Issue sio kuwa Slaa mtu mdogo au la... issue ni kukubali matokeo au kutokubaliana nayo. Uchakachuaji uliofanywa haukubaliki hata kidogo, ndio maana hakuna sababu ya kwenda. Wewe unaona hakupunguzi kitu una tatizo, inadhihirisha kuna watu hawafurahii wizi unaofanywa. Hatuwezi kuhalalisha dhambi na dhuluma kwa kisingizio cha utaifa au amani. Utaletaje amani wakati wewe mwenyewe umeihatarisha kwa uchakachuaji? Kama Slaa asipoenda ataonekana ni mtu mwenye msimamo thabiti, kila mtu atakuwa anazungumzia hiyo issue, lazima kuna ujumbe mkubwa tuu unatakuwa umewasilishwa. Message itakuwa ,sent haiwezi kuwa kawaida hata kidogo!