Nafasi ya Kikwete katika serikali ya Slaa? Kutembelea dunia nzima na kujitambulisha tena kuwa urais wake umekwisha.
Kwa wale wote wenye akili tumegundua mtu anayetumia jina la masonjo humu ndani ni malaria sugu amejibadili kuficha aibu, kama una hoja endelea na jina lako la zamani ms, usiogope kivuli chako.
Alichokisema Kikwete kinaitwa hekima.
Kikwete anajua na watanzania wote wenye mawazo yasiyo na ulevi wa upenzi wanajua kuwa Kikwete atashinda, kuingia kwa Dr Slaa kumeongeza msisimko wa sintafahamu ya nani atakamata nafasi ya pili.
CCM haitatawala milele, ila 2010-2015 bado haina kizuizi.
Mkuu hakuna guarantee kwenye siasa...Nani alijua mabadiliko makubwa ya siasa za Kenya mwaka ule 2002.Yale yaliyotokea Kenya yanaweza kutokea mahali popote.Watanzania wa leo (2010) wameamka na kila mtu anashiriki siasa.Rais Kikwete na Utawala wake wanalijua hili.Ngoja baada ya NEC ya 14/August (Mchujo wa Wagombea Ubunge) ndio utaungana na watanzania wengine kujua kuwa mabadiliko yanawezekana.Kumbuka wale akina Lipumba na Dr.Slaa si watu tofauti ni watanzania kama Mimi na Wewe,kwa maana hiyo tusiwaone tofauti kwa sababu tu ya utofauti wa Kiitikadi!....Nanukuu "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM" - Hayati Mwl.Nyerere.
Haupo serious;
Hilo haliwezekana kwa sababu mbili;
1. Waziri Mkuu ni lazima AWE MBUNGE WA KUCHAGULIWA(sio kuteuliwa au viti maalumu)
2. Kikwete atakuwa ni RAIS wakati Dr Slaa atakuwa ni Katibu Mkuu wa Chadema.