Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dr Slaa kweli ni mkombozi. Mungu ni mwema
13. Kawe, 14: Ulanga kwa Prof. Mlambiti,
Ninalia machozi ya furaha. Ninamfurahia Mungu wangu, nawafurahia watanzania, namfurahia rais wangu mpya Dr Slaa kwa kujitoa na kukubali kuwaongoza watanzania kama rais. Mheshimiwa rais Dr Slaa tunakuahidi watanzania, nitaitumikia nchi yangu kwa moyo wangu wote. Tulihitaji rais anayeipenda nchi na watu wake kutuongoza ili tufanye mapinduzi ya maendeleo katika nchi yetu. Mheshiwa Dr. Slaa ninaiona roho yako na moyo wako unavyoipenda nchi yetu. Umemwomba Mungu akujalie busara kuiongoza nchi yetu nasi watanzani tunazidi kumwomba Mungu akupatie afya njema ya mwili na roho utende kadiri ya kiu uliyonayo ya kuwahudumia watanzania kwa upendo. Kweli Mungu anaweza. Nakosa maneno ya kuongea kwa furaha kuu niliyonayo.
Tunajua unajukumu kubwa la kutuongoza na kuponya majeraha katika nchi yetu. Majereha yaliyosababishwa na uchu wa madaraka wa CCM uliojengwa katika tamaa za ufisadi hadi kutaka kujenga mifarakano inayohatarisha umoja wetu kama nchi. Dr. Slaa unapoanza jukumu jipya la rais wa nchi rudisha umoja wa watanzania uliojeruhiwa na CCM. Asante Mungu, asante Dr. Slaa.
Mtazamo chanya wakati ambapo JK na timu yake ya NEC wanachakachua kura za thamani zilizopigwa na watanzania waliochoka na CCM na ufisadi wake; kura zilizopigwa ili kumuinging Dr Slaa madarakani. Shukrani hii kwa Dr Slaa ni sala ya pekee ya imani kwa ajili ya kuhakikisha uchakachuaji haufanikiwi. Tuombe bila kukoma, ili uchakacuaji unaoendelea hivi sasa usifanikiwe.
MUNGU ibarikin Africa; MUNGU ibariki Tanzania na CHADEMA! Amen!
Kiongozi wa kweli huitwa na watu awatumikie , dr slaa aliitwa akaomba ridhaa ya wana wa karatu wakakubali kutupa watanzania zawadi ya kiongozi wa ukweli. Wabarikiwe sana wooote, wanazuoni, wana wa karatu na watanzania kwa ujumla. Mungu bariki taifa letu tanzania.
Amen
Mtazamo chanya kama huu unanenepesha mifupa na kuleta faraja na matazamio ya namna ya pekee; hii ni sala ya namna ya pekee inayotolewa na wazalendo wa nchi hii wakati ambapo ni dhahiri timu ya NEC imeshaanza kuchakachua kura za watanzania kwa Dr Slaa na watanzania. Tuendelee kumlilia MUNGU ili muujiza wa namna fulani utokee, mafisadi waaibike.
MUNGU Ibariki Afrika MUNGU Ibariki Tanzania; MUNGU Kibariki CHADEMA!
matokeo bado hayajatangazwa!