahara bila kazi kwa sababu ana sifa ya kiongozi bora. Anyways, kila la heri mheshimiwa vice president.
 
aw,aachwe aendelee kula mshahara bila kazi kwa sababu ana sifa kiongozi bora. Anyways, kila la heri mheshimiwa vice president.

Mama si umeshaambiwa anafanya kazi. Wanamwita Mzee wa Mikasi (Ya kukata utepe lakini siyo ile mingine) Kwa watu walio karibu na Dk Shein wanasema ni mchapa kazi ila ni mtu asiyependa 'misifa'. Inawezekana kabisa JK hakupenda Shein awe Mgombea Mwenza na inawezekana kabisa System ya JK ilim-neglect Dk Shein siku za nyuma. We mwenyewe si uliona akina EL walivyokuwa wakitafuta umaarufu kwa kujipa 'urais mtarajiwa' Sasa Dk Shein angefanya nini? Tangu Lowassa aondoke madarakani JK amekuwa karibu sana na Shein kuanzia kwenye uteuzi wa Waziri Mkuu. Kumbuka Shein alikuwa Tanga na ikabidi aahirishe ziara ile. Ilivyo ni kwamba Shein anaweza naye akaanza kutafuta nguvu za kisiasa unategemea JK atamfanya nini AU watu wanataka tuje tushuhudie yale ya Rawlings wa Ghana na Makamu wake ya kutwangana ngumi hadharani? Kwenye nchi kama yetu ambayo ndiyo kwanza tuko darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi ya Demokrasia tunawahitaji watu kama Dk Shein. Angalia kule Rwanda ambako Rais alikuwa Pastor Bizimungu na Makamu wake Paul Kagame. Bizimungu alipotaka kutumia nguvu zake za Urais, Kagame akamuundia zengwe yuko wapi leo zaidi ya kuishia 'Lupango' anakooza na Kagame kampa masharti kwamba akitaka kutoka huko 'aape' kwamba hatajihusisha na Siasa! Angalia 'gomvi' la Thabo Mbeki na Makamu wake Rais Jacob Zumah! Shein angekuwa na uchu wa madaraka angeweza kujitengeneza akawa Zumah wa Bongo.

Kwa vurugu hizi za Wazenj kuhusu Muungano, tunawahitaji watu kama kina Shein na yule mtangulizi wake Omar Juma wenye siasa za mlengo wa kati. Kumbuka Salmini alivyoanza chokochoko ya kutaka kurudi madarakani, yule Marehemu alikuwa ni mtu wa kwanza kwa viongozi wa kitaifa 'kumrushia' makombora Komandoo na lile lilirahisisha kazi Ben kumtolea nje!
 
Ahhhh.., sielewi wala sioni huo uchapa kazi wake!

Yaani kwa jinsi mambo yanavyo kwenda kombo yeye anamsaidiaje JK? sidhani kama kukaa kwake kimya ni busara hata kidogo, tena huyu ni muoga ambaye hafai kabisa kuwa kiongozi! Yuko wapi katika kukemea woga wa mwenzake wa kuto taka kugusa mafisadi, kama yeye ni mtu safi amsaidie mwenzie ama apaaze sauti yake, 'he is not a baby by the way', kwanini asiseme? Tuache kumpaka viungo vya pilau kukubali kwake kugeuka boya manake hafai kuwa kiongozi period!
 
Ahhhh.., sielewi wala sioni huo uchapa kazi wake!

Yaani kwa jinsi mambo yanavyo kwenda kombo yeye anamsaidiaje JK? sidhani kama kukaa kwake kimya ni busara hata kidogo, tena huyu ni muoga ambaye hafai kabisa kuwa kiongozi! Yuko wapi katika kukemea woga wa mwenzake wa kuto taka kugusa mafisadi, kama yeye ni mtu safi amsaidie mwenzie ama apaaze sauti yake
, 'he is not a baby by the way', kwanini asiseme? Tuache kumpaka viungo vya pilau kukubali kwake kugeuka boya manake hafai kuwa kiongozi period!

...same applies to the entirely CCM CC, NEC, (most) MPs, Prime Minister, Permanent Secretaries, Tanzania Ambassadors, etc etc
 
Ukiangalia harakaharaka utaona Shein anatengwa Hata mimi nimewahi kufikiri hivyo.
lakini katiba inampa nafasi ya Waziri mkuu kufahamika zaidi kuliko makamu wa raisi.Inawezekana kweli JK hampi nafasi sana shein but bado nafasi yake kama makamu wa raisi ipo pale pale.Kama tukienda juujuu unaweza kuuliza kwa nini Rice anaonekana ana nguvu kuliko makamu wa raisi.Ni mambo ya kiutendaji tuu haya ingawa anaonekana ceremonial!Who knowa kama haziivi na mkuu wa kaya?
 
Ahhhh.., sielewi wala sioni huo uchapa kazi wake!

Yaani kwa jinsi mambo yanavyo kwenda kombo yeye anamsaidiaje JK? sidhani kama kukaa kwake kimya ni busara hata kidogo, tena huyu ni muoga ambaye hafai kabisa kuwa kiongozi! Yuko wapi katika kukemea woga wa mwenzake wa kuto taka kugusa mafisadi, kama yeye ni mtu safi amsaidie mwenzie ama apaaze sauti yake, 'he is not a baby by the way', kwanini asiseme? Tuache kumpaka viungo vya pilau kukubali kwake kugeuka boya manake hafai kuwa kiongozi period!

yawezekana anafuata sera yao ya kukosoana vikaoni na anavyoonekana probably amesema sasa ameona haisaidii ameamua kuacha mambo yaende kama yatakavyokwenda!
 
Ahhhh.., sielewi wala sioni huo uchapa kazi wake!

Yaani kwa jinsi mambo yanavyo kwenda kombo yeye anamsaidiaje JK? sidhani kama kukaa kwake kimya ni busara hata kidogo, tena huyu ni muoga ambaye hafai kabisa kuwa kiongozi! Yuko wapi katika kukemea woga wa mwenzake wa kuto taka kugusa mafisadi, kama yeye ni mtu safi amsaidie mwenzie ama apaaze sauti yake, 'he is not a baby by the way', kwanini asiseme? Tuache kumpaka viungo vya pilau kukubali kwake kugeuka boya manake hafai kuwa kiongozi period!
Naomba kuuliza kuchapa kazi ni kuonekana kwenye vyombo vya habari? Maana sisi tunategemea habari kuwa anachapa kazi kwa matukio ya nje(Ziara). Pia kuna kazi za ndani mfano muda mwing hapa JF tunahoji Mkuu wa kaya anasafiri sana, files, na documents nyingine anapitia nani ambazo Mkuu wa kaya angetakiwa kupitia?

Pia hamna mmoja wetu anayeingia kwenye vikao vya mawaziri na kujua kuwa yeye anakaa tu kimya kwa haagizi mawazi husika kushughulikia maswala kama ufisadi n.k.

Kwangu sina cha kuchangia kuhusu Dr shein maana sina full info za utendaji wake. Habari nazotegemea ni TV, magazeti etc.. Kule ofisini kwa ndani sijui nini anafanya.
 
..Ofisi ya Makamu wa Raisi ina wizara zipi na bajeti kiasi gani?

..moja ya njia za kuipa nguvu nafasi ya makamu wa Raisi ni kuongeza wizara zitakazokuwa chini ya usimamizi wake.
 
Naomba kuuliza kuchapa kazi ni kuonekana kwenye vyombo vya habari? Maana sisi tunategemea habari kuwa anachapa kazi kwa matukio ya nje(Ziara). Pia kuna kazi za ndani mfano muda mwing hapa JF tunahoji Mkuu wa kaya anasafiri sana, files, na documents nyingine anapitia nani ambazo Mkuu wa kaya angetakiwa kupitia?

Pia hamna mmoja wetu anayeingia kwenye vikao vya mawaziri na kujua kuwa yeye anakaa tu kimya kwa haagizi mawazi husika kushughulikia maswala kama ufisadi n.k.

Kwangu sina cha kuchangia kuhusu Dr shein maana sina full info za utendaji wake. Habari nazotegemea ni TV, magazeti etc.. Kule ofisini kwa ndani sijui nini anafanya.

kazi kweli kweli. Hata mimi niko puzzled kinamna.
 
Bwana Lazarosmtindi ina maana mtu anafikia nafasi ya Umakamu wa Rais akiwa hana wazo la Urais? Mimi nadhani urais anautaka. I know the man is extremely intelligent hasa katika eneo lake la specialisation. Unajua hii ya kusema Wapemba hawafai ni potofu na ndo maana wakamzushia Salim kuwa Hizibu. Salim angekuwa Rais baada ya nyerere lakini hiyo xenophobea ya Upemba ikamwangusha. But, trust me, I think there are very brilliant chaps in Pemba than in Unguja!
Ni kweli kabisa kuna wapemba wana akili mahodari wa kazi na biashara kuliko waunguja
 
Dr. Shein ndiyo mtu wa pili kwa madaraka katika Tanzania. Hata hivyo, majukumu yake yameanishwa kwenye Katiba vizuri tu:
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya
Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku
hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini
au yuko nje ya nchi.

Sasa, atakuwa amebaguliwa au anabaguliwa endapo Rais akiondoka basi haruhusiwi kufanya kazi za Rais; kwamba maamuzi yeyote ya serikali hapewi taarifa; kwamba akimuita waziri yeyote kupata taarifa waziri huyo anagoma na kusema "namsubiri Rais" n.k Kuna ushahidi wa jambo la namna hiyo?

Kwamba Rais hajawahi kumwagiza kufanya jambo lolote kwa niaba yake na anaamua kumruka na kumpa Waziri mwingine au Waziri Mkuu wakati Makamu yupo na hana jingine la kufanya, hapo atakuwa amebagugliwa

Kwamba anakatazwa kumsaidia Rais kufanya shughuli mbalimbali za siku kwa siku. Kwa maneno mengine Makamu anaweza kumuita na kumhoji au hata kufuatilia jambo lolote linalomuangukia Rais siku kwa siku. Endapo kuna ushahidi kuwa Shein amekataliwa kufanya hilo jukumu lake la Kikatiba hapo tutasema amebaguliwa!

Na Waziri Mkuu je anakaribiana na cheo au majukumu na yale ya Makamu wa Rais?

Katiba inasema hivi (pamoja na mabadiliko yake ya baadaye)
52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,
usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali
Bungeni.
(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu
atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au
mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

Angalia tofauti ya majukumu yake na yale ya Makamu wa Rais kuhusu shughuli za Muungano.

Na pia Katiba inaongeza majukumu yafuatayo:

53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Sasa utaona kuwa kwa mtindo huu Waziri Mkuu atakuwa anasikika zaidi na kuonekana zaidi kwa sababu yeye ndiye anasimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali kila siku. Makamu wa Rais yuko kwenye "background".
 
Kuna uwezekano rais hamu-assign kazi vice president au anamuassign kazi ya kusoma mafile ambayo sio lazima tuione directly.
 
haitaji kum-assign kwani nafasi yake ni ya Kikatiba, anaweza kufanya jambo lolote ambalo anajua anamsaidia Rais na kwenye mambo mengine Rais anaweza kumuagiza kitu fulani, lakini kila asubuhi hasubiri maelekezo kutoka kwa Rais.

Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa Rais aliamua kuweka wizara fulani chini ya VP, ile ya Mambo ya Muungano, Mazingira, n.k
 
Back
Top Bottom