Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Kilimanjaro Magharibi, ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la KICC, Dr. Glorious Shoo, amekemea vikali matukio ya karibuni ya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini, yakiwemo shambulio kwa Padre Dr. Charles Kitima na tukio la utekaji wa Mdude Nyangali.
Akizungumza na vyombo vya habari kama mwananchi wa kawaida, bila kuiwakilisha taasisi yoyote, Dr. Shoo amesema matukio hayo ni “kama kengele ya hatari”, siyo tu kwa viongozi wa dini bali kwa kila Mtanzania anayependa haki, utu na amani.
Sakata la kutekwa kwa Mdude unaweza kulisoma hapa Pre GE2025 - Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi
“Shambulio kwa Padre Kitima, tukio la Mdude, na matukio mengine yanayohusisha umwagaji damu ni jambo linalopaswa kukemewa vikali. Hatupaswi kuzoea utekaji kama jambo la kawaida,” amesema Dr. Shoo.
Soma Pia: Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
Askofu Shoo amesema kuwa taifa la Tanzania limejijengea heshima kubwa katika ukanda huu wa Afrika kwa kuwa taifa la amani, haki na maelewano, na hivyo haifai kuyumbishwa kwa matendo ya vitisho dhidi ya watu wanaosema au kusimamia haki.
Ametoa rai kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa matukio hayo yanachunguzwa kwa kina, wahusika wanakamatwa na hatua stahiki zinachukuliwa kwa mujibu wa sheria.