Elections 2010 Dr. Slaa akishinda Urais, Kikwete apewe nafasi gani?

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
5,558
Reaction score
1,456
Jamaa kwa Jinsi upepo unavyovuma sasa hv katika Siasa za Tanzania, kutona na Kura za Maoni ndani ya JF pamoja na Kura za Maoni zinazoendeshwa na Gazeti la Serikali ya Kikwete ni wazi kwamba Dr. Wildroad Slaa atapata Ushindi mnono na Kuunda Serikali. Lakini vile vile CHADEMA siyo rahsisi kushinda Majority ya viti vya Bunge na hivyo kuilazimisha CHADEMA iunde Serikali ya Mseto

Je Wana JF mnavyomfahamu Dr. Wilbroad Slaa, Je Ataweza kumteua Jakaya Kikwete katika zile nafasi zake kumi za Upendeleo kisha akampa Uwaziri Mkuu?

Yaani

Rais. Dr . Slaa (CHADEMA)
PM Jakaya Kikwete ( CCM)

Mimi naona Amtose tu
 
Sidhani kama President Slaa atamhitaji JK kwenye cabinet yake. Hana sifa yoyote ya kumfanya awe waziri. Labda ampe u-DC au sanasana mkurugenzi wa sanaa na michezo ili ashughulikie vizuri promotion ya Bongo Flavor.
 
Haupo serious;

Hilo haliwezekana kwa sababu mbili;

1. Waziri Mkuu ni lazima AWE MBUNGE WA KUCHAGULIWA(sio kuteuliwa au viti maalumu)
2. Kikwete atakuwa ni RAIS wakati Dr Slaa atakuwa ni Katibu Mkuu wa Chadema.
 
JK mwenyewe hana uhakika na nafasi ya kushinda mpaka amewatahadharisha wanaCCM wenzake waachane na kauli kwamba CCM itatawala milele! Sasa wewe ujasiri huo unautoa wapi?
 
Ndio hapo utakapoonekana umuhimu wa kubali Katiba ya Jamhuri ya Muungano,Katiba yetu bado ina mapengo mengi,kiasi cha kusema ikitokea kushinda kwa chama kingine utaona mkanganyiko utakaotokea....Kelele ya kufanyiwa Mabadiliko Katiba ni lazima kwa sasa.
 
JK mwenyewe hana uhakika na nafasi ya kushinda mpaka amewatahadharisha wanaCCM wenzake waachane na kauli kwamba CCM itatawala milele! Sasa wewe ujasiri huo unautoa wapi?

Unauliza ujasiri anaupata wapi? Angalia ni lini kajiunga

Masonjo
user-online.png
Junior Member Join Date Sun Aug 2010
Posts 6
Thanks : 1
Thanked 0 Times in 0 Posts

Tunafahamu mtakuja kwa mamia kwa kulipwa ujira wa kudhalilishwa. Mtaondoka vichwa chini. This is JF.
 
Mnaanza kuhesabu vifaranga kabla kuku ajatotoa...!?
 
JK mwenyewe hana uhakika na nafasi ya kushinda mpaka amewatahadharisha wanaCCM wenzake waachane na kauli kwamba CCM itatawala milele! Sasa wewe ujasiri huo unautoa wapi?

Alichokisema Kikwete kinaitwa hekima.

Kikwete anajua na watanzania wote wenye mawazo yasiyo na ulevi wa upenzi wanajua kuwa Kikwete atashinda, kuingia kwa Dr Slaa kumeongeza msisimko wa sintafahamu ya nani atakamata nafasi ya pili.

CCM haitatawala milele, ila 2010-2015 bado haina kizuizi.
 
Nafasi ya Kikwete katika serikali ya Slaa? Kutembelea dunia nzima na kujitambulisha tena kuwa urais wake umekwisha.
 
Alichokisema Kikwete kinaitwa hekima.

Kikwete anajua na watanzania wote wenye mawazo yasiyo na ulevi wa upenzi wanajua kuwa Kikwete atashinda, kuingia kwa Dr Slaa kumeongeza msisimko wa sintafahamu ya nani atakamata nafasi ya pili.

CCM haitatawala milele, ila 2010-2015 bado haina kizuizi.

Mkuu hakuna guarantee kwenye siasa...Nani alijua mabadiliko makubwa ya siasa za Kenya mwaka ule 2002.Yale yaliyotokea Kenya yanaweza kutokea mahali popote.Watanzania wa leo (2010) wameamka na kila mtu anashiriki siasa.Rais Kikwete na Utawala wake wanalijua hili.Ngoja baada ya NEC ya 14/August (Mchujo wa Wagombea Ubunge) ndio utaungana na watanzania wengine kujua kuwa mabadiliko yanawezekana.Kumbuka wale akina Lipumba na Dr.Slaa si watu tofauti ni watanzania kama Mimi na Wewe,kwa maana hiyo tusiwaone tofauti kwa sababu tu ya utofauti wa Kiitikadi!....Nanukuu "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM" - Hayati Mwl.Nyerere.
 
"A new broom sweeps clean, but an old broom knows every corner".
 
Haya mambo ya serikali ya mseto yanatoka wapi jamani?

CCM ikishinda, serikali yao. CCM wakishindwa, serikali ya mseto. What?

Ujanja ujanja tu wa kuwa madarakani kwa migongo ya wengine. The last 25 years wamefanya madudu leo inakuaje tuwaruhusu kwenye serikali kama wakishindwa?

Kwa mtazamo wangu, wakishindwa wakae pembeni. Ila nitampa JK nafasi anayostahili, Cello number 1 Ukonga.

Usiniulize kuhusu BM, EL na mafisadi wengine maana nitawsha moto. Tanzania itajitosheleza kwa maji katika kanda za kati.
 
Haupo serious;

Hilo haliwezekana kwa sababu mbili;

1. Waziri Mkuu ni lazima AWE MBUNGE WA KUCHAGULIWA(sio kuteuliwa au viti maalumu)
2. Kikwete atakuwa ni RAIS wakati Dr Slaa atakuwa ni Katibu Mkuu wa Chadema.

Tatizo LENU (I mean "wenzetu" mnaojiunga nasi kwa kasi ya ajabu kadri uchaguzi unavyojongea huku mkiwa na "ajenda maalum") hamtaki kuona wala kusikia sie tunaonyonywa na kukandamizwa na mafisadi tukionyesha kupata mkombozi in form of Dkt Slaa na Chadema.Haiwaingii akilini kuwa mwajiri wenu aliyeingia Ikulu kwa nguvu ya mafisadi anaweza kung'oka Ikulu kama victim wa kukumbatia ufisadi huohuo.

As to wadhifa kwa Mkwere,anapaswa kuungana na Liyumba na Babu Seya.They would have some old scores to settle.
 
Unauliza ujasiri anaupata wapi? Angalia ni lini kajiunga

Masonjo
user-online.png
Junior Member Join Date Sun Aug 2010
Posts 6
Thanks : 1
Thanked 0 Times in 0 Posts

Tunafahamu mtakuja kwa mamia kwa kulipwa ujira wa kudhalilishwa. Mtaondoka vichwa chini. This is JF.
Mkuu,kumbe tuko wengi tuliowashtukia!
I think kuna umuhimu wa kuanzisha a name-and-shame initiative.Yani mara baada ya Chadema kumtangaza Dkt Slaa kumekuwa na kasi kubwa ya "wenzetu" kujiunga na JF,which could have been cool if they were not sent on a mission by mafisadi.Wanahaha kweli,na japo hadharani wanaweka brave face kuwa JK atashinda ( na hivyo wao kuendelea na ajira zao za Usalama wa Mafisadi zilizopatikana kifisadi pia) lakini ni dhahiri kwamba wamepatwa na mchecheto.

Na waje zaidi na zaidi.All of sudden JF imekuwa kimbilio kwao ilhali ni haohao waliotamani kuiona ikifungiwa.Wataumbuka as they did when they couldn't stop JF in the first place.
 
Kwa wale wote wenye akili tumegundua mtu anayetumia jina la masonjo humu ndani ni malaria sugu amejibadili kuficha aibu, kama una hoja endelea na jina lako la zamani ms, usiogope kivuli chako.
 
Noted
 
Waziri wa Michezo, Utamaduni, Maafa na Harambee
 
Sidhani kama President Slaa atamhitaji JK kwenye cabinet yake. Hana sifa yoyote ya kumfanya awe waziri. Labda ampe u-DC au sanasana mkurugenzi wa sanaa na michezo ili ashughulikie vizuri promotion ya Bongo Flavor.

Umesahau na Miss Tanzania kama mjomba Lundenga.
 
tanzania hatuna sheria za majority. tunatumia kanuni ya winner take all... na hivyo kupotezea kabisa uwezekano wa kuundwa kwa serikali tajwa.

leo kikwete amempa mh dk slaa cheo gani kwa utumishi uliotukuka aliowafanyia watanzania? sasa kwa nini yeye apewe nafasi yoyote?
 
Back
Top Bottom