wapiga kura mil 19.7 (source nec), Dr slaa kapata kura nyingi halali (ushaidi: mabomu yaliyopigwa nchi nzima mfano dar, mwanza, Arusha, mbeya, kigoma, kilombero, shy nk). kikwete kapata zilizobaki,nyingi zikiwa ni za kuchakachua. NEC itamtangaza kikwete rais wa JMT, what a waste of time and resources! maisha yataendelea hivyo hivyo kama yalivyokuwa kabla ya uchaguzi,wanaofuraia au kupinga wizi wa ccm wote tupo jahazi moja la ufukara, elimu mbovu, matihabu hafifu, umeme wa mgao, usafiri mbovu nk. Kama wewe unanufaika na ufisadi na unaakili angalau kidogo tu zaidi ya bata, jiulize unafurahia nini, je ni kuendesha benzi kwenye mitaa ya vumbi isiyo na taa ndani ya jiji kuu la nchi liitwalo dar? je nikumiliki nyumba ya mabilioni lakini ndani ya geti unakisima cha maji au septic tanks sababu hayo ya bomba hayaaminiki na jiji halina drainage system? je ni kumpeleka mtoto wako shuleni na hela za kununua chips maana shule haitoi lunch kwa wanafunzi wa shule za misingi? je ni kukimbilia india kutibiwa sababu nchi yako ni duni kifikira na haiwezi kutibu wananchi wake yenyewe? je ni kuwaona ndugu zako uliowaacha uswekeni bado wakitembea pekupeku bila viatu, wakiishi ndani ya nyumba za udongo na vikoroboi/vibatali? je ni kuwaona raia wema na heshima zao wakigombania dala dala au wale wanaotembea kwa miguu kwa sababu hawezi kulipa nauli?