Bullet
nilazima ujue kutofautisha tafiti za kisayansi na polls za media, hivi unajua ni watanzania wangapi wanaishi vijijini na hawana access na hizo media polls, ni aibu mkuu
Ukipita maeneo ya mijini na kuhoji watu hasa wasomi asilimia kubwa watakuambia wanataka upinzani, lakini je niasilimia ngapi kulinganisha na wa vijijini ambao wao CCM ni kila kitu,
Upinzania wanashindwa kuelewa nguvu ya CCM ipo wapi ili hali wanajua fika, Nguvu ya CCM ipo vijijini ambapo watu wakiamua wanaamua kweli na ndio maana hata hao wapinzani sehemu walizo shinda nyingi ni vijijini maana ukiwaelimisha wanakuelewa kweli na si kama mijini ambapo wapinzani wamepatolea macho na wanashindwa kupata majimbo mengi mijini.
Hivyo basi polls za media hazina ukweli wowote kitaalamu maana unaweza kuvote hata mara 100 ukiweza
Na kila chaguzi mambo huwa hivi hivi, kauli za watz waleo sio wa jana, wameamka nk. lakini mwisho wa siku matokeo ya tafiti kama za REDET ndio yanayotoa picha halisi ya matokeo ya uchaguzi