Dr Slaa aliwahi kuonesha resprocal obligation Tujifunze kwake lakini pia asipoteze karama hiyo

Dr Slaa aliwahi kuonesha resprocal obligation Tujifunze kwake lakini pia asipoteze karama hiyo

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Resprocal obligation !

Kwa kiswahili rahisi sana hili ni jukumu "nenda rudi"

Dr Wilbrod Slaa aliwahi kuwa padre wa kanisa katoliki na baadaye akaomba kuondoka kwenye upadre kwa mujibu wa taratibu za Kanisa na baadaye akaruhusiwa "kuacha" upadre japo ukishakuwa padre kamwe haiwezekani kuwa mwingine.

Pamoja na yote aliruhusiwa kuacha upadre na hatimaye akaingia kwenye siasa rasmi. Baada ya kuingia huko ni wazi Kanisa(Kwa maana ya uongozi na waumini) lilikuwa na mashaka mazito.Mashaka haya yalihusu iwapo ataanza kutoa siri za altareni na parokiani kwa jamii ?

Nilichofurahia na kilichoendelea kuijenga imani yangu ni kuwa hakuwahi kutoa siri ya upadre au kanisa.Alifanya vyema na alinipendeza sana na hakika umma wa watanzania ulifurahia sana huduma yake katika upya na kumuona sio padre bali ni mwananchi mzalendo na mtanzania anayeipenda nchi yake.

Dr Slaa alipoona kuwa Chadema inataka kukengeuka mwaka 2015 na kumteua Mzee wa mabadikiko aliamua kuondoka chadema na akatoa sababu za msingi sana ambazo kila mwenye uelewa alizielewa na hivyo alibakia kuwa kama shujaa wa watanzania wazalendo.Alipotoa press conference pale Serena aliongea mengi kwa uchungu na aliainisha sababu za msingi kwa nini ameachana na ukatibu mkuu wa chadema in a fairly manner.

Mashaka makubwa yaliibuka kwa wanachadema ambapo walihisi angetoa hadharani mabaya ya kificho yaliyokuwa yanafanyika humo.kamwe hakufanya hivyo ...Resprocal obligation ilimuongoza.
Hatimaye John Pombe Magufuli aliingia madarakani na akapitia mafaili,akakumbuka uzoefu wake na akasikia mwangwi wa nchi na hivyo akamteua kuwa balozi.

Baada ya Kifo cha Magufuli Dr Slaa akastaafishwa ubalozi lakini kwa heshima kubwa hakuja kwenye media kulalamika au kutoa siri alizobebeshwa akiwa katika nafasi hiyo licha ya kuwa kuna wakati aliibuka kukemea issues mbalimbali kama mwanasiasa mkongwe ikiwemo swala la DP WORLD.

Hivi karibuni Dr wilbrod Slaa anaibuka tena akichagiza mjadala ulioanzishwa na PolePole ...nikiona kama vile anataka kwenda kwenye muelekeo wa kuivunja kanuni ile muhimu ya Resprocal obligation.

Hapa nimeona ni vyema nikamjadili yeye na muelekeo wake kwa kuwa ana uzoefu mkubwa sana katika kanisa (aliwahi kuwa katibu wa TEC) ,ana uzoefu wa pekee kwenye siasa za Tanzania na kanisa na uzoefu wa kibalozi.
Zaidi ana watu wengi nyuma yake kwani aliwahi kugombea Urais wa Tanzania.

Je kama mzee muhimu kwenye Taifa,Chama cha mapinduzi,Chama CHADEMA na Kanisa Katoliki na itifaki ya kimataifa anasimama wapi na hii principle Resprocal obligation?

Anapomuona kijana wake Humphrey PolePole akijaribu kukiuka hii principle anamuasa nini?
kwa leo ni hayo tu...naingia mtaani kusikia vifijo ,nderemo na vilio vichache baada CCM kuwatangaza wagombea wake.

CIAO!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Great Philosophy,Patiency,Persistance,Persevearance are the order of the game!
 
Back
Top Bottom