Mkuu hakuna guarantee kwenye siasa...Nani alijua mabadiliko makubwa ya siasa za Kenya mwaka ule 2002.Yale yaliyotokea Kenya yanaweza kutokea mahali popote.Watanzania wa leo (2010) wameamka na kila mtu anashiriki siasa.Rais Kikwete na Utawala wake wanalijua hili.Ngoja baada ya NEC ya 14/August (Mchujo wa Wagombea Ubunge) ndio utaungana na watanzania wengine kujua kuwa mabadiliko yanawezekana.Kumbuka wale akina Lipumba na Dr.Slaa si watu tofauti ni watanzania kama Mimi na Wewe,kwa maana hiyo tusiwaone tofauti kwa sababu tu ya utofauti wa Kiitikadi!....Nanukuu "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM" - Hayati Mwl.Nyerere.